Ndugu Mlenge,
Umeniuliza 25% au 1/4 ni ya kitu gani, si ndiyo eeh?
Nilivyokuelewa = ni ya jumla ya michango ya mstaafu ktk muda wake wote wa utumishi + mchango wa mwajiri kwa kuzingatia kanuni ya kukokotoa mafao hayo.....
Kama nimekosea/sijaelewa, niko tayari kueleweshwa zaidi na zaidi.....
Ni ndiyo, ndugu Kitaturu.
Jumla ya michango (ya mtumishi + ya mwajiri) haina uhusika wowote katika kuamua mafao ya mtu aliyechangia kuanzia miaka 15. Mafao ya pensheni ni kama bima ya kumsaidia mtu asiadhirike (fainali) uzeeni. Mafao ya pensheni si kama akaunti ya benki. Mafao yanaangalia vitu viwili tu:
1.
Amechangia kwa muda gani? [Idadi ya Michango]
2.
Mshahara wake wa mwisho ulikuwaje? [
Wastani wa Jumla ya Mishahara ya Mwaka Mzima, (ukiangalia mishahara mikubwa aliyowahi kuipata kwa miaka mitatu, katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho kabla kustaafu)].
Lengo ni kumfanya mstaafu apate angalau mshahara angalau unafanana na mshahara wake wa mwisho kila mwezi mpaka atakapofariki.
Ukitaka kupata amani moyoni, chukulia michango unayopelekewa kwenye mifuko ya pensheni ni sawa tu na michango yako unayopelekewa kwenye mfuko wa bima ya afya: ni kama ada ya uanachama na siyo amana kama za kwenye SACCOS au benki.
Mwisho wa mwaka huendi NHIF kusema, mmekata mshahara wangu mwaka mzima, na mimi sijaumwa. Nirudishieni
hela zangu! Kwenye mafao ni hivyohivyo. Cha kuzungumzia ni muda wa kuchangia, na ukubwa wa mshahara wako wa mwisho. Na pensheni utakayolipwa kila mwezi. Chukulia malipo ya mkupuo kama "retro-rockets" za kukuwezesha kupata "soft-landing" kuingia kwenye kustaafu.
Je, kipi unapenda:
A. Mafao ya mkupuo makubwa, pensheni ya kila mwezi iwe ni kama utani (nauli ya kwenda kuyachukua toka kijijini kwenda wilayani ni kubwa kuliko mafao)
B. Pensheni ya kila mwezi ni kubwa (si haba, yanakuwezesha kupata rizki ya kila siku), mafao ya mkupuo kama haya?
Kama wewe tayari umeshastaafu, bila shaka jibu lako ni B. Kama bado kustaafu jibu la wengi ni A.
Hapa tunafikia kwenye maamuzi ya kifalsafa:
1. Je, mstaafu apewe hela
zake zote, kwa mkupuo, na halafu apambane na hali yake akizitumbua vibaya? Ni mtu mzima mwenye akili timamu.
Hela zake, kwa nini mtu aanze kumpangia matumizi? Mpe chake, asepe!
Mbele ya safari kelele zote za kusema pensheni ya kila mwezi ni ndogo mno, haiendani na uhalisia, nk. ZIPUUZWE.
2. Je, kujiunga kwenye mifuko ya pensheni kuwe ni
hiari au lazima?,
Kwa hiyo, 25% ni ya kwa kile ambacho mfuko unakadiria kuwa ni gharama itakazotumia kumpa hifadhi ya jamii
mwanachama wa mfuko. Hiyo 25% siyo ya robo kwa yale mafao ya mkupuo.
Kama ulimsikia mwenzio alipata 100m wakati anastaafu, ina maana bado na wewe utapata hizohizo, kama sifa zenu zinafanana. Kwa vile mifuko mingi ilikuwa inatumia 25% kwa miaka mingi.