Budget ya 2010-2011 inaonyesha kuwa recurrent expenditure ambayo inainclude mishahara ni bn 7790, sawa na asilimia 67% ya budget yote ya serekali ya trilioni 11610 tzs. Makusanyo ya ndani ni bn 6003 tzs. Katika recurrent expenditure kuna mambo mengi sana, lakini mishahara inaweza kuwa ni moja ya sehemu nene nene. Sikuweza kupata mchanganuo wa mishahara ya wafanyakazi katika bajeti hiyo ni asilimia ngapi-- kama kuna mwenye nayo aiweke hapa tuichambue. Kama serekali inakusanya wastani wa bilioni 450 kwa mwezi, kwa mwaka itakusanya 5400bn, sawa na tofauti ya bn 603 pungufu ya budget ya makusanyo ya ndani
Mkulo kwa unafiki mkubwa ameshidwa kutaja ziada/nakisi ya mapato na matumizi baada ya kuchojoa mishahara. Ina maana ukishalipa mishahara kinachobaki ni ziada na ni akiba, je kuhusu usafiri, hospitali, ruzuku za vyama vya siasa, safari za JK, vitafunwa vya ofisi, mafuta ya magari ya serekali, viongozi wastaafu etc. Ukishalipa vyote hivyo ziada au pungufu ni kiasi gani-- hilo ndilo alitakiwa asema na hakusema na ndio hapo Zito anapokuwa shujaa kwani ndipo haswa alipopasema
Ni kweli serekali inaweza kuwa na uwezo wa kulipa mishahara kufuatia makusanyo yake, kama mishahara ingekuwa first priority, but je ni kipi kinaanza kulipwa, kama vitafunwa vya wakubwa vinaanza kulipwa kabla ya mshahara wa kalumakenge, ni wazi kuwa kinachobaki baada ya kuondoa matumizi hayo ya wakubwa ni kidogo kuweza kuwalipa kina kalumakenge kima cha chini.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa kuna pengo la mapato na matumizi, matumizi ni makubwa kuliko mapato, na Mkulo hilo hakulionyesha, yeye kaonyesha tu matumizi ya serekali kwa upande wa mishahara, hakusema mengine. So ukishatoa hayo mengine, kinachobaki ni kidogo kuweza kulipa wafanyakazi- ukizingatia kuwa mishahara iko ranked low kwenye order ya matumizi ya serekali na ndio maana serekali inakopa. Zito is absolutely right, Mkulo umezidi kuiumbua serekali ya JK
Na hawa waandishi wa habari uchwara wasioweza kuuliza maswali ya kiuchmabuzi zaidi wananiudhi kama nini