Mkurugenzi Mbeya: Wafanyabiashara wanatumika tu!

Mkurugenzi Mbeya: Wafanyabiashara wanatumika tu!

Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi huyo amedai wafanyabiashara wanatumika tu kuna watu wapo nyuma ya hayo maandamano na vurugu! Wakati huo huo Kandoro amewapiga mkwara wanaoleta vurugu kuwa watakutana na mkono wa sheria.Watu zaidi ya 200 wamekamatwa huku watu 12 wakiwa wamejeruhiwa watano wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi,Polisi wawili wamejeruhiwa pia!

Kiongozi yoyote asiyekuwa responsible uwa anatafuta sehemu ya kuficha uovu wake.....aiingii akilini kusema kuwa wafanyabiashara wanatumiwa wakati wewe utimizi wajibu wako...ni lini serikali itaacha kusingizia udhaifu wake kuwa ni CDM? japo ajasema kuwa ni CDM lakini najua anamaanisha hivyo. Lakini pia nawapa eko CDM kama wameweza kuwavuta wanachi wakawasikiliza namna hii.....well done CDM kama ni kweli!!!
 
Biashara bila mpangilio ni vurugu. Ni vema washanyabiashara ndogondogo wakafuata taratibu zilizowekwa kwa sehemu za kuweza kufanya biashara zao. Hii ya kupanga biashara zao hadi barabarani sio sahihi kabisa zaidi ni bugudha kubwa kwa watembeo kwa miguu na sio salama hata kwao wenyewe.

Mkuu Ni Utaratibu gani unaotaka kufuatwa? Viongozi wetu wabaya sana Mkuu na wamewaonea hawa jamaa kwa Muda Mrefu sana! Hawa jamaa walijenga Machinga Complex halafu wakajigawia wenyewe vile vyumba vya Biashara sasa wanawapangishia Wamachinga kwa bei ya Ulanguzi. Mkuu hata paka ni Mnyama mpole sana lakini ukimuweka kwenye kona atakurarua tu.
 
Hebu weka upunguani wake hapa...

huu hapa:
mosi: hauwezi kuwatowa wamachinga sehemu wanayopatia kipato bila kuwaonyesha wapi waende.
Pili: kusema wamachinga wanatumika wakati wanadai haki yao.
Tatu: hawajui watu wa mbeya vizuru kuwa hawataki watu wababe(kama unakumbuka walimpiga mkwele na mawe)
mwisho: kutumia nguvu nyingi, pesa nyingi kwa kitu ambacho angeweza kukaa mezani na wamachinga na kumaliza.
 
Its common sense ukimuondoa mtu mahala kama unamjari muoneshe pa kwenda!
Huitaji kuwa ccm au cdm kujua hayo
 
Polisi waendelee kutoa kipigo kikali na kuwakamata wale wote wanaofanya vurugu.nchi hii hatuwezi kuona inavurugwa na wanasiasa kwa uroho wao wa madaraka.Rais ni KIKWETE CDM wanapaswa kufaham hilo waache kuratibu vurugu hapa nchini za kumuondoa J.K madarakani.

Ebu nikumbushe lini CDM walimtambua Kikwete? Walishamjulisha kwa vitendo walipomsusia hutuba bungeni Yeye ni rais wa mafisadi labda na wewe kama ni fisadi.
 
Polisi waendelee kutoa kipigo kikali na kuwakamata wale wote wanaofanya vurugu.nchi hii hatuwezi kuona inavurugwa na wanasiasa kwa uroho wao wa madaraka.Rais ni KIKWETE CDM wanapaswa kufaham hilo waache kuratibu vurugu hapa nchini za kumuondoa J.K madarakani.
I fkn second that!!
 
kaka unachosema ni sahihi hata mmachinga ukimkuta anasema wanipangie sehemu niitakayo nitakwenda bila shuruti. Lakini tatizo la watawala wanataka kuwaondoa wa2 kwa nguvu aka ubabe bila kuwaonesha wapi waende.
Kama wamachinga wanasema hivyo, hii ni hatua nzuri sana katika suala zima la kupanga mji. Hivyo ni jukumu la Halmashauri yao kuona wafanyabiashara hao watapewa eneo lipi lilio salama kwao na kwa wateja wao.

