Mkulo ajitetea, akana kumuuzia Mohamed Ent Kiwanja, amrushia kombora Mkurugenzi CHC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo ajitetea, akana kumuuzia Mohamed Ent Kiwanja, amrushia kombora Mkurugenzi CHC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Apr 27, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Wana JF, Ningewaleteeni taarifa yote ya Mkulo kukana kuhusika kwake, lakini nawaleteeni kipande tu maana taarifa yake ni ndefu sanaaa. Narudia tena usizingatie namba hizo nimepunguza baadhi ya maneno katika taarifa hii ni ndefu mnoooo.

  1.0 Tungependa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja hizo kama ifuatavyo:- Kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere hakikuuzwa na Wizara ya Fedha, wala na Waziri wa Fedha. Kiwanja hicho kiliuzwa na aliyekuwa Mwenyekiti na Kaimu Mkurugenzi wa CHC kinyume na maelekezo ya Wizara ya Fedha na Kamati ya Wataalam (DTT), kwamba kiwanja hicho kiuzwe kwa bei ya soko kwa kuzingatia Sheria na Taratibu.

  2.0 Ukweli upo kwamba, baada ya maelekezo ya Wizara ya Fedha kwamba bei ya soko na taratibu na sheria zitumike, Kamati ya Wataalamu wa Serikali, ilikaa na kushauri kwamba taratibu na sheria ni kutangaza ili kupata bei ya soko.

  3.0 Bodi ya CHC ilikaa na kujadili maelekezo ya Wizara ya Fedha na ushauri wa Kamati ya Wataalam. Baadhi ya Wajumbe wa Bodi walishindwa kuelewa maana ya taratibu na sheria na bei ya soko, hivyo Bodi iliagiza Waziri wa Fedha aombwe ufafanuzi. Mwenyekiti na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CHC walitumwa na Bodi wamwone Waziri wa Fedha ili warudishe majibu kwenye Bodi. Waziri wa Fedha alitoa maelezo kwao kwamba, tayari alishatoa maelekezo kwa maandishi hivyo waendelee kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa.

  4.0 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CHC hawakurudi kwenye Bodi baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Fedha, bali waliamua kuuza kiwanja hicho kwa bei ya Mtathmini, badala ya kutangaza na kupata bei ya soko kama walivyoelekezwa na Wizara ya Fedha na Kamati ya Wataalam. Aidha, hawakurudi kwa Wizara ya Fedha kutoa taarifa ya utekelezaji wa maelekezo ya Wizara.

  5.0 Tuhuma kuhusu kwamba, Wizara ya Fedha ilihusika katika uuzwaji wa kiwanja hicho kwa kutoa maagizo kwa uongozi wa Shirika kuuza kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere bila kuishirikisha Bodi ya Wakurugenzi, hazina ukweli.

  6.0 Kwa kuzingatia maelekezo ya Waziri wa Fedha ni dhahiri kuwa, Mhe. Waziri wa Fedha, hakuhusika na uuzaji wa kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere na wala hakuingilia utendaji wa CHC. Maelekezo aliyotoa yaliitaka CHC ifanye maamuzi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.Badala yake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CHC waliamua kuuza kiwanja hicho bila kuzingatia ushauri wa Kamati ya Wataalam (DTT) na maelekezo ya Wizara ya Fedha.

  7.0 Kwa misingi hiyo, tuhuma kwamba, Mhe. Waziri wa Fedha alihusika na uuzaji wa kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere sio za ukweli.
  KATIBU MKUU
  WIZARA YA FEDHA
  APRILI, 2012
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ukitaka kusoma taarifa yote hii hapa

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA FEDHA


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU SHUTUMA DHIDI YA WAZIRI WA FEDHA YA KUHUSIKA KUUZA KIWANJA CHA CHC NA. 10 BILA KUZINGATIA TARATIBU

  UTANGULIZI
  Wakati PSRC ilipokuwa chini ya Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji, mwaka 2002 iliuza kiwanja Na. 192 kwa Mohamed Enterprise (T) Limited (METL) na mwaka 2003 ikauza kiwanja Na. 191 kwa Dar es Salaam RTC. Viwanja hivyo viliuzwa kabla ya PSRC kuvunjwa tarehe 31 Desemba, 2007 na shughuli zake kukabidhiwa CHC tarehe 1 Januari, 2008, ambapo ndiyo shughuli za CHC zilihamishiwa Wizara ya Fedha.

  Kiwanja Na. 192 (au Na. 11 kwa sasa), cha GAPEX (iliyovunjwa na baadhi ya mali zake kukabidhiwa PSRC) na kiwanja Na. 191 cha Dar es Salaam RTC, vilikuwa katika eneo moja vikitumia barabara moja kuingia kwa kupitia ndani ya kiwanja Na. 191 kutokea barabara ya Nyerere (Pugu Road). Hata hivyo, PSRC waliuza viwanja hivyo bila kwanza kutoa njia (access road) kuingia kiwanja Na. 192.

  Dar es salaam RTC walianza kupatiwa hati ya kiwanja Na. 191, hivyo kukawa na mgogoro wa muda mrefu kwa sababu METL hakuweza kupatiwa hati na Manispaa ya Temeke bila ya kuwa na njia. Vile vile Dar es Salaam RTC kutokana na kero ya magari makubwa ya METL, walikataa yasiendelee kupita katika kiwanja chao bila malipo. Malipo ya madai ya Sh. 2.34bn ya barabara yanayodaiwa na Dar es Salaam RTC hayakuwahi kulipwa na Serikali hadi sasa.

  Kwa misingi hiyo PSRC ilitakiwa kutoa access road kwa METL. Kamati ya Serikali chini ya CHC ilitafakari suala hilo nakuona kwamba, kiwanja Na. 10 ambacho kiliwekwa chini ya PSRC kupitia mali za TANGOLD iliyokuwa kampuni tanzu ya NMC, kingeweza kutumiwa kutatua tatizo hilo. Kiwanja Na. 10 kilikuwa kimepangishwa kwa M/s Noble Azania Investment Ltd (NAIL) na aliweka pingamizi asinyang'anywe na PSRC. METL alikubali kwamba endapo atapewa kiwanja hicho ili apate barabara atachukua na kesi na madai ya NAIL.

  Katika Mkutano wake wa Saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, masuala kadhaa yalijitokeza na kujadiliwa. Aidha, katika majadiliano hayo baadhi ya waheshimiwa wabunge walichangia hoja za POAC na PAC kwa kumshutumu Mhe Waziri wa Fedha. Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wakichangia hoja walisema kuwa, baadhi ya Mawaziri ni wezi na kuwa wanatafuna fedha za Watanzania bila ya woga, na kuwa Mhe. Waziri wa Fedha ameuza viwanja vya CHC. Aidha, walidai kuwa, alihusika katika uuzaji wa mali ya Serikali katika kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere na kwamba ameingilia utendaji wa Mashirika ya Serikali ikiwamo CHC.

  Tungependa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja hizo kama ifuatavyo:- Kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere hakikuuzwa na Wizara ya Fedha, wala na Waziri wa Fedha. Kiwanja hicho kiliuzwa na aliyekuwa Mwenyekiti na Kaimu Mkurugenzi wa CHC kinyume na maelekezo ya Wizara ya Fedha na Kamati ya Wataalam (DTT), kwamba kiwanja hicho kiuzwe kwa bei ya soko kwa kuzingatia Sheria na Taratibu.

  Ukweli upo kwamba, baada ya maelekezo ya Wizara ya Fedha kwamba bei ya soko na taratibu na sheria zitumike, Kamati ya Wataalamu wa Serikali, ilikaa na kushauri kwamba taratibu na sheria ni kutangaza ili kupata bei ya soko.

  Bodi ya CHC ilikaa na kujadili maelekezo ya Wizara ya Fedha na ushauri wa Kamati ya Wataalam. Baadhi ya Wajumbe wa Bodi walishindwa kuelewa maana ya taratibu na sheria na bei ya soko, hivyo Bodi iliagiza Waziri wa Fedha aombwe ufafanuzi. Mwenyekiti na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CHC walitumwa na Bodi wamwone Waziri wa Fedha ili warudishe majibu kwenye Bodi. Waziri wa Fedha alitoa maelezo kwao kwamba, tayari alishatoa maelekezo kwa maandishi hivyo waendelee kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa.

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CHC hawakurudi kwenye Bodi baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Fedha, bali waliamua kuuza kiwanja hicho kwa bei ya Mtathmini, badala ya kutangaza na kupata bei ya soko kama walivyoelekezwa na Wizara ya Fedha na Kamati ya Wataalam. Aidha, hawakurudi kwa Wizara ya Fedha kutoa taarifa ya utekelezaji wa maelekezo ya Wizara.

  Aidha ni vyema ijulikane kwamba, ukaguzi maalumu uliofanywa huko CHC na Mkaguzi wa Nje, wakati wote wa ukaguzi Wizara ya Fedha haikuhusishwa kutoa ufafanuzi au taarifa yoyote.

