Mkosamali: Mrema anajipendeleza alipwe mafao

Mkosamali: Mrema anajipendeleza alipwe mafao

Kule vunjo TLP means Tutamfata Lyatonga Popote! Hahahaha
 
Napenda kuweka sawa kila moja aelewe udokta wa Mrema ameupata vipi.
Udokta wa mrema sio wa darasani wa kuandika makabrasha kibao.
Mrema alitunukiwa udokta wa heshima na ubalozi wa Marekani kwa kutambua mchango mkubwa alioufanya pindi akiwa kiongozi wa serikali.
Mimi nashangaa mpaka leo serikali imeshindwa kumuenzi Mrema angalau kuita barabara moja kwa heshima yake.
 
Hivi Mrema alikuwa anaigiza au kweli ni jasiri? Nakumbuka tulivyompigania 1995 huwezi kuamini kama ni huyu,ila wenye kumbukumbu nzuri mtakumbuka mwishoni mwa miaka ya 90 baada ya kupata ubunge tmk mrema aliwahi kuongea uongo bungeni, walipotaka kumsimamisha akadai wamsamehe eti familia yake inamtegemea, tangu wakati huo mioyo ya wengi ikasinyaa kwa mzee huyu
 
Usaliti ni kwenda kinyume na mlichokubaliana, watoke hadharani watuoneshe Mrema walikubaliana nae kitu gani halafu akasaliti, msiwe wepesi wa kutumia misamiati kwa kuwa imezoeleka kwenye masikio yenu basi nanyi mnaitumia tu. Kama Mlikubaliana mtoke nje halafu akagoma ndio mngemwita msaliti lakini kama hamkumshirikiskwenye uamuzi wa kutoka nje atoke nje kwa kuwa Mbowe, Mnyaa na Mbatia wanatoka basi nae aunge tela?
 
Kiukweli Kauli na Vitendo vya wabunge vijana ndani ya Bunge vinafifisha Nguvu za sisi tunafikiria tunahitaji vijana wengi katka bunge letu hasa ukizingatia ni nchi pekee katka EAC hatuna free youth National council....tunaona kuwa kuwapigania vijana kuwa wengi bungeni hasa wenye lengo la ku_change the country sio kutoa Lugha za dharau kwa wanasiasa au viongozi waliopita....Binafsi nilisononeka sana kwa masikio yangu nikisikia Kauli ya Mkosamali kwa Mh Mrema....alipaswa kumpa heshima hata kwa Umri wala sio uanasiasa wake......Vurugu za mbunge wa Mbeya mjini nazo hazikuleta vijana katka eneo la vijana hasa ktk harakati za kuwapigania vijana kushika nafasi ukweli hata wazee wetu katika maeneo yetu ya uchaguzi ukweli wanatafakari haya.....

Hivi Zitto sio mpinzani? mbona namjua sana kwa jazba mbona hajawai tukana au kutoa kashfa wa yeyote.....!!! Ile kozi yay young political leaders waliopata akina Zitto 2003....nafikir ni wakat wa kuitafutia mitaala..... aliwahi kusema Mwl Jk baba wa Taifa Tabora, akiwahutubia baraza la vijana 1984, alisema " Vijana msiposimama na kuonyesha mnaweza kiakil na kimatendo katka uongozi wa Taifa lenu leo , basi Mtachungwa kama Pundamilia wa Mikumi"

Kwenye suala la vijana tuache ushabiki wa siasa...tuna hoja moja tu....sisi ndio viongozi wa leo..bali kujali chama chako...

VIJANA KWANZA, UZALENDO KWANZA..........
 
Katika mtu alie uharibu upinzani ni Mrema. Kama Angeku Sio yeye kupandikiza mamluki katika vyama vya upinzani Basi Ccm sasaiv isingekua madarakani! Huyu mtu hafai tena ni msanii mkubwa na huo ubunge wake ni wa kupewa tu ndo maana hapingi jambo lolote kwa serikali!
 
Ndugu watanzania wenzangu kwa kijana yeyote aliye kuwa anajitambua kati kati ya miaka 1980 na 1995 atakubaliana nami kuwa mhe, Mrema amelifanyia mambo mengi Taifa hili hususani ktk nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani na hata akiwa naibu waziri mkuuu, sasa kitendo cha mkosa mali kumtusi mzee huyu wa makamo kuwa anabembeleza mafao yake kwa kuwaunga mkono CCM kikanifanya nijiulize kuwa hivi mkosa mali hatambui kazi zilizo fanywa na huyu mzee kubwa nikajiuliza hivi hawa wabunge huwa wanalipwa mishahara tofauti hadi wanadharauliana kiwango chakuwafanya viongozi wenzao ni maskini? Kwa umri, heshima na hata umaarufu wa mhe, Dkt Mrema mimi nilikuwa namshauri Mkosamali asijitafutie umaarufu kwa kumtusi mzee Mrema na badala yake amuombe radhi mzee Mrema wakulaumiwa ni CCM ndio walio leta hoja.

