Mkulo na Khijjah kumbe walikuwa "wanapiga"!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo na Khijjah kumbe walikuwa "wanapiga"!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by builddontbreak, May 9, 2012.

 1. b

  builddontbreak New Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Vigogo watafuna nchi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][​IMG]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][​IMG]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD] Imeandikwa na Deodatus Balile, Dar es Salaam [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Jumanne, Mei 08, 2012 06:43 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]*Wabunge wawili CCM walipwa fidia Sh milioni 964 bado jengo lauzwa
  *Zitto asema kalinunua Fida Hussein
  *Ataka Katibu Mkuu Fedha ahojiwe
  Wakati Rais Jakaya Kikwete amebadili Baraza la Mawaziri kutokana na shinikizo la Bunge, taarifa zimevuja kutoka serikalini kuwa kuna vigogo na watendaji wakuu wanaouza mali za umma kama zao.

  Mawasiliano ya siri yaliyonaswa na Gazeti la JAMHURI yamebaini kuwa waliokabidhiwa jukumu la kulinda mali za umma - ama wameziachia au kwa makusudi - wameamua zitafunwe na wenye meno.
  Baadhi ya mambo yanakuwa kama sinema. Desemba 2003 Jengo lililokuwa likitumiwa na wakala wa ukarabati wa magari ya Serikali (TMSC), lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kwenye makutano ya Mtaa wa Jamhuri kando ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, liliuzwa kwa aliyekuwa Mbunge wa Mvomero (CCM), Suleiman Saddiq.

  Saddiq alinunua jengo hilo lililopo Kitalu Na 24 kupitia kampuni yake ya Saddiq Super Service Station (SSSS), baada ya kushinda zabuni akiwa na mshirika wake kibiashara, Richard Ndasa, ambaye naye ni Mbunge wa Sumve kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Wawili hawa walishinda zabuni iliyotangazwa na Serikali, lakini baada ya kulipa asilimia 10 ya zabuni yaani Sh milioni 130, waliokuwa wafanyakazi wa TMSC waliamua kufungua kesi mahakamani. Kesi hiyo iliendelea na ilipofikia mwaka 2009, yaani miaka sita baadaye Ndasa na Saddiq waliamua kuihoji serikalini kulikoni jengo hilo hawakabidhiwi na hatima ya fedha zao walizotoa ilikuwa ipi.

  Uchunguzi wa JAMHURI unaonyesha kuwa Wizara ya Fedha kupitia barua mbili - moja yenye kumbukumbu namba TYC/T/200/414/46 ya Aprili 14, 2009 na nyingine TYC/T/200/414/51 - ililiandikia Shirika Hodhi la Mashirika ya Serikali (CHC) kuwataka wasitishe uuzaji wa jengo hilo lenye ukubwa wa kuanzia mtaa mmoja hadi mtaa wa pili karibu na Jengo la Haidery Plaza eneo la Posta Mpya.

  Wizara pia iliwataka CHC kuanzisha mazungumzo jinsi ya kuwarejeshea SSSS gharama walizotoa za Sh milioni 130 kama malipo ya awali na fidia ya usumbufu. Kampuni ya SSSS yenyewe ilitaka irejeshewe Sh bilioni 3.9 kwa biashara iliyopotea kati ya fedha hizo sh milioni 500 zikiwa za usumbufu. Mazungumzo kati ya CHC na SSSS yalikwama.

  Ijumaa Juni 5, 2009 Bodi ya Wakurugenzi wa CHC ilikutana Dar es Salaam kuamua suala hilo bila mafanikio. Waliohudhuria kikao hicho ni Dk. Raphael Chegeni, Peter Bakilana, Methusela Mbajo, Shuma Kissege na Rosemary Tesha.

  Mambo yalitulia hadi Mei 4, 2010 timu ya wataalamu wa Serikali ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijjah, aliyekuwa mwenyekiti wa kikao ilipokutana. Hapa ndipo ulipofanyika uamuzi wa kuitia kitanzi Serikali.

  Wengine waliohudhuria kikao hiki ni Joyce Mapunjo, O. N. Assery, E. Mlaki, M. Kejo na J. W. Hellela. SSSS waliwakilishwa na Sulaiman A. Sadiq (MB) na Richard Ndasa (MB).

  Ingawa taarifa ya CAG inasema haijulikani nani aliyewateua wajumbe wa Serikali kufanya kazi hii, taarifa hiyo inaongeza: "Hatimaye waliamua SSSS walipwe Sh 964,188,491.17 zinazohusisha Sh milioni 130 walizolipa kama malipo ya awali, Sh 334,188,491.17 zikiwa asilimia 20 ya riba tangu Desemba 2003 hadi Aprili 2010 na Sh milioni 500 kama fidia ya usumbufu."

  Kikao hicho kilimwamuru aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao, Khijjah, baada ya kuwa ametia saini na Saddiq makubaliano ya malipo hayo, apeleke nakala ya makubaliano hayo kwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo (wakati huo), pia amshauri iwapo walipe fedha hizo au la.