Ukiangalia kwa juu juu ama kwa haraka haraka pale Mwanjelwa hakuna nafasi hiyo kwa wingi wao. Hii ni challenge kwa Halmashauri yao, aidha tabia ya Umachanga ni kufanya biashara kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu. Iwapo hakuna nafasi hiyo, wanaweza kabisa kuwaacha hapo hapo na kuwashauri kufanya biashara zao katika siku kadhaa tu katika wiki, mfano kama biashara za product za mashambani pale Kiwira.
 
chadema unscrupulous politicians are conspiring with bandits to launch violent demonstrations in order to confront the ruling party from implenting its election manifesto. We have recently witnessed a series of manipulated rallies and demonstration which are engineered for the purpose of making it difficult for the government to execute its development duties. As a result the government is now unnecessarily forced to relocate its budget funds and commit them to expenses incurred by security forces while dealing with chadema violent protesters which in turn will have a disastrous effect to the country's economy wellbeing. As far as i can see, i still believe that chadema leaders are capable of helping our government to build our country's future and can do better than choreographing needless rallies and demonstrations which are of no help to an average citizen.

shame on you!!!!!!!!
 
Kinachosikitisha ni kwamba kama mkurugenzi anatoa kauli kama hizo mbele ya mkuu wa mkoa basi ujue hawanampango wa kutatua hilo tatizo! Serikali ya kipuuzi sana hii' maeneo kibao wanawahamisha watu ili wawapishe wawekezaji,sasa wanashindwa nin kutafuta maeneo mazuri kwa wamachinga ili wafanye biashara zao vizuri?!
 
kichwa boga sasa chadema wameingiaje au kazi yenu nikuipaisha cdm shem on u magambaaz

Ngoja nikwambie! Kandoro anawakilisha CDM so baada ya CDM kumwambia awahamishe wale walala hoi pale akaenda kuwahamisha. Walala hoi wakastrike! So kwa kupitia inteljensia wakagundua kuwa nyuma ya hawa machinga kuna CDM na soon watagundua kuwa Kandoro ni mmoja wa walioanzisha hizo vurugu.
 
Kama wamachinga wanasema hivyo, hii ni hatua nzuri sana katika suala zima la kupanga mji. Hivyo ni jukumu la Halmashauri yao kuona wafanyabiashara hao watapewa eneo lipi lilio salama kwao na kwa wateja wao.

Ukiangalia kwa juu juu ama kwa haraka haraka pale Mwanjelwa hakuna nafasi hiyo kwa wingi wao. Hii ni challenge kwa Halmashauri yao, aidha tabia ya Umachanga ni kufanya biashara kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu. Iwapo hakuna nafasi hiyo, wanaweza kabisa kuwaacha hapo hapo na kuwashauri kufanya biashara zao katika siku kadhaa tu katika wiki, mfano kama biashara za product za mashambani pale Kiwira.

kaka hii kitu walishawahi kuzungumza na wakashauliana wafunge barabara ile ya makunguru mwanjelwa ndo wamachinga wakae hapo. My be walikuwa wanapima upepo kama wanaweza kuwatowa kwa nguvu.
 
Mkuu Ni Utaratibu gani unaotaka kufuatwa? Viongozi wetu wabaya sana Mkuu na wamewaonea hawa jamaa kwa Muda Mrefu sana! Hawa jamaa walijenga Machinga Complex halafu wakajigawia wenyewe vile vyumba vya Biashara sasa wanawapangishia Wamachinga kwa bei ya Ulanguzi. Mkuu hata paka ni Mnyama mpole sana lakini ukimuweka kwenye kona atakurarua tu.
Unapozungumzia viongozi, na hasa katika halmashauri, ni kuanzia ngazi ya Udiwani. Leo diwani anaitwa mheshimiwa. Hapa tayali amejiweka mbali sana na wananchi wake, hivyo ni rahisi sana kufanya ufisadi wa namna hiyo.

