Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amekuwa waziri kwa miaka mitatu na nusu. Haya tuna Mawaziri 30 asuming kila mmoja amekodi mara nane tu @ 8 zidisha mara $5000 (wastani) = $ 1,200,000 (Tsh Billion 18)! kukodi ndege tu!! Kama siyo ubadhirifu ni nini?? Halafu anakomaa komaa
Mkuu hesabu yako nzuri, lakini hujawapigia hesabu ya posho ya hao madereva wao na mafuta ya bure ya kwenda Dodoma
Ni kweli, mahafali na huo mkutano vyote vilipangwa, hakuna dharula hata moja hapo. Hoja kubwa kwa nini gari limfuate dodoma wakati kule magari yapo?
..kwanini anataka akodi ndege kisirisiri?
..kwanini kuwe na usiri ktk matumizi ya fedha za walipa kodi?
..kwanini anafikiri maisha yake yako hatarini ikiwa anatekeleza majukumu yake kwa haki na uadilifu?
Wala haishangazi sana maana Mkuu wake wa kazi kaongelea swala la udini kufungua bunge, hajui kuwa ni jukumu lake kuhakikisha analikemea kwa uwazi mara moja pale linapojitokeza. Badala yake anangoja kuyumba kisiasa ndiyo abatize kuporomoka kwa sifa yake kitaifa kuwa ilitokana na udini. Kiongozi asiyeweza ku-delagate authority ili wakati hayupo kazi ziendelee kama kawaida siyo kiongozi mzuri hata kidogo. Angeweza kuondoka jana yake na kumwachia Waziri mdogo hiyo Wizara hata Katibu Mkuu angeliweza kuifanya. Siku hizi njia za mawasiliano ni nyingi sana akiwa kwenye V8 anaweza kuchapa kazi sana tu ila ni ule ule ujinga wa viongozi kujiona miungu watu.Hata inashangaza zaidi kuona kua hajui kua jukumu la kufundisha usiri ofisini kwake lipo chini yake. Kashindwa kufundisha usiri ofisini yeye mwenyewe badala yake anatulaumu sisi wa kariakoo sokoni. Wakubwa wake walimpa cheo ili awafichie siri zao ama la sivyo wanamfutia uraia ama wanamuumbua na vyeti vyake - hii ndio CCM's office culture.