Mkullo amka kutoka usingizini, wewe unajiona uko hatarini kwa sababu tu watu wamepiga picha wakati unapanda ndege kwenda Dodoma na wakati huo huo unamwambia dereva akufuate na gari la serikali. Hujakanusha kama sio kweli umesema hiyo ni kweli lakini ulifanya hivyo na ulikuwa unawahi mkutano kitu kilichofanya serikali US $ 5,000.
Awali ya yote, Hii si sababu ya msingi kujustify matumizi hayo kwani kuna naibu waziri kwa nini yeye asishughulike kwenye moja ya kazi hizo na wewe ufanye nyingine????? Hii yote ni kujilimbikizia madaraka hakuna delegation of powers.
Lakini kwangu mimi naona uko isolated na realities of life, wananchi wa Tanzania kwa ujumla wao maisha yao yako hatarini kuliko wewe unapokuja na udhanifu wako kuwa upo hatarini kwa sababu tu ya kufuja fedha. Fikiria ni watanzania wangapi ambao hawajui kama watapata mlo wao wa siku hiyo , mheshimiwa waziri ni wengi sana.
Ni Watanzania wangapi ambao wanashindwa kununua dawa ya malaria kwa ajili ya kutibu watoto wao, ni wanagapi amabao wanashindwa kulipia gharama za matibabu? Nadhani ni wengi sana,
Ni akina mama wanagapi ambao vichanga vyao vinafariki kabla ya kufika miezi sita, ni maelfu mheshimiwa waziri, ni akina mama wangapi wanalala chini pindi wapojifungua, ni watoto wanagapi wanakosa madawati na wanakaa kwenye vumbi toka Januari hadi Disemba, toka darasa la kwanza hadi la saba ni wengi wakimeza vumbi kila siku wapokuwa darasani.
Waziri, kati ya makundi hao na wewe ni nani maisha yao yako hatarini zaidi???????
Tafakari, you owe an apology to Tanzanians, labda kama hukusema hayo maneno.