Mkulima, tafsiri yake ni umaskini hii sio sawa

Hardlife

JF-Expert Member
Apr 11, 2021
2,750
6,247
Leo nimepata bahati ya kuongea na watoto wa shule ya msingi moja hivi hapa jijini Dar. Kuna ujumbe nilikuwa na ufikisha kwao pamoja na walimu wao.

Kama kawaida wakati namaliza kuongea nikawaambia mkazane kusoma kwakuwa wengine humu mtakuwa Ma engineer, daktari, rubani, (wao wakasema Rais, Mbunge, Waziri na Polisi) nikamalizia na wengine mtakuwa Wakulima.

Hapo kwenye Wakulima watoto wamenicheka sana. Hii inaashiria kwamba kuwa mkulima ni sawa na umasikini na hii issue si kwa watoto tu hao bali hata kwa baadhi ya watu wazima kabisa.

Juhudi za makusudi zinahitajika sana katika kuondoa hiyo dhana na naamini ikifutika hata vijana wengi wasiokuwa na ajira wanaweza kuunda vikundi na kupata mikopo na kupambana na kilimo.
 
South Africa kuna mtuu anaitwa BOER ki Afrikaans hicho, huyo ni mtu ambaye anaogopeka kupita maelezo ukisikia mkulima kila mtu anamuogopa
 
Hiyo pesa aliyonayo ni ya kizazi kwa kizazi, kibongo bongo tunawaita makaburu. Kaburu la south Africa achana nalo.

Kibongo bongo mfanyalazi anaheshimika ila mkulima wanamzarau, sasa huku nikinyume chake
Hayo mageuzi ndio yanatakiwa tuyafanye sasa.
 
Back
Top Bottom