Ray J Enterprise
Member
- Jul 18, 2022
- 24
- 47
Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani ambayo imekuwa na changamoto ya vijana kukosa ajira mara baada ya kuhitimu masomo. Kumekuwa na mitazamo mingi juu ya tatizo hili ambapo wengine wamefikia hatua ya kusema ni bomu linalojiandaa kulipuka.
Kwa vyovyote vile kuna haja ya kulipa kipaumbele suala la ajira kwa vijana. Itakumbukwa kwamba sehemu kubwa ya watu katika nchi yetu ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Kwa muktadha wa Tanzania kama zilivyo nchi nyingine zinazoendelea kilimo ndiyo sekta pekee ambayo imeajiri kundi kubwa la nguvu kazi japokuwa inakabiriwa na ushiriki mdogo kutoka kwa vijana.
Kuna haja kama taifa kuangalia namna ambavyo tunaweza kukitumia kilimo kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatakiwa kufanyika kuhakikisha Tanzania inaondokana na tatizo la ajira kupitia sekta ya kilimo ili kupata maendeleo yatakayonufaisha walio wengi katika zama hizi;
Kutoa ruzuku za pembejeo katika sekta ya kilimo mfano mbolea, vifaa vya kilimo, madawa nk. Mfano mbolea inauzwa sh. 60,000 kwa mfuko mmoja ikiwekwa ruzuku ya sh. 30,000 maana yake mbolea itauzwa kwa mkulima kwa nusu bei.
Hii itaongeza ushiriki wa vijana katika kilimo na itapunguza gharama kwa wakulima ambao kwa asilimia kubwa ni walala hoi. Hatua hii italeta tija na kufanya kilimo kisiwe kimbilio la watu hohe hahe na badala yake kila mtu ataweza kulima na hivyo kuongeza uzalishaji na kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Sambamba na hili serikali ipitie upya changamoto na fursa zilizojitokeza kwenye sera na mipango yote ya kilimo iliyopita ili kuboresha na kusahihisha makosa.
Kama taifa tujikite katika kilimo cha mkakati hususan kilimo cha mazao ya biashara ambacho kitaenda sambamba na uongezaji wa thamani ya malighafi ili kuleta tija katika masoko. Pia kitaongeza wigo wa mapato ya serikali na kitazalisha ajira nyingi pasipo kutumia teknolojia ya juu ambayo kwa kiasi kikubwa huua ajira. Mfano badala ya kuuza mahindi ghafi tunakoboa mahindi, tunasaga na kuuza unga wa sembe.
Ina maana watu watalima, watahudumia, watavuna, watasafirisha, watakoboa, vifungashio vitauzwa na badaaye yataingia sokoni. Katika hili utaona kuna mnyororo mkubwa ambapo mahindi yatapita kabla ya kuingia sokoni.
Sambamba na hilo hapo juu, Maeneo yenye nusu jangwa/ukame kama vile Dodoma na Singida yangetengwa kwa ajili ya kilimo cha mkakati cha alizeti ambazo zitatumika kuzalisha mafuta ya alizeti na hivyo kuondoa utegemezi wa mafuta kutoka nje ya nchi.
Pia mkoa wa Kigoma na maeneo rafiki yangetengwa kwa ajili ya kilimo cha michikichi ambapo mafuta ya mawese yatazalishwa na baadaye kuzalisha mafuta ya kula (Korie).
Tusimamie kwa dhati kabisa uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani kwa baadhi ya malighafi ambazo zimekuwa zikipotea hovyo bila sababu za msingi mfano maembe, parachichi, tangawizi, nyanya, karatasi nk. Mfano maembe yanaweza kukusanywa nchi nzima na kutengeneza juisi za maembe na unga wa maembe ukauzwa nje na nyanya zikatengenezwa sosi ya nyanya (tomato sauce). Hebu fikiria maembe yanavyozagaa wakati wa masika na kutuletea balaa la kipindupindu yaani baraka au neema inageuka kuwa laana – resource curse.
