Mkumbo: Tanzania Iko Tayari kwa Uwekezaji wa Kimataifa

Mkumbo: Tanzania Iko Tayari kwa Uwekezaji wa Kimataifa

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
573
Reaction score
359

London, Uingereza — Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), amewahakikishia wawekezaji wa Uingereza kuwa Tanzania ni nchi salama, yenye uthabiti wa kisiasa na inayoendelea kutekeleza mageuzi ya kina ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Prof. Mkumbo alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza ulioandaliwa na taasisi ya kimataifa ya Clyde & Co, ikiwa ni sehemu ya ziara yake rasmi ya kikazi nchini humo.

Katika hotuba yake, Waziri alisema Tanzania inaanza safari ya kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwa katika nafasi nzuri, kutokana na uthabiti wa uchumi, amani na utulivu wa kisiasa, pamoja na mageuzi yanayoendelea kufanyika ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Alieleza kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika baada ya athari za janga la UVIKO-19, ambapo kasi ya ukuaji imepanda kutoka asilimia 4.7 mwaka 2022 hadi asilimia 5.9 mwaka 2025, huku ikitarajiwa kufikia asilimia 6.3 mwaka 2026. Aidha, aliongeza kuwa kiwango cha mfumuko wa bei kimeendelea kubaki chini ya asilimia 5 kwa zaidi ya muongo mmoja, jambo linaloonesha uthabiti wa mazingira ya kiuchumi.

Akizungumzia mazingira ya uwekezaji, Prof. Mkumbo alisema Serikali inaendelea kuimarisha amani na usalama, kufanya maboresho ya sera za kodi na udhibiti, pamoja na kuongeza uwazi na utabiri wa sera ili kuwapa wawekezaji uhakika zaidi. Alifafanua kuwa kuanzishwa kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA) kupitia kuunganisha taasisi mbili kuwa moja, kumeongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wawekezaji.

Waziri huyo aliainisha pia fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini, akibainisha kuwa Tanzania ina zaidi ya hekta milioni 44 za ardhi yenye rutuba, rasilimali nyingi za madini na nishati, pamoja na nafasi ya kipekee ya kijiografia inayoiunganisha Afrika Mashariki, Kati na Kusini kupitia bandari, reli, barabara na anga. Alisisitiza kuwa Tanzania ina madini 22 ya kimkakati yanayohitajika katika mpito wa nishati duniani.


281326.jpg




Kuhusu uhusiano wa Tanzania na Uingereza, Prof. Mkumbo alisema ushirikiano wa nchi hizo mbili umeendelea kwa zaidi ya miongo sita, ambapo biashara ya pande mbili imefikia thamani ya pauni milioni 650, huku uwekezaji wa Uingereza unaokadiriwa kufikia pauni bilioni 4.89 ukizalisha zaidi ya ajira 131,000 nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Clyde & Co, Bw. Michael Clayton, aliipongeza Tanzania kwa juhudi zake za kufanya mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji, akisisitiza kuwa majukwaa ya majadiliano kama hayo ni muhimu katika kujenga imani na kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali na wawekezaji wa kimataifa.



Akihitimisha hotuba yake, Prof. Mkumbo aliwaalika wawekezaji wa Uingereza kuwa washirika wa karibu wa Tanzania katika kutekeleza Dira ya Taifa 2050, akisisitiza kwa msisitizo:

“Tuko wazi kwa biashara. Tunafanya mageuzi. Tunakua. Na tuko tayari kushirikiana.”
 
Anahutibia kama anaongea na vijana wa UVCCM.
Nimefanya kazi na taasisi mbalimbali za uwekezaji wa kimataifa. Sisi huwa hatutilii umuhimu maneno ya wanasiasa. Makampuni yote makubwa huwa yanafanya uchunguzi yenyewe, husubiri uambiwe na wanadiasa. Na hata kwenye ranking, huwezi kuingiza hotuba za wanasiasa kama kigezo cha kusema nchi hii ina mazingira mazuri ya kisiasa.

Unaua watu zaidi ya 10,000 halafu unadanganya watu kuwa nchi ina usalama na amani!! Very stupid! Unadhani hao waingereza wameshuka leo Duniani toka sayari ya Mars, na hivyo hawajui hali ya Tanzania?
Mahali popote penye brutality, hakuna mwekezaji makini atakuja, kwa sababu nature ya binadamu ni kugomea ugandamizaji. Mahali ambapo watu wanaonewa, kuna siku lazima watariot. Na kukitokea riot, wawekezaji mnakuwa kwenye risk kwani ninyi mnachukuliwa kama mnaoupatia nguvu utawala dhalimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom