Nadhani nawe umefikia mwisho wako wa kufikiria au nawe pia ni sehemu ya mfumo kandamizi. Hakuna sehemu CDM waliwahi kusema manahitaji kumwondoa KIKWETE madarakani na wanatambua kuwa yeye ni Rais. Kinachojitokeza ni uvivu wa kufikiria wa viongozi wetu na kushindwa kutatua matatizo ya wananchi, ndiyo maana kiongozi mmoja mkubwa sana aliwahi kusema hajui matatizo ya watanzania yanatokana na nini na bado yuko pale pale akiendelea kutumaini atawasaidia watanzania kuondokana na shida zao ambazo hajui chanzo chake ni nini!!!!. Tuache unafiki wa kudhani kila demonstrations zina wanasiasa nyuma yake, tushughulikie matatizo ya watanzania, vinginevyo huu ni mwanzo tu, tutegemee vurugu nyingi zaidi na zaidi!!!!!.