Mkullo: Maisha yangu yako hatarini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkullo: Maisha yangu yako hatarini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumiabusara, Jan 22, 2011.

 1. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amewashukia watendaji wa ofisi yake kwamba wanahatarisha maisha yake kwa kuvujisha siri za wizara hiyo.

  Mkulo alitoa kauli hiyo baada ya gazeti hili hivi karibuni kuripoti kuwa alikodi ndege kwenda Dodoma na kumuagiza dereva wake amfuate kwa shangingi lake aina ya G8.

  Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika wizara hiyo kwenye ukumbi wa BZ, ulioko nje kidogo ya mji wa Morogoro.

  Bila kutaja majina, waziri huyo mwenye dhamana ya fedha, alisema utafiti wake umeonyesha kuwa wavujishaji wakuu wa siri katika wizara yake ni wakurugenzi, makamishina na watendaji wa kati..

  "Hivi karibuni gazeti moja (Tanzania Daima Jumatano), likaamua kufuatilia safari ya waziri na dereva wake toka Dar es Salaam kwenda Dodoma baada ya kukodiwa ndege kwa gharama ya dola 5,000 bila kufanya uchunguzi kwa sababu gani ilifanyika hivyo...lakini ilikuwa imesukwa na baadhi ya watendaji wetu, tena wamo humu ili wamchafue Mkulo," alisema.

  Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi lakini iliyorefushwa na ufafanuzi wa taarifa hiyo iliyoonyesha kumkera sana Waziri Mkulo hivyo kumlazimu kutumia zaidi ya dakika 30 kutoa ufafanuzi juu ya mazingira ya kukodiwa ndege hiyo, Mkulo alisema hana mamlaka ya kujiamulia kukodi ndege na kuongeza kuwa tangu awe waziri, amekodiwa ndege mara nane tu.

  Mkulo ambaye alionyesha kukerwa sana na taarifa hiyo, alisema wizara iliamua kumkodia ndege hiyo yeye na dereva wake kwenda Dodoma kutokana na majukumu yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kulazimika kukutana na baadhi ya mabalozi na mawaziri wa fedha toka nje ya nchi ambao walikuwa wanaliingizia taifa takriban dola za Kimarekani milioni 100.

  "Akaandaliwa mwandishi uwanja wa ndege Dar es Salaam apige picha ndege anayopanda waziri na kule Dodoma akaandaliwa mwandishi kupiga picha ndege atakayoshuka waziri...ni hatari sana; hebu fikiria kama wangekuwa maharamia mimi si nigeuawa kwa dola 5,000 zinazodaiwa nimefuja!?" aliongeza.

  Akitahadharisha juu ya kutokuwa na siri katika utumishi hususan serikalini katika wizara nyeti kama hazina ambayo ni roho ya nchi, Mkulo alisema kama hakuna usiri wa nyaraka katika serikali yoyote waelewe kuwa hakutakuwa na utawala.

  Alisema nyaraka za serikali sasa zimezagaa mitaani hususan kwenye masoko likiwemo la Kariakoo jijini Dar es Salaam zikitumika katika matumizi yasiyo sahihi kwa wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wauza vitumbua na karanga.

  Awali Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, akiwasalimia wafanyakazi katika mkutano huo jana alisema mbali na kulitumikia taifa kama mkaguzi na mdhibiti wa mali za serikali amebaini kuwa wizara hiyo inakabiliwa na tatizo la matumizi makubwa kuliko mapato jambo linalosababisha kushindwa kufikia malengo.

  Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.

  Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.

  Taarifa hiyo ambayo ilimkera sana Waziri Mkulo, ilidai kuwa ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.  Source: Tanzania daima
   
 2. n

  niweze JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Njia nyingine ya Viongozi wa CCM kutafuta Sympathy kwa Wananchi. Huyu Jambazi amechukua ndege, trip nne na hatujui nyingine ngapi haja repoti na vitu vingine alivyoibia watanzania. Leo hii anazungumza utumbo mbele ya wapenda nchi waliofichua hili jambo...kama hakufanya kosa mbona hukusema mapema? Kwa hiyo kutokana na hili jambo Mkulo haoni makosa makubwa kafanya? Kweli CCM Viziwi...

  Sasa viongozi wa CCM na Serikali ni victims wa changes Zinazo kuja? Ngoja ni Kutaarifu Mr Mkulo, nchi zenye Katiba ya nguvu unatakiwa kujihudhuru kabla ya yote. Pili repoti ikitoka na unatakiwakwenda jela na kurudisha pesa ulizo tumia. Ondoa upuuzi kulia kwako...Wanawake wanajifungua wakilala chini Muhimbili wewe unatumia ndege kwenda mikoani Tanzania? Mr Mkulo angalia Katiba zinapofanya kazi:   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. m

  matawi JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Failure to plan is plan to fail, nina uhakika ratiba ya kukutana na mabalozi alikuwa nayo 1 year ago. Kiherehe cha kukodi ndege kimetokea wapi. Yaani inanikera sana kuona waziri hawi mfano wa kuwa na displine. Au ni zile digree za kufoji?
   