  Tuhuma kuhusu kwamba, Wizara ya Fedha ilihusika katika uuzwaji wa kiwanja hicho kwa kutoa maagizo kwa uongozi wa Shirika kuuza kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere bila kuishirikisha Bodi ya Wakurugenzi, hazina ukweli.

  Hakuna maagizo yoyote ya Wizara ya Fedha yanayosema kuwa, kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere kiuzwe kwa kampuni ya METL kwa kiasi cha shilingi bilioni 2.46 bila kuzingatia sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2006.

  Kwa kuzingatia maelekezo ya Waziri wa Fedha ni dhahiri kuwa, Mhe. Waziri wa Fedha, hakuhusika na uuzaji wa kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere na wala hakuingilia utendaji wa CHC. Maelekezo aliyotoa yaliitaka CHC ifanye maamuzi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.

  Badala yake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CHC waliamua kuuza kiwanja hicho bila kuzingatia ushauri wa Kamati ya Wataalam (DTT) na maelekezo ya Wizara ya Fedha.

  Kwa misingi hiyo, tuhuma kwamba, Mhe. Waziri wa Fedha alihusika na uuzaji wa kiwanja Na. 10 barabara ya Nyerere sio za ukweli.  KATIBU MKUU
  WIZARA YA FEDHA
  APRILI, 2012

   
 3. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama aya zinajirudiarudia vile? uchunguzi huru unahitajika kujua ukweli ila ni haki yake kujitetea au kutetewa.
   
 4. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka kusema kamati ya bunge sio huru eeeh? Nyie ndo mnataka kila kitu tume ndani ya tume! Kamati ishatoa report tena mnataka tume huru ya wapi? Itoke mbinguni? Kama amekiuka taratibu atoke na ashtakiwe report ya kamati ya bunge inatosha kuwa evidence!
   
 5. paty

  paty JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,257
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  " bra bra braa, " asite utani, si tunataka afikishwe mahakamani
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Does it Help or change anything?wasting of time and peoples Money kukanusha ukweli kwanini hayo maelezo hawakutoa kwenye Kamati?Shame on you!Ur always Reactive and not Proactive!
   
 7. M

  Moony JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Jipange sawasawa kwani bado; utajitetea sanaaaaaaa.:high5:
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  huyu dewiji nae! bungeni hatumsikii si kuunga mkono wala kupinga hoja! kumbe ubunge kwake ni mtama ili arubuni na kupewa ardhi yetu eeh!.
  TUNDU LISU, TUNAKUPA ASIGHNMENT YA KWANZA BAADA YA USHINDI, WAPE ELIMU YA URAIA NDUGU ZAKO WA SINGIDA MJINI IWAKOLEE, TUMUONDOE DEWIJI!!!!!!!!!
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  bei ya soko ni ipi?square meter sh 6000?mkulo hakua na msimamo thabiti ktk jambo hili.kwa nini wauze ardhi kwa muhindi?
   
 10. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mh. Mkullo ulikua wapi wakati haya yanatendeka? Kwanini ukuchuua hatua stahiki kwa waliovunja sheria? Unapashwa kuelewa ya kuaelewa ya kwamba kauli yako ya kujitetetea imechelewa.

  Kamahaya yasingeibuliwa ungelikaa kimya hivyo kuhusika kwako au kutohusika kwako hakubadirli mazingira ya kosa.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,769
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280
  Tunarudi pale pale - HUU NI UFALME ULIOFITINIKA HAUWEZI KUSIMAMA KWA MAANA MUNGU AMEUKATAA! Naona kila mtu anaongea lake kama wale waliokuwa wanajenga Babeli. Pambaf zao!
   
 12. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Boss wake anaamini mtu akiwa na kipara basi ana akili nyingi sana. They all go down the drain,lol! Ka nchi kamefilisika
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,769
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280

  Ni kweli Mkuu siku ipo tena yaja atakapojitetea ndani ya vizimba vya mahakama na pingu mkononi. Asidhanie ataendelea kutuandikia vinyaraka vya kizushi kama hivi akiwa ndani ya V8 full kipupwe kwa gharama ya jasho la mlalahoi. WATAJUTA.
   
 14. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Kwani hapa ni Mkulo anaejitetea au Katibu Mkuu wa hazina ndio anamtetea Mkulo..?
   