  Ikumbukwe kazi hizi zilipaswa kufanywa na CHC na Khijjah na Sadiq si waajiriwa wa CHC lakini wakaifanya kazi hiyo. Siku sita baadaye CHC iliwaandikia Wizara ya Fedha ikieleza majumuisho ya maafikiano yaliyofikiwa kwenye kikao cha Mei 4, 2010, wakimuomba Katibu Mkuu Khijjah awasilishe uamuzi wa kikao kwa Waziri wa Fedha. Hapa ndipo sanaa ilipotokea.

  Barua hii ilikuwa inaandikwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Khijjah, ambaye kwa bahati mbaya ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao kilichopitisha malipo hayo. Pili kama zilivyo taratibu, Wizara ya Fedha ilipaswa kuwajibu CHC barua hiyo lakini hadi leo hawajawahi kupewa jibu la barua hiyo.

  La mwisho na kubwa kuliko yote bila kupitia CHC, Wizara ya Fedha iliamua kuwaandikia SSSS hundi safi ya Sh 964,188,491.17 na waheshimiwa wawili waliotajwa ‘wakavuta mkwanja'.

  Ndasa alipohojiwa na JAMHURI alikiri mlolongo huo kufuatwa, ila akasema: "Sisi tulifuata taratibu zote za zabuni na tukashinda, lakini baada ya kuona muda umepita na wafanyakazi wanaendelea kuvutana na Serikali, tukaona hakuna sababu ya kuvutana na Serikali ikitiliwa maanani kuwa sisi ni wabunge wa CCM.

  "Serikali ilitwambia inataka kulitumia jengo hilo kujenga ofisi za Serikali na kupunguza gharama ya kupanga majengo mengine, sisi tukaona hili ni jambo jema. Lakini baadaye tukashangaa kusikia kuwa jengo hili limeuzwa kwa Fida Hussein kwa Sh bilioni 3. Tuliona huu ni uhuni mkubwa.

  "Tuliondoka mimi na Murad (Saddiq) tukaenda kwa Fida Hussein na kumuuliza aliuziwaje jengo hilo, akasema yeye alilinunua mnadani. Kwamba baada ya wafanyakazi kushinda kesi, mahakama iliamuru liuzwe naye akawapo siku ya mnada akalinunua Sh bilioni tatu.

  "Tuliona huu ni uhuni tukaenda hadi Wizara ya Fedha kumuona mtu wa TR (Msajili wa Hazina) anaitwa Masoud, huyu tulivyomuuliza akauma midomo akasema mara Serikali imekata rufaa, hata yeye haelewi vizuri kinachoendelea, tukabaki tunashangaa."

  Gazeti la JAMHURI ilipopiga simu za Murad (Saddiq) na Fida Hussein muda wote zilikuwa zinaita bila kupokewa.

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alisema kilichotokea hakiweza kuvumilika kwani hii ni kuiba fedha za Serikali mchana kweupe.

  "Fikiria serikali imelipa Sh milioni 964 kurejesha umiliki wa jengo, hata kama haikufuata taratibu, lakini pia mbali na fedha hizo kulipwa jengo limenadishwa na mahakama sasa analimiliki Fida Hussein si Serikali… huu ni wizi wa mchana lazima maafisa waliohusika watafutwe ili mali ya umma irejeshwe. Jengo lile lina thamani ya Sh bilioni 15, kiwanja kipo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na ni kikubwa ajabu, wabunge hatutakubali lazima kieleweke," alisema Zitto.

  Hii ni moja ya kashfa zilizoibuliwa na CAG katika taarifa yake ya fedha, iliyowasilishwa katika kikao cha Bunge kilichomalizika Aprili na ripoti hiyo imeonyesha wizi na matukio makubwa ajabu ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

  Kutokana na hali hiyo, wabunge walitishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwa maana kuwa akiondoka Baraza la Mawaziri lingevunjika na hivyo mawaziri wanaotuhumiwa wakaondoka.

  Zitto aliyeanzisha hoja hiyo, alipohojiwa na JAMHURI alisema: "Wabunge tumefanya kazi nzuri, lakini napenda kuwakumbusha kuwa wasijisahau. Moto huu uwe wa kudumu na mawaziri walioteuliwa wajue hawana ‘honey moon' (fungate).

  "Kikao kijacho watapambana na bajeti wakati mawaziri wanaposulubiwa. Wakajipange wachape kazi. Nawapongeza wabunge kwa kazi nzuri waliyofanya na nawataka waiendeleze," amesema.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kumbe Ndassa nae Kibaka?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  ....Kikwete kwenye kashfa kama hizi hunyamaza kimya kabisa kama hahusiki, nitashangaa sana akitia neno kwenye kashfa hii nzito kuonyesha msimamo wake kwenye ufisadi huu.
   
