Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo komesha hii tabia

Embezzler

JF-Expert Member
Sep 8, 2023
1,874
4,658
Kipindi cha Magufuli watumishi wote walihakikiwa na walioonekana hawana vigezo walitimuliwa. Wakati wa kuhakikiwa kila mtumishi alileta vyeti halisi, barua ya kuajiriwa na ya kudhinitishwa. Vyeti vya ndoa, kuzaliwa/affidavit n.k.

Pamoja na nakala za vyeti vyote na barua zote kuwa kwenye faili la mtumishi lakini kila mwezi watumishi wanaambiwa wapeleke vyeti na barua zote mpaka za kupandishwa madaraja Kama vile vitu hivyo haviko kwenye mafaili hapo manispaa.

Jana Tena watumishi wameambiwa wapeleke barua zote na vyeti. Kwanini Ubungo wanahakiki watumishi kila mwezi, kwanini wasitumie mafaili yaliyoko ofisini au komputa ambazo zipo pale?

Kwanini Hawa kina Mndeme, Mtoi na Mary wasitumie mafaili kutafuta tafuta watumishi?
 
Back
Top Bottom