Mkurugenzi Halmashauri ya Masasi asimamishwa kazi kwa Ubadhirifu aliofanya Tarime Vijijini

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Apoo Tindwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kusaidia maendeleo kwa jamii (CSR) kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara.

Apoo ambaye kabla ya kuhamishiwa mkoani Mtwara alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime vijijini ambapo pamoja na watu wengine wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Sh5.6 bilioni zilizotolewa na mgodi huo kwaajili ya miradi ya maendeleo katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo uliopo wilayani Tarime.

Bashungwa ametangaza maamuzi hayo leo Mei 6, 2022 katika kijiji cha Genkuru wilayani Tarime baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Genkuru kilichogharimu zaidi ya Sh700 milioni ambacho hadi sasa hakijakamilika licha ya kugharimu kiasi hicho cha fedha, fedha ambazo ni sehemu ya fedha za CSR.

Chanzo: Mwananchi

TAARIFA YA WIZARA

D1175220-4DC5-45DA-8694-024BAE6426EA.jpeg
 
Haya ndo matatizo ya kuhamisha tatizo kwenda mahali pengine.
 
Bashungwa huwa hapepesi macho kwenye maamuzi yake. Wizara ya OR-TAMISEMI imepata mtu sahihi
 
Usemi wao wakileo ni kuwa wanakula kulingana na urefu wa kamba zao.
 
Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Apoo Tindwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kusaidia maendeleo kwa jamii (CSR) kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara.

Apoo ambaye kabla ya kuhamishiwa mkoani Mtwara alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime vijijini ambapo pamoja na watu wengine wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Sh5.6 bilioni zilizotolewa na mgodi huo kwaajili ya miradi ya maendeleo katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo uliopo wilayani Tarime.

Bashungwa ametangaza maamuzi hayo leo Mei 6, 2022 katika kijiji cha Genkuru wilayani Tarime baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Genkuru kilichogharimu zaidi ya Sh700 milioni ambacho hadi sasa hakijakamilika licha ya kugharimu kiasi hicho cha fedha, fedha ambazo ni sehemu ya fedha za CSR.

Chanzo: Mwananchi

TAARIFA YA WIZARA

View attachment 2214432
Watakwambia Jiwe alidhibiti Rushwa saizi watu wanajipimia kwa urefu wa kamba yao. 😂😂😂😂
 
Watakwambia Jiwe alidhibiti Rushwa saizi watu wanajipimia kwa urefu wa kamba yao.

Magufuli alijitahidi kudhibiti kwa kiasi chake japo yeye peke yake asingeweza kuwadhibiti wezi waliojaa serikalini, hasara kubwa iliyobaki ni kwamba hakuacha mifumo ya kudhibiti kile alichopenda kukisimamia yeye

Kwa sasa hali inaweza kuwa mbaya sana kama Rais Samia hatakuwa mkali.
Watu wanakula hela za umma sana Rais akiwa mpole mpole na mifumo ikawa legelege
 
Magufuli alijitahidi kudhibiti kwa kiasi chake japo yeye peke yake asingeweza kuwadhibiti wezi waliojaa serikalini.

Kwa sasa hali inaweza kuwa mbaya sana kama Rais Samia hatakuwa mkali.
Watu wanakula hela za umma sana Rais akiwa mpole mpole
Lugha imebadilika 😆😆,huo wizi haujafanyika awamu ya 6 naomba ieleweke..

Awamu ya 6 ukipiga unachukuliwa hatua nadhani umemsikia PM na Bashungwa last month alichomfanya yule DED wa Mvomero.
 
Lugha imebadilika ,huo wizi haujafanyika awamu ya 6 naomba ieleweke..

Awamu ya 6 ukipiga unachukuliwa hatua nadhani umemsikia PM na Bashungwa last month alichomfanya yule DED wa Mvomero.

Wala siko hapa kutetea mtu nasema uhalisia, ule utata wa Magufuli ulisaidia kutisha wala rushwa lakini bado asingeweza kuwadhibiti wote kwa sababu hapakuwa na mifumo ya kudhibiti zaidi ya yeye kama mtu mmoja wengi waliita one man show ambapo kuondoka kwake mambo yanarudi kama kawaida.

Haya mambo ya awamu sina shida nayo maana hata baada ya Samia watu wa awamu ya 7 watakuwa na maneno mengi kuzungumzia upigaji wa awamu ya 6.
Kama nchi tunapaswa kupata mifumo sio mtu, mtu akiondoka tunarudi kule kule, tukiwa na mfumo nchi itaenda vizuri.
Hawa wakubwa wamewekewa kinga za kutoshitakiwa wala kubughudhiwa wakiondoka madarakani, hii inatugharimu sana watu wanawapa rafiki zao access za kula pesa za umma na hatuna cha kuwafanya.

Fikiri zaidi kuhusu nchi achana na Magufuli, achana na Samia hao wote watapita lakini Tanzania itabaki
 
Ulisaidia vipi ikiwa watu walijua anatishia ila hachukui hatua?

Saizi hutishwi ila ukibainika unalo
 
Mtu ameiba na ushaidi upo badala ya kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi unampa likizo ya kwenda kutumbua pesa zenyewe, Sasa gharama zilizotumika kujenga mahakama ya mafisadi ni ya nini!?
 
Hamna kitu atafanyiwa huyo mkurugenzi. Hii nchi inafaa ipewe heshima yake Duniani, kama moja ya kitovu cha ufisadi wa waziwazi kabisa unafanywa na wanasiasa na hawagusiki.
 
Back
Top Bottom