Mkosoaji wa serikali auawa Cambodia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mkosoaji na mwanaharakti mkubwa wa serikali nchini Cambodia ameuawa kwa kupigwa risasi hii leo jumapili katika mji mkuu wa nchi hiyo wakati kukiibuka mvutano wa kisiasa baina ya waziri mkuu Hun Sen na upinzani unaotarajiwa kutoa changamoto katika uchaguzi wa mapema mwakani.

Kem Ley mwenye umri wa miaka 46 kiongozi wa kundi la uhamasishaji la "Khmer kwa ajili ya Khmer" amepigwa risasi mara tatu katika kituo cha kuweka mafuta, polisi wamesema.

Mtuhumiwa amekamatwa na amekiri kufanya mauaji hayo katika mzozo wa kifedha. Video za mauaji hayo zilisambaa kwa haraka. Ubalozi wa Marekani mjini Phnom Penh umesema mwanaharakati huyo alikuwa mchambuzi mashuhuri kabisa wa kisiasa huku Uingereza ikisema taifa limepoteza mtu muhimu sana.

Chanzo: DW


 
Back
Top Bottom