Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,805
- 24,437
Watanzania sasa tumekuwa tunatukana lugha yetu sisi wenyewe. Kustaafu ni kuacha kufanya kazi ama kwa hiari ama baada ya kufikia umri wa kustaafu uliowekwa na sheria ili ama ujipumuzishe au ufanye shughuli nyingine. Nafasi nyingi za kisiasa ambazo hazina retirement age haziwezi kuwa na mstaafu unless mtu huyo amejindoa mwenyewe kwa hiari kama ambavyo walivyofanya akina Nyerere, Abdul Wakil, na Kawawa; marais wote waliomfuatia Nyerere hawakustaafu. Vile Vile mawaziri wote waliokosa nafasi hizo kwa kutokuteuliwa tena siyo wastaafu.Waziri wa fedha mstaafu Mustapha Mkulo,jana 19 may alipokewa kwa shangwe na vingora na mamia ya wananchi wa jimbo lake .mapokezi hayo yalianzia mji mdogo wa Kimamba na kuhitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kilosa na hafra ya chakula kwenye makazi rasmi ya mbunge iliyohudhuriwa na makada wote wa chama wakiongozwa na Elias Tarimo Dc kilosa.
Ni makosa kutamka ifuatavyo: Rais Mstaafu Mwinyi, Rais Mstaafu Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu Lowasa, na Waziri Wa Fedha Mstaafu Mkulo, n.k.