Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu...........!!!!!!

Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu...........!!!!!!

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,997
Happy holiday guys....

First Scenario....
Huyu mkaka alihamia Dar akitokea mkoani (Sitaki maswali mkoani ndo wapi tafadhali, cha muhimu unaelewa) alipofika Dar akatafuta mpenzi kama kawaida, huko mkoani alimuacha mchumba ambaye keshafanya process zote imebaki miezi minne tu ndoa ifungwe. Sasa basi akampata dada P, akamwambia eeh bana mie nilikuwa na mpenzi "sio mchumba tena" huko Mkoani, ila kwa vile nimehamia hapa Dar sidhani kama tutadumu uzingatia distance relationship ni ngumu sana kusurvive. Mdada akajaa, hao wakawa wapenzi... Siku ya siku wakatoka out bana, mkaka akakutana na marafiki zake wanaomfahamu tokea hukooo Mkoani....

Si wakaanza kumpongeza mkaka, hongera bana, huyu ndo mtarajiwa?? Mkaka akawa anapotezea kiaina ila mdada machale yakawa yanamcheza... Mmmmh...... Ila wanaume bana, nimewanyooshea mikono, mdada kuuliza akaambiwa ni utani.... Basi kila wanapokuwa pamoja, mkaka akipigiwa simu na mchumba wa Mkoani anaongea kwa ukali sana as if hamtaki kumbe ilikuwa danganya toto!!! Mwisho wa siku.mdada aliconfirm kuwa hawajaachana ikabidi ajiweke pembeni na mkaka akamuoa yuleee mchumba wa Mkoani.

Second Scenario.....
Huyu pia kahamia Dar akitokea Mkoani, ana mchumba huko Mkoani na baada ye miezi minne anakwenda kutoa mahari.... kapata msichana mrembo zaidi kuliko mchumba wa Mkoani, mapenzi yamekolea haswaaa mpaka mdada anashukuru Mungu kuwa kapata mume... Masikini angelijua anadanganywa asingejiachia kiasi hiko, namuonea huruma i wish nimwambie ila mmmh... Lisilonihusu!! Jamani wanaume muwe na huruma, si bora uwe muwazi mie nina mchumba kama vp tumegane kisera kuliko kuwahadaa wadada kiasi hiko!!!!!

Third scenario.....
Sasa huyu jamaa kiboko, kwanza ameoa ana kama miaka 2 katika ndoa, mbali na kuwa katika ndoa kabla hajaoa alizaa na wanawake wawili tofauti ila hakuwaoa, kaja kaoa mwanamke mwingineeee kabisaaa.... Basi kakutana na bidada, hapa naona alijaribu kuuma na kupuliza. Kamwambia kabisa mie nimeoa ndio, ila simpendi kabisa mke wangu nahisi aliniroga. Sasa wewe nizalie mtoto afu nitakuoa, nitaachana na mke wangu. JAMANI UONGO MWINGINE HAUNA MASHIKO KABISAAAAA.... Bidada kagoma, basi jamaa kuona hivo si akamwambia bidada kama huamini basi twende nikajiatambulishe kwenu....

Haooo mpaka kwao na bidada kujitambulisha ila kwa sharti la kutosema kama keshaoa, basi akajitambulisha na bidada si akabeba mimba!!!! DAH... HAPA KIUKWELI ALIBUG MEEEN.... Bahati mbaya alipata miscariage ikawa pona yake, alikalishwa kitimoto na mashost mpaka kikaeleka... Saiv naona ameeanza kupata akili kuwa alikuwa anadanganywa kweupeeee.....

Jamani hivi kwa scenario kama hizo yatashindwa kutokea ya akina Ufoo Saro?? Katika 1st scenario unadhani mdada atakuja kumpenda sana mwanaume atakayempata???
2nd scenario... Sijui itakuwaje mdada akigundua anadanganywa, i wish nimwambie ila mmmmhhh.... :tape: :tape:
3rd scenario huyu mwanaume ni muuaji....
 
Chakushangaza sasa!!!,,, wadada ndio wana wapenda wanaume wahivi kinooowmer.....
 
This kind on man's are very good professional in how to approach girls.
Na huwa hawakataliwi bhana, Lol...
 
hahaha yaani nimecheka mpk basi hata stori sijaimaliza eti hutaki maswali mkoan ndo wapi hahahah!!!!
 
wewe akija man akimwambia tumegane kisera utakubali maisha ?mapenzi bila ya uongo hayaendii
 
mwengine anajua kabisa umeoa na una mtoto ila kukikucha tu anaanza kukutumia vimesaage mambo umeamkaje??? unategemea nini?
 
Yani ni majanga haswa...kuna mmoja yani ndoa imeenda kuzuiwa kanisani..

Mkaka kumbe kaoa na ana mtoto mmoja tena ndoa ya kanisani...akapata mdada mwingine akamtolea hadi mahari mkewe kaja kujua ni siku wanaenda kanisani... ikabidi mkewe aende na cheti cha ndoa kuonyesha huyu mwanaume kashaoa..
 
Hawa wanaume tunawapenda lakini.....!! Men....can't live with them, can't live without them!
Wapi Karucee ?!
 
Last edited by a moderator:
Hivi naomba kuuliza wanawake wote hapa MMU, mwanaune anapokutongoza akilini mwenu huwa mnakuwa na majibu yapi?

Au huwa mnajidhatiti vipi mnapoanzisha mahusiano na a total stranger?
 
duuh hzi stori,znazd kunfundisha kitu ..ht km upo kwny uhusiano uwe mguu ndan mguu nje mana yn maumivu anytime,..o rathr to be on the safe side uwe na kidumu pembeni and ufahamiane na watu wengi hata kama akizingua una pa kupunguzia mawazo
 
Hivi naomba kuuliza wanawake wote hapa MMU, mwanaune anapokutongoza akilini mwenu huwa mnakuwa na majibu yapi?

Au huwa mnajidhatiti vipi mnapoanzisha mahusiano na a total stranger?

situation za kutongozwa zinakuja tofauti tofauti,utajaribu kumpima mtu kadri uwezavyo ujue yeye ni nani pamoja na wewe mwenyewe ni kiasi gani umempenda,..YOU CANT PREVENT HEARTBREAKS HT KM UMEMJUA MTU ALL UR LIFE..LOVE IS A RISK
 
duuh hzi stori,znazd kunfundisha kitu ..ht km upo kwny uhusiano uwe mguu ndan mguu nje mana yn maumivu anytime,..o rathr to be on the safe side uwe na kidumu pembeni and ufahamiane na watu wengi hata kama akizingua una pa kupunguzia mawazo
kidumu na ukimwi juu.
 
Back
Top Bottom