Gari la BATCO latumbukia mtoni, mtu mmoja afariki dunia na 25 kujeruhiwa

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
GBORBi1W8AAY25A.jpg

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya gari la abiria la kampuni ya Batco linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mahaha wilayani Magu linadaiwa kusombwa na maji mapema asubuhi wakati dereva akijaribu kuvuka daraja la Mto Simiyu.

Afisa Habari wa wilaya ya Magu amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uongozi upo njiani kuelekea eneo la tukio.

Taarifa zaidi zinafuata.

---- UPDATE----

Mtu Mmoja amefariki Dunia na wengine ishirini na tano kunusurika kufuatia ajali iliyotokea katika mto Simiyu Wilayani Magu Mkoani Mwanza baada ya basi dogo aina ya Tata kampuni ya Batco iliyokuwa inatokea Wilayani Bariadi kuelekeka Jijini Mwanza kuacha njia na kutumbukia ndani ya mto huo.
 
Basi ilo linalofanya safari zake kati ya mwanza kwenda musoma limepata ajali asubuhi ya Leo kwa kutumbukia kwenye daraja la simiyu

Taarifa mpaka sasa ni kondakta na watoto wengi wamekufa kutokana na kuzama kwa basi hilo na shughuli ya uokoaji unaendelea.
 
Ina maana hakuna rekodi ya majina ya abiria waliopanda kwenye gari hilo?

Na hilo daraja linahitajika maboresho maana ni pafinyu mno (narrow bridge).
 
View attachment 2841394
Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya gari la abiria la kampuni ya Batco linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mahaha wilayani Magu linadaiwa kusombwa na maji mapema asubuhi wakati dereva akijaribu kuvuka daraja la Mto Simiyu.

Afisa Habari wa wilaya ya Magu amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uongozi upo njiani kuelekea eneo la tukio.

Taarifa zaidi zinafuata
hiyo kampuni aisee nayachukia mabasi yake. hasa yanayoenda tarime mwanza, hayana haraka na sisi watu wa kanda maalum tunapenda mambo yaende faster.
Mungu awasaidie majeruhi na kuwapa faraja ndugu wa victims wote
 
Aisee nikiangalia hayo maji naona mto una kina kirefu kupona hapo ni majaliwa ya Mungu tu si vinginevyo...
 
if you make it in Africa , you can make it anywhere . Infrastructures should be our priority . MAMA YUPO BUSY NA V8 NA SIASA SAFI . Pathetic 🚮🚮 government
Sasa kuanguka kwa hilo basi kuna link gani na raisi. Wakati mwingine mumuonee huruma yule mama. Uzembe wa dereva unamungiza raisi kmnyko.
 
Sasa kuanguka kwa hilo basi kuna link gani na raisi. Wakati mwingine mumuonee huruma yule mama. Uzembe wa dereva unamhingiza raisi kmnyko.
Mkuu unaweza kutukana maana naona bus ndio limetumbukia Mtoni daraja wamesimama watu halina tatizo sasa hata haieleweki ilikuaje likatumbukia mtoni huku daraja likiwa sawa halijavunjika...
 
Back
Top Bottom