Mkopo wa SGR wa tril 3.3 kwa riba ya 9% kwa miaka 20 tutalipa jumla ya zaidi ya Tshs Tril 7.36 huku riba ikiwa tril 4.06

View attachment 1358881

Kwa mujibu wa Zitto Kabwe mkopo wa ujenzi wa SGR tuliokopeshwa na benki ya Kibiashara tumepewa kwa riba inayoitwa nafuu ya 9% kwa muda wa miaka 20.

Nimejaribu kuichakata kujua hayo malipo tunayalipaje na kaeli reli itazalisha kuaeza kurejesha fedha hizo kwa wakati? Na rejesho kwa mwezi tuzalishe faida isiyopungua bilioni 30 kwa mwezi.
Investment on SGR is not only tied to business where investment costs have to be returned by profitable business where the equilibrium is attained at an intersection of costs and returns curves! Zitto knows all too well that SGR is a long term Socioeconomic venture! Calculate the NPVs as well on a 20 year term to understand economic viability of the investment, economists have done their job already. The project offers wide ranging benefits including services to citizenry! Rapid transport, reliable transport, durable transport, cheaper transport.....Repayment of the loan is not tied to business profits generated by transportation of goods and passengers in the rapid train system only, but by all taxable busines incomes generated around it which contribute to national GDP in the long run.
 
Halafu Kituko cha Serikali ya Magufuli mkopo unaanza kulipwa hata kabla ya reli kuanza kazi.
Kikwete pamoja na uzembe wake lakini asingeweza kusani mikataba ya kichoko namna iyo.
Bandari ya bagamoyo kikwete alitaka kusaini nii!!! Fikiri kabla ya kusema
 
Hivi ni nani atakuja kulipa hiyo. Kama tunahela kuna ulazima gani wa kukopa trillioni 3 halafu tuje kulipa 7. Kwa nini tuko desperate hivyo?
 
Mtoa mada, bila kutuwekea mkataba hapa kuonyesha riba ya 9%, haya ulioandika hapa yatabaki kuwa hadhithi ya kutunga.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Na hiyo ni iwapo mkopo utaishia hapo hapo, lakini ni dhahiri mkopo zaidi utahitajika ili kazi iishe, ama mradi usikamilike lakini deni liwe kubwa zaidi. Kumbuka hawa wanaokopa sasa kusaka kiki za kisiasa hawatakuwa madarakani na pengine duniani, hivyo ngoma itakuwa kwa watakaokuwepo madarakani.
Kimbembe kwa walipa kodi, watakao beba mzigo kupitia tozo mbali mbali zitakazoletwa na serikali.walio madarakani wengine hata kodi hawakatwi pamoja na mishahara mikubwa .
 
Nchi hii kikubwa pumzi tu
View attachment 1358881

Kwa mujibu wa Zitto Kabwe mkopo wa ujenzi wa SGR tuliokopeshwa na benki ya Kibiashara tumepewa kwa riba inayoitwa nafuu ya 9% kwa muda wa miaka 20.

Nimejaribu kuichakata kujua hayo malipo tunayalipaje na kaeli reli itazalisha kuaeza kurejesha fedha hizo kwa wakati? Na rejesho kwa mwezi tuzalishe faida isiyopungua bilioni 30 kwa mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningeshauri kwenye huo mkopo uwanja wa chatto na ile mbuga ya wananyama viwekwe rehani. Siku mabeberu yakija yaje yachukue tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
.

Agreed. Jimbo lote la Chato na hiyo Mbuga ya Chato-Burigi ndiyo viwe dhamana ya mkopo ili mabeberu wakija wachukue hiyo sehemu. Wakifanya hivyo itatusaidia huko mbeleni eneo hilo lisitoe tena rais wakuja kutupa majanga kama huyu aliyepo.
 
Hivi ni nani atakuja kulipa hiyo. Kama tunahela kuna ulazima gani wa kukopa trillioni 3 halafu tuje kulipa 7. Kwa nini tuko desperate hivyo?

Mkuu,hyo ni michongo ya watu ya upigaji,mwisho wa siku mwananchi ndiye atakayelipa.

Maamuzi ya kuijenga hiyo SGR hayakuwa shirikishi,tungeweza kuziboresha reli ya kati na ya Tazara kwanza halafu baadae tukiwa vizuri ndio mdogo mdogo tungeanza na SGR,ila shida hii nchi hakuna ushirikishaji wa mijadala mipana zaidi ili kupata mawazo ya wadau wengi,linalofikiriwa na kikundi fulani cha wachache ndio kinalazimishwa kifanyike,matokeo yake pesa hazitoshi na hakuna cha kupitishwa hata na Bunge kukopa hizo pesa,zinakopwa tu bila kuomba idhini ya wawakilishi wa wananchi(wabunge).

Vizazi vyetu vitapata shida sana aisee kwa haya madeni makubwa tunayowavisha.
 
Serikali ya awamu ya saba ijipange mapema kupokea madeni.




Au watakopa pesa ili kulipa madeni ili madeni ya awamu ya saba yalipwe na serikali zinazofuata kama awamu ya nane na awamu ya tisa.😁
 
Halafu Kituko cha Serikali ya Magufuli mkopo unaanza kulipwa hata kabla ya reli kuanza kazi.
Kikwete pamoja na uzembe wake lakini asingeweza kusani mikataba ya kichoko namna iyo.

Ukikopa kwenye commercial banks lazima ujipange hasa. Hamna grace period kama mikopo ya WB.
 
Back
Top Bottom