 4. a

  adobe JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  JK huyu ndo alimwambia Mkulo asiwajibike eti atamtetea hadi mwisho ila mwishowe akamkaaanga mchana kabla ya kutangaza mabadiliko hayo ya mawaziri juzi.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ataongea kama kamati kuu ya CCM ikimfuata ikulu imshinikize aseme kitiu..ah mi siku hizi nishazoea kusikia hizi habari...NOTHING SURPRISES ME ANYMORE THESE DAYS
   
 6. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,644
  Trophy Points: 280
  Aiseeeeeeeee...... usaniiii.... Uwiziiiiij wa waziiiiiii..... i feel pain... kamata hawa wote Khijah... Bi Kejo na wengine haraka sana JK do that.... plz
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kikwete angehusika angeruhusu CAG aipeleke ripoti bungeni ikajadiliwe? hayo yote yalikuwepo kwenye ripoti.

  Mmemsakama sana Kikwete, mnarukia jitihada zake kuzifanya hoja zenu kumshutumu, hivi huwa mnafikiri kiukweli>

  Mie naona mnajidanganya kila kukicha. Mngeyajuwa haya kama Kikwete hajampa meno CAG?
   
 8. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  JK? Are you out of your mind. Hamna wa kumfunga paka kengele hapa.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Alijua upepo utakua vilevile kama miaka ya nyuma na sheria inasema lzm report ipelekwe bungeni.
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu hata watoto wake waki peksheni wallet yake hukaa kimya au kutabasamu
   
 11. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tatizo Mawizarani kuzungukana ni kawaida yao huku Watanzania tukiumizwa.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Ukiona general anakimbia uwanja wa mapambano basi jua fika jeshi lishapoteza vita....kashfa kama hizi ndo za kuonyesha maana ya kuwa kiongozi. Ila Tanzania hela ya walipa kodi wala haiogopwi na kuheshimiwa
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Watanzania eeeeeeeeeeh! Nchi imeingiliwa na tauni ya mapanya.
  [Wanatafuna noti - JK 04-05-2012].
   
 14. D

  Dina JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Haya mambo ukiyajua (sikia) ndio moyo unazidi kuuma! Hawa watu mbona wanajisahau hivi jamani? Hivi kuna siku kweli mwanamke wa kijijini atafungua bomba la maji ndani ya nyumba yake kweli?
   
 15. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Jk kabanwa na shughuri za safari za kila siku pia na shughuri za serikali pamoja na chama chake nina hisi hii riport alisoma juju tu hakuingia kwa ndani zaidi akaruhusu isonge mbele . kwa hiyo naye sasa anashitushwa na wingi wa madudu hayo.

  hata wabunge pamoja na kupewa riport hiyo mapema hawakuweza kuisoma yote mpaka wakati wanaanza vikao vya bunge. Ndo maana mpaka leo bado tunaendelea kupata madudu kutoka katika riport hiyo kama hiyo ya hilo jengo. nahisi tutaendelea kusikia mengi. bado unashanga hili linaibuka jingine
   
 16. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  JK hana uwezo wa kuzuia taarifa ya mdhibiti mkuu wa Serikali maana ipo kisheria inatakiwa tarehe 31/03 ya kila mwaka iwe tayari na CAG kuwasilisha kwake ikiwa confidential na baada ya hapo,Rais anakabidhi Ofisi ya Bunge na ndipo inakuwa public document.Yeye alishindwa kujua upepo utakuwaje kwa serikali yake na ndio maana baada ya kukabidhiwa na kuisoma kabla ya kupelekwa bungeni hakukuwa na serious statement kutoka kwa JK mwenyewe juu ya ubadhirifu ulikokuwa umegunduliwa na CAG hata kama ungekuwa na magnitude ndogo.
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kikwete hawezi kumn'goa Alhajj mwingine baada ya Alhajj Mkullo.
   
 18. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwani anasomaga ripoti? Hujui tuna vilaza wengi tu hata mikataba ya aibu huingia kizembe kwaajili ya uvivu wa kusoma? ukitaka kuwamaliza viongozi wetu tengeneza taarifa/ripoti yako na iwe na kurasa nyingi utashangaa.., kimsingi alipaswa kuliongelea hili kipekee si katika mambo ya jumla, maana yeye hufikiri sasa kwa kubadili mawaziri haya yote yatakuwa yamekwisha lakini ukweli ni kwamba watarajie mtikisiko zaidi hata ya uliuopita maana tutataka kuona sasa mali zilizouzwa kiholela zikirudi na watuhumiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.. ni bora sheria ya uhujumu uchumi ifanyiwe marekebisho ikibidi hata kuwatia kizuizini wahusika.
   
 19. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kiguu na njia safari hii anenda kula bata wapi?. Hanaga mda na mambo yenu. Bata tu kwanza kamda kenyewe kanaisha
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Aongee nini wakati naye ana mgao wake hapo?
   
Loading...