Bajeti inayotakiwa kwenda kwa nchi wahisani ni ile iliyopitishwa na bunge au rasimu(draft)yake?Kama ni rasimu basi lazima wanapelekewa tena inayopitishwa bungeni kwakuwa hata wao hujua kuwa hiyo ni rasimu ya bajeti.Kwa nini sasa hawakupelekewa?Jibu ni moja.Draft waliyokuwa nayo ilikuwa inawanufaisha viongozi kwa namna moja au nyingine.Kama iliyopitishwa na bunge ingeongeza maslahi zaidi kwa viongozi zaidi ya draft waliyonayo wahisani,je wahisani wasingepelekewa bajeti hiyo haraka mara baada ya kupitishwa na bunge?Na je hili limetokea bajeti hii tu au na zilizopita?Watanzania tunaliwa na kuibiwa na hawa wezi wa kalamu.
Tatizo hawawezi kupeleka budget iliyokwisha kupitshwa kwani inaulaji wao sasa wanapeleka draft ili wawekezaje waone vile vipaumbele vyao vinatekelezwa. Ikisha wanabadilisha kuingiza makadirio yao kama vitafunio vya bilioni 2.5, samani za bilioni 6, magari ya bilioni 10 basi maisha kula kuku kwenda mbele. Halafu tunauliza maendeleo ya tanzania yanapatikana wapi?