Tuanzishe kanda za kiuchumi kulingana na upatatikanaji wa malighafi kwa kanda husika. Mfano tuanzishe kiwanda kikubwa cha alizeti katika mikoa ya Dodoma na Singida ambapo ni mikoa rafiki kwa alizeti, hii itapelekea kuzaliwa viwanda vidogo vya kutengeneza vyakula vya mifugo kupitia mabaki (mashudu) ya alizeti. Ili kutekeleza mpango huu tumpe kazi kila mkuu wa mkoa na wilaya kukaa na wataalamu wa mkoa kuandaa tathmini ya gharama ya kila kiwanda kwa mkoa husika na baadaye kuuza hisa kwa wananchi ili kupata fedha stahiki na fedha zitakazopelea zitakopwa benki kukamilisha kiwango hicho.
Mfano kiwanda cha alizeti kinagharimu bilioni 20, zitauzwa hisa kwa kuanza na wakazi wa mkoa au kanda husika ili kupata kiasi hicho. Hii pia itakuwa ina maana ya kuweka uchumi mikononi mwa wananchi kupitia uchumi shirikishi na kupunguza tofauti ya walionacho na wasionacho. Vilevile, wananchi hususani wakulima watapata soko la uhakika kwa mazao yao na ajira pia.
Tuhakikishe tunaondoa matumizi ya jembe la mkono kwa wakulima wetu kwa kuvitumia vyama vya ushirika, vikundi vya wakulima, mashirika, makampuni na taasisi ambazo zitalazimika kuwakopesha matrekta wakulima katika vikundi vyao. Hali kadhalika kila kanda iweke mikakati madhubuti ya kuzalisha matrekta ya wakulima ambapo watakuwa wanayasambaza kwa wakulima kupitia ruzuku watakazokuwa wanapata kutoka serikalini.
Hili litaenda sambamba na uboreshaji na kuinua kiwango cha teknolojia kwa wakulima ikiwa ni pamoja na kujikita kwenye kilimo cha umwagiliaji kuondokana na utegemezi wa mvua. Tuna mabonde mengi tu ambayo kama yakitumiwa vizuri tutaondokana na kadhia hii ya kutegemea mvua.
Vilevile, tunapaswa kuongeza bajeti kwenye wizara ya kilimo na mifugo kwa ajili ya utafiti na kuzalisha mbegu za kisasa (chotara) za kilimo na mifugo mfano kuku, ng’ombe, mbuzi, nguruwe, samaki, kuanzisha maabara za kupima udongo na uanzishaji wa bima ya kilimo.
Zoezi hili liende sambamba na kuelimisha wakulima juu ya kilimo chenye tija na ufugaji wa kisasa ili kuongeza tija katika sekta hizi. Pia tuanzishe ufugaji wa kisasa wa samaki kando kando ya bahari, maziwa, mito na mabwawa ambapo kutakuwa na vitalu (Pond liners) vya samaki ambavyo vitatumia maji ya vyanzo husika bila kuathiri mazingira ya vyanzo hivyo. Watu waelimishwe juu ya ufugaji huu wa samaki bila kuathiri viumbe walioko katika vyanzo vya maji.
Mfano vitalu vinaanzishwa mita kadhaa kutoka chanzo cha maji kuvutwa na kujazwa kwenye kitalu kwa kutumia mpira na baadaye vifaranga kuingizwa humo. Hii itapunguza uvuvi haramu na pia samaki wataachwa waongezeke kwa kuwa uvuvi utakuwa ukiendelea kwenye vitalu husika bila kuathiri upatikanaji wa samaki sokoni.
Kwa kuhitimisha nipende kusema kuwa binafsi naamini kuwa kama tukitekeleza mambo haya yote niliyoyaeleza basi tatizo la ajira kwa vijana linawezekana kutatuliwa kabisa. Cha msingi ni kuweka nia na kuhimizana kufanya kazi kwa bidii pasipo kuhujumu mali za umma na mali za wanyonge.
Wakati tukiishi hapa duniani ni vyema tutambue kuwa tuna wajibu wa kuzitumia fursa zote tulizojaliwa na mwenyezi Mungu zitusaidie kutatua changamoto na kututimizia mahitaji yetu muhimu. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa ili tufanikiwe tunahitaji ardhi, watu na uongozi safi (bora) na ni vitu ambavyo tayari tunavyo kumbe tunahitaji kiongozi/viongozi wa kuwaonyesha njia wananchi ili Tanzania ipate maendeleo yatakayonufaisha walio wengi katika zama hizi.