Mrema nae eti ni Dr.hivi mbona watu wanajiita tu madaktari kwa muda mrefu sana kwa nini wasifikie level ya uprofesa kabisa maana haiwezekani mtu awe daktari miaka 20 asiufike uprofesa.Back to the topic mimi naungana na Mkosamali maana kama si kubembeleza pensheni kwa nini asipewe mapema baada ya kuacha utumishi wa uma
 
kama alivyousotea Dr Mrema, alipewa baada ya kazi zake nyingi zilizoonyesha mafanikio ndani ya Tanzania akiwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu! mrema asingepambana na majambazi yaliyokuwa yametishia uhai wa taifa hili na biashara za magendo pengine nchi ingeingia machafukoni na hata hiyo MD yako usingeipata. TUDHAMINI KAZI ZA WENZETU!
....so dr nyerere...!!!? sio
 
Kiukweli Kauli na Vitendo vya wabunge vijana ndani ya Bunge vinafifisha Nguvu za sisi tunafikiria tunahitaji vijana wengi katka bunge letu hasa ukizingatia ni nchi pekee katka EAC hatuna free youth National council....tunaona kuwa kuwapigania vijana kuwa wengi bungeni hasa wenye lengo la ku_change the country sio kutoa Lugha za dharau kwa wanasiasa au viongozi waliopita....Binafsi nilisononeka sana kwa masikio yangu nikisikia Kauli ya Mkosamali kwa Mh Mrema....alipaswa kumpa heshima hata kwa Umri wala sio uanasiasa wake......Vurugu za mbunge wa Mbeya mjini nazo hazikuleta vijana katka eneo la vijana hasa ktk harakati za kuwapigania vijana kushika nafasi ukweli hata wazee wetu katika maeneo yetu ya uchaguzi ukweli wanatafakari haya.....

Hivi Zitto sio mpinzani? mbona namjua sana kwa jazba mbona hajawai tukana au kutoa kashfa wa yeyote.....!!! Ile kozi yay young political leaders waliopata akina Zitto 2003....nafikir ni wakat wa kuitafutia mitaala..... aliwahi kusema Mwl Jk baba wa Taifa Tabora, akiwahutubia baraza la vijana 1984, alisema " Vijana msiposimama na kuonyesha mnaweza kiakil na kimatendo katka uongozi wa Taifa lenu leo , basi Mtachungwa kama Pundamilia wa Mikumi"

Kwenye suala la vijana tuache ushabiki wa siasa...tuna hoja moja tu....sisi ndio viongozi wa leo..bali kujali chama chako...

VIJANA KWANZA, UZALENDO KWANZA..........

Hivi inshu yake imefikia wapi mpaka sasa? c walisema kafunguliwa kesi polisi?
 
Mrema ni mwakilishi kwa kupigiwa kura kupitia Chama pinzani.
Kama haelewi wajibu wake kama mpinzani ni dhahiri hajitambui na Huo U-docta ni feki.
Namshauri afuatlie hiyo pension yake akapumzike,kwenye siasa hana issue tena.
 
Nimegundua kwenye siasa kuna unafiki mkubwa sana...mf. CDM na CUF leo wameungana kesho itakuwa vingine...NSSR waliiunga mkono CCM kuchukua Halmashauri na kukataa kuungana na CDM..leo wameungana kinafkii.. Mrema ndo hajijambui..labda umri..

hiki chama nacho kipo Tanzania?
 
kama alivyousotea Dr Mrema, alipewa baada ya kazi zake nyingi zilizoonyesha mafanikio ndani ya Tanzania akiwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu! mrema asingepambana na majambazi yaliyokuwa yametishia uhai wa taifa hili na biashara za magendo pengine nchi ingeingia machafukoni na hata hiyo MD yako usingeipata. TUDHAMINI KAZI ZA WENZETU!

Tudhamini ndio nini?
 
Acheni ujinga na ushamba bana...kila mtu dr..dr...mnajua watu wanavyosota kupata huo udr....acheni kabisa bana....yule ni <b>bwana</b>mrema....tena mnafki na msaliti...!!!

Tena wala sio "bwana" bali ni "ndugu" Mrema
 
........hatambui kazi zilizo fanywa na huyu mzee kubwa....Kwa umri, heshima na hata umaarufu wake..... Mkosamali asijitafutie umaarufu kwa kumtusi mzee Mrema na badala yake amuombe radhi mzee Mrema....

We Kafisadi, natumaini bado hujakua...labda kisiasa.... kitendo Mrema alichokifanya Bungeni na ambavyo amewahi kuvifanya achilia mbali mambo ya msingi aliyoyafanya akiwa Waziri; ni mambo ambayo mtu inayekiongoza chama kinachotaka kuchikua dola hakiwezifanya kamwe labda uwe kibaraka na si vinginevyo!
Siasa haina ukubwa kaka; ukishushiwa KOMBORA LA KISIASA usione huyu jamaa, kanidharau; jibu kisiasa na si vinginevyo km unavyojikanyaga hapa kwenye UZI!
 
Tatizo MaCCM huwa hayapendi kusikia ukweli,alichokosea Mkosamali ni nini? amefanya kuwakumbusha VILAZA wa ccm mmlipe mafao yake, na pia ache kujipandekeza, kama ni haki yake adai ila asijipendekeze. HAKI YA MTU INADAIWA NA WALA HAOMBWI, labda wanafanya hivyo wauza UNGA Waliokamata Uchina tu na wale walotia meli moto itally waliotii amri ya mtoto wa Rais KILAZA.
 
Mrema alipofikia ni kama changudoa kisiasa, kumpa heshima huyu mzee unajitafutia laana, wazee wanao hifadhi wezi ni kuwapa za uso tu.
 
Mrema kafanya makubwa enzi hizo, sasa anayabomoa. Huwezi kupewa heshima kwa kuyabomoa mazuri ya awali. Tamaa mbaya. Afu kuna msimfiche Mrema kwenye kichaka cha uzee eti asisemwe na vijana, ni upuuzi. Akiboronga no matter una umri gani, mwambie ajue wapi kaboronga. Kama anaogopa kusemwa kwa kujipendekeza kwake aache siasa. Siasa haina Umri unapata na kutoa madongo
 
Mrema mwenyewe alisema kwamba alijipendekeza kwa CDM wakamtosa,sasa anajipendekeza kwa serikali ya ccm apate chake,pia wamjali jimboni kwake..sijaona kosa la mkosa mali hapo.kayasema aliyoyasema mrema bungeni.
 
Back
Top Bottom