 4. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ni kweli, mahafali na huo mkutano vyote vilipangwa, hakuna dharula hata moja hapo. Hoja kubwa kwa nini gari limfuate dodoma wakati kule magari yapo?
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Usiri huo na utawala huo ndio uliotuletea Richmond, Dowans, n.k....
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Amekuwa waziri kwa miaka mitatu na nusu. Haya tuna Mawaziri 30 asuming kila mmoja amekodi mara nane tu @ 8 zidisha mara $5000 (wastani) = $ 1,200,000 (Tsh Billion 18)! kukodi ndege tu!! Kama siyo ubadhirifu ni nini?? Halafu anakomaa komaa
   
 7. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Naamini Siri za sekali ni zile zenye manufaa kwa Taifa, Si vinginevyo. Kesi ya Dowans imeendeshwa kwa siri hapo Movenpick, matokeo yake tumeyaona.
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Wizi mtupi kule kuna hazina ndogo kwanini atumie gari la dar wakati ameisha kodi ndege??kwahiyo kaunguza diesel bure!dar to dom
  +5000usd?=watumishi siyo wasiri??shame on him!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Hawajali kabisa maslahi ya nchi wao wanatumbua tu mapesa hovyo hovyo ambayo yangeweza kufanyia mambo ya maana chungu nzima. Wanapigiwa kelele kila siku na walipa kodi lakini inaelekea hawataki kabisa kusikia vilio vyao na kuendelea na matumizi yasiyo na tija kila siku iendayo kwa Mungu.

   
 10. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  teh teh teh
  nakulilia tanzania
  .

  baba omba omba watoto omba omba na huku wankula hela za yatima.....
   
 11. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Lakini naye aache uzushi, amekuiwa obama. Sasa kama junior kama huuyu anafanya mambo ya siri kaisi hiki, mkuu wake itakuwaje. Pengine kila siku ule msafara unao tuboa morogoro road ni danganya toto tuu, mtu mwenyewe kesha fika na hecopta yake mapema sisi tunahangaika kupak magari pembeni mkuu apite, kumba ni raia tuu wenye magari ya ikulu , kutembea chalinze.
   
 12. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kimsingi wizara imeshindwa kuelezea kwa nini walikodi ndege na gari likaenda Dodoma pamoja na kuwa Waziri alikuwa na majukumu mengine muhimu Dar es salaam. Hivi Manaibu waziri wanafanya kazi gani kama kila sehemu inabidi waziri mwenyewe awepo
   
 13. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The man has the audacity to justify anavyofuja pesa za uma

  kwa nini akasirike hii waste of public funds kuwekwa kwenye public domain?


  kwani kule dodoma asingepata gari la kumzungusha? kulikuwa na umuhim gani wa yeye kufuatwa ga GARI tena sio moja from DAR...hapo kulikuwa na per diem za dereva wake, mafuta, misosi pale segera na malazi...

  This comes from a man with a fake degree ambaye hajawahi kusimama kukanusha kuhusu hili,

  This also come from a man ambaye hajawahi kuweka wazi kuhusu utata wa uraia wake, No wonder anatumia ARROGANT na INSENSITIVE language dhidi ya WAUZA MAANDAZI na VITUMBUA....Kariakoo ambako tunaishi sie WASWAHILI


  Kwani aliona taabu gani kutumia analogy nyingine badala ya maneno ya wafunga vitumbua na maandani na kariakoo? why not kwao huko KILOSA if not MALAWI?


  Of course this is the man in charge of our economy and cares less about watu wa chini

  This country has gone to the dogs
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hata mimi sioni mantiki ya kila sehemu lazima yeye awepo kule dodoma angeenda naibu waziri yeye asubirie dar hao mabalozi waliosema wanaiingizia nchi...twajua ku justfy tu huko.

  Sidhani mahafali yana manufaa sanaa hadi kukodi ndege kwa garama kubwa vile ,ila Mkulo anakuwa hajui hata kujenga hoja sikuzote sijui hata kwa wafadhili inakuwaje watakuwa wanatushangaa sana....mtu bogus vile eti waziri wa fedha au ndio ile dhana ya majuha wawili kila mmj anamuona mwenzake afadhali
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kuhusu gari ni lazima na vyema kwenda; huo ndio ulikuwa usafiri sahihi nadhani moja ya hoja zao kununua hizo V8 ilikuwa ni mwendo kasi mkubwa, kama gari lisinge enda Dom ni utata zaidi maana lazima arudi Dar angetutia hasa nyinge ya $5,000; kwa hiyo gari haliepukiki hapo.

  Tatizo kubwa hapa ni kukodi ndege safari ya saa 6; kwa ujinga wake wa kushindwa ku-plan safari imetupa gharama $5,000 sijui ni karo ya wanafunzi wangapi!? alafu anaonyesha ni mpuuzi zaidi anasema ameshawai kukodi ndege mara nne tu!!!! Jamani hatuna Rais amtimue huyu mtu, TAKUKURU haina wataalam wenye uwezo wa Kiuchunguzi mbona kosa liko wazi sasa Mramba walimkamata wa nini kama siyo unafki; yani Mkulo ni mbumbumbu kiasi hicho hajui kwamba siku ina saa 24 na wiki siku 7 na mwezi siku 30-31 azipange vyema hasiumize hii nchni maskini?

   
 16. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Amesema mara nane tu, siyo nne mkuu
   
 17. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  Phew! Hivyo ni vijisent tu wazee serikalini...nyie ni wanafunzi?
   
 18. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,171
  Likes Received: 1,900
  Trophy Points: 280
  Hili ni pigo la lAANA nchi yetu imepigwa!!;

  HERI KWAO WAZALENDO wanaokemea hali hii kwa njia yeyote waliyo nayo mikononi mwao

  na laana hii iwakute wote wanaofanya ufisadi kwa vitendo na mawazo, wanaoona na kukaa kimya....

  NA WOTE WENYE MWILI TUSEME AMINA!!!
   
 19. M

  MLEKWA Senior Member

  #19
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikiwa Sokoine aliekuwa Waziri
  Mkuu alikua akipanda gari na mwisho kugongwa jee wewe Mkulo CCM inatia Kichefu chefu
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Mkullo aache matumizi mabaya na usalama wake utakuwepo............................

  Na ni vyema akafahamu hakuna siri katika wizi wa mali ya umma...............................

   
Loading...