 15. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Waaaaaooo, I like this part....yaani Wizara imetuma maelekezo yenye taratibu na sheria...waliotumiwa hawajazielewa vizuri....wanaenda zilikotoka hizi taratibu na sheria then mhukisa mkuu (waziri) anawajibu kuwa kila kitu kaweka kwenye maandashi na warudi tu wakatekeleze (kile alichoambiwa na watu hawa hawajakielewa)...hope utaelewa (katika hali ya kawaida) kama umempa junior wako kitu afanye na akaja kwako ukwawa busy kutomweleza namna ya kufanya bali "aende tu" na afanye kama "ulivyomwagiza", atakaposhindwa kufanya hivyo hutakuwa na sababu ya kulaumu

  Hahaaaaa, guess what Mheshimiwa Katibu.....hawa watu walikuwa smart sana.....ulitaka warudi tena kwenye Bodi kupeleka taarifa gani?? Kile ambacho hawakuelewa walitumwa na bodi waje waulizie and kwa kuwa waziri alikuwa busy kwenye yale madili yetu hakuweza kuwasaidia hata kidogo...sasa warudishe jibu gani kwenye bodi??? Halafu unajikanganya sana mheshimiwa waziri.....huku unanesha waziri hakuwapa ufafanuzi bali aliwaambia tu waangalie taratibu kama walivyopelekewa, hapa tena unasema baada ya waziri kuwapa ufafanuzi...Ni kweli Mheshimiwa katibu huelewi tofauti kati ya "maagizo" na "ufafanuzi" wa maagizo yale ambayo watu wamekuja kuwaambia hawajaelewa???

  Pia kuhusu kuto kurudi kwa waziri tena wangerudije wakati waziri alishindwa kuwapa hata ushirikiano wkati wanahitaji maelezo ya ziada ya namna ya kufanya vizuri kwa maagizo hayo......Na kwa serikali yenu ilivyo legelege kanuni ni ndogo tu....Nipuuzie leo na mimi nikupuuzie kesho THEN NGOMA DRAW na hunifanyi kitu..lol

  Lakini pia Mheshimiwa Katibu, je ninyi mnafanya kazi tu kwa kungojea kuletewa taarifa na sio kufuatilia?? Mlipoona wamekuja na wameondoka na hakuna feedback mlichukua hatua gani???
  Labda kweli tuhuma hazina ukweli, lakini kama mwananchi wa kawaida unaniacha na maswali mengi....ofisi yako haiko makini...it is a negligence of duty....hakuna mahali umeelezea kwenye utetezi wako ni kwa naman gani mlifuatilia utekelezaji wa maagizo yenu kwa mujibu wa taratibu na mlifanya nini baada ya kugundua taratibu na sheria mlizowapelekea zimekiukwa.......Mnaonekana kuwa na kitu tunaita "negligence of duty" na ndiyo maana wajanja wametumia hiyo opportunity na kuwa-sideline hata kwenye ukaguzi....SAYING SO, WEWE NA WAZIRI WAKO HAMUWEZI KUKWEPA KUWAJIBIKA KWA HILI
   
 16. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  As far as I'm concerned Mkulo anapashwa kulimwa risasi mchana kweupe kwa hujuma nyingi na nzito alizowafanyia watanzani maskini na kwa kupanga na kutekeleza ufisadi mwimgi. I JUST HATE AND DESPISE HIM!
   
 17. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,769
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280
  Vyovyote iwavyo, ni ufalme ule ule mmoja uliofitinika ambao u karibu kusambaratika. Huyo Katibu Mkuu mwenyewe ni mchafu balaa na uprofesa wake.
   
 18. p

  politiki JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  naona katibu anajaribu kumuokoa bosi alikuwa wapi siku zote hasiyapeleke haya kwa CAG. Too little to late.
   
 19. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii taarifa ya wizara ya Fedha inasikitisha, kwanza inaelekea hata hawaelewi hoja wao wako na POAC tu! Kwa kifupi wamekurupuka, maana ripoti ya POAC haijazungumzia uuzwaji wa hiki kiwanja hata seheMu moja, bali ni special audit ya CAG kwenye shirika la CHC, kwa maana hiyo wanasema CAG ni muongo?

  Swali dogo tu la kujiuliza ni kwanini Mkulo alipoitwa na CAG kuhojiwa juu ya jambo hili wakati uchunguzi unaendelea alisema 'hana muda'? Halafu leo ndio kapata muda wa kujitetea? Too late baba
   
 20. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Wengine wanawakana manaibu wao,wengine wanasali hadi redioni kuwa ni watumishi wa bwana watendewe bwana atakavyo...ila siku yaja tutataifisha mpaka suti zao kama vile yaliomkuta late Chiluba kule Lusaka,waache tu ila wajue mahela yetu ipo siku yatarudi tu hazina kule walikoyachota
   
Loading...