Mkulo: Kilichoenda kwa wahisani si bajeti ni "makadirio" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo: Kilichoenda kwa wahisani si bajeti ni "makadirio"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AmaniKatoshi, Dec 9, 2010.

 1. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkulo: Kilichoenda kwa wahisani si bajeti

  Mwananchi, Wednesday, 08 December 2010
  Raymond Kaminyoge

  SIKU tatu
  baada ya Kundi la nchi wahisani wa maendeleo ambalo zinachangia kwenye bajeti ya Tanzania (GBS) kuibua kashfa kuwa Serikali iliwapelekea bajeti tofauti na iliyopitishwa na Bunge, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo, ameibuka na kusema kilichokua kimepekwa kwao ni makadirio.

  Alisema bajeti iliyowasilishwa kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF) yalikuwa makadirio ambayo yalibadilishwa katika mchakato wa kuiandaa na kwamba bajeti iliyopitishwa na Bunge ndiyo inayotambulika.


  Mkulo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti.


  "Kuna mchakato mrefu wakati wa kuandaa bajeti, tuliwapa makadirio ya bajeti yetu mwezi Aprili mwaka huu, baada ya hapo bajeti ilipitia kwenye Baraza la Mawaziri ambalo lilifanya marekebisho. Katika kipindi hicho kuna marekebisho yalifanywa hivyo kutofautiana na makadirio tuliyowapelekea wahisani," alisema Mkulo na kuongeza:


  "
  Ndiyo maana nasema sijawahi kupeleka kwa wahisani bajeti tofauti na iliyopelekwa bungeni. Nasisitiza kuwa bajeti ni moja tu ambayo ndiyo hiyo niliyowasilisha bungeni baada ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri," alisema.

  Alisema ni utaratibu wa kawaida wahisani kupelekewa makadirio mapema, lakini mambo hubadilika kutokana na gharama eza kuendesha Serikali kubadilika".


  "
  Msidhani Mkulo ndiye anayeandaa bajeti pekee yake, Baraza la Mawaziri ndilo lenye kauli ya mwisho kuhusu bajeti ya nchi, wanaweza kubadilisha chochote wakati wahisani mlishawapelekea bajeti yenu mapema," alisema Mkulo.

  Jumatatu wiki hii, Mwenyekiti wa kundi la wahisani wa maendeleo ambalo linachangia kwenye bajeti kuu ya Tanzania (GBS), Svein Baera, katika hotuba yake ambayo Mwananchi ina nakala, alisema serikali ilipeleka IMF, bajeti tofauti na iliyopitishwa na Bunge.


  Taarifa hiyo ilitolewa huku wahisani hao wakiwa wamezuia theluthi moja ya zaidi ya dola za Marekani 800 milioni ambazo zinatakiwa zichangiwe na wahisani kwenye Bajeti Kuu ya 2010/11, wakiishinikiza Serikali iharakishe utekelezaji wa programu ya mageuzi, yakiwemo ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma.


  Baera alibainisha maeneo sita kuwa ndiyo mhimili wa mjadala wao na serikali.

  "Napenda kuainisha maeneo sita ya ujumbe wetu ili kuweka sawa jukwaa la majadiliano yetu haya ya mwaka. Kuna tofauti kati ya bajeti iliyowasilishwa kwa bodi ya (Shirika la Kimataifa la Fedha) IMF na ile iliyopitishwa na Bunge Julai 2010," alisema Baera.

  Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani".


  Baera alisema kukosekana kwa uwazi katika matumizi, vipaumbele, mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili.  My take:
  1. Kwa nini imemchukua Mh Mkulo siku tatu kujibu shutuma wakati jibu alikuwa nalo kwa kuwa alihusika kwenye mchakato wote?


  2. Je, kwa nini Mh Mkulo anasema budget inaandaliwa na watu wengi? Ina maana anataka kusema kosa hilo sio la kwake?

  3. Kwa kuwa ofisi yake inahusika moja kwa moja kwa nini anatoa majibu ya kujihami badala ya kuchukua uamuzi wa kuijuzulu?

  4. Je, Mkulo anataka kutuambia kuwa bajeti sio makadirio?


  Hebu tuliangalie hili wana Jf
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Huyu waziri anafanya mambo kama conmen wa pale nje ya Bills. Hii mambo ya kupeleka bajeti mbili ni utapeli ulioukuka aache masihala.
   
 3. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu umeuliza maswali ya msingi sana. Mimi nadhani ni vyema tukiangalia maneno ya Mkulo kwa maana zaidi ya mbili.
  1. Imechukua siku 3 kwa kuwa;
  a. Hajui kinachoendelea hivyo wasaidizi wake walilazimika kutafuta sababu
  b. Walikuwa wamechakachua na ilibidi watunge sababu.

  2.Bajeti inaandaliwa na watu wengi ana maanisha;
  a.hakuna coordination nzuri ya ku-reconcile data kutoka pande husika (inefficiency)
  b.timu ya wachakachuaji ilihusisha watu nje ya wataalam wa wizara, hivyo mahesabu hayakwenda sawa

  3. Kwa nini hajiuzulu? Kwa sababu;
  a. haoni kosa ni hitlafu ndogo tu iliyotokea.
  b. kosa halikusababishwa na yeye bali ile timu ya wachakachuaji walioharibu mahesabu

  4. Je bajeti si makadirio?
  a. nothing is set in stone, lkn bajeti ni realistic projection
  b. hawezi kukubali kuwa ni makadirio kwani itazua maswli mengi.

  Kama jibu ya maswali yako yote ni (a) basi Mkulo ni incompetent arrogant unreliable leader.
  Kama jibu ni (b) basi Mkulo ni scapegoat na anajua hilo hivyo anatuma ujumbe kwa wahusika - he is not taking this lying down!
  Nawasilisha.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu nakupongeza kwa namna ulivyoweza kujengea hoja maswali ya AmaniKatoshi
  Zaidi ya hayo maswali na mfano wa majibu. Pia tutafakari kile ambacho Mkulo hakukisema ni kuwa hayo makadirio yalikuwa replaced baada ya bajeti kupitishwa?? I mean lini walipeleka bajeti kamili IMF? Sidhani wahisani walikurupuka na kudai bajeti ina kasoro. Je ina maana kama IMF wangetoa fungu ambalo limetokana na makadirio hayo hiyo ziada ingerejeshwa au ndo ingekuwa kwenye menu list ya mafisadi??
   
 5. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #5
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu Susuviri na wengine, nimefurahishwa sana na majibu yako. Nilipata majibu yanayoendana na ya kwako baada ya kuuliza maswali yangu, lakini nimependelea zaidi yametoka kwako na kuonyesha jinsi "tatizo la usiri wa madudu, uchakachuaji na iniefficiency and lack of accountability" yanavyoitafuna nchi yetu na kodi zetu wavuja jasho.

  Kuongezea na swali la mchangiaji wa mwisho najiuliza "kwa nini Mkulo alitata mtoa shutuma aende kwa ofisi yake ili wakazungumze?" na je si ukweli majibu yake ametimiza wajibu kutumia media baada ya kugundua ilikuwa kosa kutaka kujibu shutuma tena ya mtu anayeshikilia hela za bajeti kwa kumnongoneza...na akijua kuwa hanong`onezeki?

  Sasa ninaendelea kupata picha kamili kwa nini wale wazee kule Kilosa walisema hafai....
   
 6. R

  Robin Member

  #6
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu msanii Mkulo aache kutudanganya.kwani alishindwa nini kuwapa hao wahisan bajeti iliyopitishwa ili wajue hali halisi?ni nini anaficha hapa?kweli hafai japo ni swahiba wa JK na wizara ni nzito/delicate kuliko uwezo wake but kwasababu ya kubebana ,ushikaji na upambe kapewa.
  iam so bored with minister and his president.
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Unbelivable....... Please please..... STOP INSULTING OUR INTELLIGENCE......
   
 8. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #8
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ama kwa hakika hii inaonesha wazi kwamba sasa wahisani wameanza kushtukia mipango ya kisanii inayoendeshwa na serikali ya CCM na JK wao hivyo wameanza kufuatilia kila kitu kinachofanywa na serikali hasa katika mipango iliyo katika maandishi. Hata wao pia wanakumbuka jinsi sheria ya gharama za uchaguzi ilivyochakachuliwa mara baada ya kupitishwa bungeni na rais kupewa nyingine iliyoongezwa vipengele ambavyo havikujadiliwa na bunge. Kwa kuzingatia hilo la umaarufu wa kuchakachua kila kitu ilibidi wahisani wachukue muda kuangalia uwezekano wa bajeti kuchakachuliwa na hilo wameliona, sasa hapa Mkullo anakuja na maneno mepesi ya kupoza eti alipeleka makadirio kwa wahisani. Sasa ina maana hayo makadirio yametofautiana sana na hiyo bajeti halisi iliyojadiliwa na kupitishwa na bunge? Na kama ni makadirio ni lazima hiyo copy isomeke kuwa ni makadirio ya bajeti ya serikali ya JMT kwa mwaka wa fedha 2010/2011 hapa hata hao wahisani wasingesema kwamba wamepewa bajeti tofauti na iliyopitishwa na Bunge.
  Nashawishika kuamini kwamba hawa wasanii huwa wanaandaa bajeti mbili, moja inazidi ili kupata ulaji wao na ya pili ni ya kutudanganya sisi wadanganyika kuona kwamba ndio bajeti halisi iliyojadiliwa na kupitishwa na bunge letu.
  Kwa mtazamo huu namshauri Mkullo aachie ngazi kwa sababu ameliaibisha taifa.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa nnavyoifahamu Tanzania hii hasa ndiyo sababu kuu. Yaani hawa mawaziri walio wengi ni kupiga siasa tu, hawajui hata kinachoendelea. And guess wht in just this one month napata picha awamu hii ya Kikwete na serikali yake itakuwa kwenye defensive mode mpaka 2015. Hawajajiandaa kufanya lolote. I just can't believe eti JK yule yule tunayemjua will do, act or plan anaything different. Wao kazi yao kubwa ni kushinda uchaguzi tu!!!
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Dec 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kweli kabisa, kila mara JK anazungumzia juu ya kwa nini CCM imeshindwa katika majimbo kadhaa na eti ufanyike utafiti kujua hilo! Wanachofikiria hawa jamaa ni kubaki madarakani tuu na kufanya ufisadi!
   
 11. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Wakuu, naomba tuendelee kuangalia maswali mengine maana naamini tunaweza tukaendelea kupata picha kamili cha kilichojiri mpaka tumepata aibu hii kama taifa
  Naomba kwanza tumalize kuangalia maneno ya Mkulo, alitaka mtoa shutuma aende ofsini kwake kwa sababu;
  a) aligundua wasaidizi wake walichemka na alitaka ‘kusave face' yaani kuepusha kuaibika zaidi
  b) alifikiri anaweza kuwalisha maneno wahisani watulie na uchakachuaji uendelee

  Kuhusu makadirio yaliyotolewa IMF kama yalikuwa ‘replaced' hatuwezi kujua kama ni kweli au la, ila wamepata aibu ya kutosha.

  Mi binafsi nadhani ukweli ni c) yaani - both above a) and b) is true. Ni uzembe ukichanganya na uchakachuaji. :eek:
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa kuwa hawa jamaa akili yao yote ni jinsi ya kubaki madarakani na sio jinsi ya kuboresha maisha ya wananchi; na ndiyo maana awamu hii ya lala salama ya Kiwete hatafanya kitu cha maana kwa nchi hii isipokuwa kutuibia maliasili zetu yeye akishirikiana na wakina Subash wake!! Mungu mkubwa anawaona na hukumu yao wataipata hapa hapa duniani; kwani wameishaanza kuadhibiwa kwa kulazimika kunywa maji na dawa hadharani hata kwenye gwaride!!
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Acheni Wale, Nchi ni yao wao na Familia zao
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  bdo shida ya kuwa na mawaziri wenye kuwa na upeo mdogo na wasio na vision..sasa haya ndo matunda yake
   
 15. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo kilichoenda ni makadirio wengepewa...... hiyo difference ingekwenda wapi? na nani angekuwa amepitisha matumizi yake? (I thought hii ni kazi ya Bunge?)
   
 16. m

  mtukazi Member

  #16
  Dec 9, 2010
  Joined: Jun 8, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wahisani nawashukuru kwa kuwa makini na serikali ya ccm kwani hawa ni ccm ni mabingwa wa kuchakachuwa.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mwe sa zengine nataka kucheka vituko vya mawaziri wetu hebu bwana mkulo mzee wa masters ya international business tupe tofauti kati ya Budget na makadirio?
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huyu waziri kama conmen naye "makadirio" kivipi
   
 19. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Bajeti inayotakiwa kwenda kwa nchi wahisani ni ile iliyopitishwa na bunge au rasimu(draft)yake?Kama ni rasimu basi lazima wanapelekewa tena inayopitishwa bungeni kwakuwa hata wao hujua kuwa hiyo ni rasimu ya bajeti.Kwa nini sasa hawakupelekewa?Jibu ni moja.Draft waliyokuwa nayo ilikuwa inawanufaisha viongozi kwa namna moja au nyingine.Kama iliyopitishwa na bunge ingeongeza maslahi zaidi kwa viongozi zaidi ya draft waliyonayo wahisani,je wahisani wasingepelekewa bajeti hiyo haraka mara baada ya kupitishwa na bunge?Na je hili limetokea bajeti hii tu au na zilizopita?Watanzania tunaliwa na kuibiwa na hawa wezi wa kalamu.
   
 20. j

  julius Senior Member

  #20
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nadhni mimi kma mtanzania,siko proud 2 be tanzanian..wait just wait sababu kubwa yakufeel ths way,nipale vngozi wetu include our prezd wanapokua wanatalk na public wanajua sis nimaignorante..its make me sick.
   
Loading...