Njia kubwa na rahisi kufanya hivyo inatokana na nafasi yake katika halmashauri, pamoja na kushirikiana na viongozi wa Wamachinga. Kwa hili nakubaliana nawe, hata hivyo hatua zozote za halmashauri kwa wakaazi wake huendana na utoaji wa notice. Hii umfanya mfanyabiashara huyo kujua kuwa hatakiwi kuwepo eneo husika. Kinachoonekana hapa ni ufanyaji biashara holela, na usipodhibitiwa unaweza kuwa na madhara makubwa kama tunayoyaona leo kutokana na ujenzi holela katika miji yote ya Tanzania.
 
Mkuu Kibunango nimekuelewa ila katika kuwahamisha Wamachinga mambo yafuatayo lazima yazingatiwe

1. Lazima Serikali itenge eneo ambao litafikika kirahisi na watu wengi ili kuwahakikishia wamachinga kwamba watauza Bidhaa zao. Kwa mfano kwa Mbeya kulikuwa na Mpango wa Kuihamisha stendi ya Kabwe na kuipeleka Maeneo ya Uwanja wa Ndege hilo lingefanyika Sambamba na kuwahamisha Wamachinga

2. Kuwe na MoU kati ya Serikali na Wamachinga kwamba eneo wanaloenda hawasumbuliwa tena baada ya Muda Mfupi na kama Serikali itataka kuwaondoa basi iwalipe Fidia kubwa. Wamachinga wamekuwa ni watu wanaotengeza eneo la Biashara kwa maana kulifanya soko liwe Maarufu na Mara zote soko lilipopta Umaarufu Serikali imekuwa ikiwaondoa Wamachinga kwa kisingizio cha kujenga Soko la Kisasa ambalo linakuwa haliwafaidishi Wamachinga, Mifano iko mingi mkuu

Kwa hili suala la Mbeya namlaumu sana Kandoro kwa sababu ameingia akatangaza Kuwanyoosha watu wa Mbeya hii nadhani ikawajenga watu wambeya kumuonesha kwamba Hawezi kuwanyoosha. Viongozi wetu wakishakuwa wanalindwa na Polisi wanatembea na Ving'ora huwa wanajishahu
 
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi huyo amedai wafanyabiashara wanatumika tu kuna watu wapo nyuma ya hayo maandamano na vurugu! Wakati huo huo Kandoro amewapiga mkwara wanaoleta vurugu kuwa watakutana na mkono wa sheria.Watu zaidi ya 200 wamekamatwa huku watu 12 wakiwa wamejeruhiwa watano wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi,Polisi wawili wamejeruhiwa pia!
......nchi imechoka, watawala wetu wamechoka, wateule hawa, wateule wa bwana mkubwa, hawawezi tena kufikiri, wanatoa majibu mepesi, tusiwalaumu sana, pengine ni majibu ambayo bwana mkubwa anapenda kuyasikia. Hawamsaidii Rais wetu, wanafikiri ili washibe tu; Rais wangu Kikwete (hata kama sikukupigia kura), vijana hawa wamechoka, wamepoteza matumaini ya maisha bora, hawana uhakika wa kula, wengi wao hawawezi hata kujiajiri, inapotokea fujo kama hizi, wanashangilia wanabaka mali za wananchi wenzao, hivyo wanatumika na adui hawa, maisha magumu na kukosa matumaini ya kuishi , cdm hawana mkono hapa, kama hoja hii ipo ni ya kishabiki tu, haina mantiki, Ritz, Ngongo, Twahil (kwa uchache), tuache ushabiki, tutangulize uzalendo, tumsaidie Rais wetu.
 
Huyu mkurugenzi atakuwa chokonoko. Mwizi mkubwa
 
Huyu mkurugenzi atakuwa chokonoko
Ukisema hivyo ina maana Madiwani wote wa Halmashauri ya Mbeya mjini pamoja na Mbunge wao ni chokonoko (sijui una maana gani hapo). Kumbuka Mkurugenzi ni mtekelezaji wa maamuzi ya Madiwani.
 
Back
Top Bottom