MKUKUTA ni kama UKUTA?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Mwenzenu nimeamua kujifunza kwa kina huu Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA). Kwanza kwa sababu nasikia huwezi kuzungumzia mipango ya maendeleo bila kujadili au kujua MKUKUTA. Lakini pili kwa sababu watu wengi hawajui MKUKUTA kwa kina kinachostahili na hasa kwa sababu sehemu ya pili ndio inaelekea kuanza kwa kasi zote.

Swali ni kwa kiasi gani wananchi na watendaji mbalimbali wanajua juu ya MKUKUTA; jinsi gani watu wanajua unavyowagusa; na jinsi gani watu wanatakiwa kujua ili kuweza kuufanikisha?

Je wewe unaujua? kwa kiasi gani?
 
Mkukuta, mkurabita na watakuja na neno lingine ni mbinu tu za wanasiasa kuyaleta maneno magumu kwa wananchi ili kusiwe na maswali mengi kwa sababu utauliza nn wakati hata ufahamu wa hilo uulizalo huna kikubwa ni propaganda tu hakuna lingine hapo.
Ili tuendelee nyerere alishasema kuwa tunahitaji siasa safi , uongozi bora na...

Sasa siku hizi hakuna cha siasa safi wala uongozi bora ila kuna bora uongozi ndo maana hawatuelimishi maana hata ya mkukuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom