Mkopo wa milioni 10 CRDB | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkopo wa milioni 10 CRDB

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njaa, Aug 9, 2011.

1. Njaa

Njaa JF-Expert Member

#1
Aug 9, 2011
Joined: Dec 6, 2009
Messages: 970
Likes Received: 227
Trophy Points: 60
Wakuu naomba ushauri....

Mwenzenu mshahara wangu take home ni 800 000/-, nataka kukopa CRDB kama Ths 10 million hivi ili ninunue kiwanja, siewezi kukopa nje ya CRDB maana hapa kazini wana mkataba na CRDB tu, sasa naomba mnipe mwanga kuhusu huu uamumuzi je ni wa busara? nataka kulipa kwa miaka 3, vipi rates zao? kuna alternative gani kama CRDB ni kimeo?

Jamani nipeni mawazo....

Nawakilisha

2. Prodigal Son

Prodigal Son JF-Expert Member

#2
Aug 9, 2011
Joined: Dec 9, 2009
Messages: 963
Likes Received: 60
Trophy Points: 45
mkuu
nenda bank za wanyonge,access bank, nmb, akiba, crdb nadhani interest rate zao ni kubwa

utazeeka huku unalipa mkopo, na huu mfumuko wa bei utaishije kwa miaka 3 labda uwe una vyanzo vingine vya mapato

3. M

Milano Member

#3
Aug 9, 2011
Joined: Jul 12, 2011
Messages: 37
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

usiende cr mwana bora nnb

4. Dr wa ukweli

Dr wa ukweli JF-Expert Member

#4
Aug 9, 2011
Joined: Feb 28, 2011
Messages: 892
Likes Received: 27
Trophy Points: 45
kama mnamkataba na crdb ni bora ukope huko riba zao siyo kubwa kama access na kwingineko riba yao ni 19% last year labda kama wamechange na mkopo unapata kwa haraka sana.

5. Njaa

Njaa JF-Expert Member

#5
Aug 9, 2011
Joined: Dec 6, 2009
Messages: 970
Likes Received: 227
Trophy Points: 60
Asante sana wakuu (Prodigal son, milano, Dr wa ukweli .....). Ukweli ni kwamba sina ujanja, hapa kazini wana mkataba na CRDB tu, na nikichukua million 10, nitatakiwa kulipa kama Tsh 14,0000 ambapo nitatakiwa kukatwa kila mwezi Tsh 390,0000. Hii ni kiboko ila sina namna, ngoja nijipange ili niingie huu mkataba wa kuongeza umasikini

6. L

LAT JF-Expert Member

#6
Aug 9, 2011
Joined: Nov 20, 2010
Messages: 4,523
Likes Received: 86
Trophy Points: 0
Mkuu .... hongera sana .... pia zingatia sana ID yako inavyotamka

7. Kinyungu

Kinyungu JF-Expert Member

#7
Aug 9, 2011
Joined: Apr 6, 2008
Messages: 4,381
Likes Received: 3,341
Trophy Points: 280
Usikope ukanunue shamba. Huko ni kujitakia umasikini wa mchana kweupe. Kopa uanzishe biashara. Simamia biashara yako vizuri ilipe mkopo na inunue shamba/kiwanja. Utashangaa hadi watoto wako wanaanza shule unalipa mkopo...funguka macho ndugu yangu?

8. Kituko

Kituko JF-Expert Member

#8
Aug 9, 2011
Joined: Jan 12, 2009
Messages: 9,366
Likes Received: 7,002
Trophy Points: 280
Mkuu ukichukua 8,00,000Tsh ukatoa 3,90,000Tsh unabakiwa na 4,10,000Tsh ambayo ni hela inayokupasa kutumia mwezi mzima kwa miaka mitatu,
sio tatizo unaweza kujibana kwa miaka hiyo mitatu, MKUU OMBI LANGU NI KUWA UTENDEE HAKI HUO MKOPO,
usijaribu kwenda kuweka heshima Bar na kutafuta dogodgo wa kukukanda asubuhi na jioni kwa hiyo hela utakayo itabikia kwamiaka mitatu

9. AK-47

AK-47 JF-Expert Member

#9
Aug 9, 2011
Joined: Nov 12, 2009
Messages: 1,381
Likes Received: 6
Trophy Points: 135
Mkopo wa wa kiwanja ama kujenga unauma sana kwa kuwa huwa hauzalishi...ila kama unachanzo kingine cha mapato machungu yanapungua. Chukua CRDB si wabaya mimi nimekuwa nakopa hapo kwa zaidi ya miaka 6, kibaya ni pale walipoongeza kipengele cha mkopo kinachosema iwapo mdaiwa atashindwa kulipa deni lake lote muajiri atawajibika kulilipa.

10. YoungCorporate

YoungCorporate JF-Expert Member

#10
Aug 9, 2011
Joined: Apr 30, 2010
Messages: 388
Likes Received: 7
Trophy Points: 35
mm nilikopa nikanunua gari.....ni tofauti tu ya vipaumbele, taabu ya usafiri ilinishinda......

11. Mutensa

Mutensa JF-Expert Member

#11
Aug 9, 2011
Joined: Feb 20, 2009
Messages: 426
Likes Received: 12
Trophy Points: 35
Madeni hayaepukiki, ndo maana hata USA wanaongelea kuinua dari ya madeni.... Maana yake kujiongezea kiasi cha pesa ambacho wanaweza kukopa. Cha msingi hakikisha ukikopa unazingatia yafuatayo: 1. Pale unapouweka mkopo hakikisha panarudisha hela ambayo ni zaidi ya ile unayolipa kwa mwezi. Kama ni mkopo wa kujenga kwa mfano, hakikisha ni wa kumalizia nyuma ili (kodi ambayo ungelipa) - (pesa unayorudisha kwa mwezi) > 0. Uzuri utamaliza mkopo na nyumba itabaki ya kwako....2. kama ni pesa ya biashara basi (mauzo)-(matumizi ya mwezi)-(manunuzi)-(pesa ya kurudisha) = x. Hakikisha x > 0, halafu inafidia gharama zisizoepukika ( fixed costs) ndani ya muda ambao gharama hizo zinajirudia. Mfano umenunua mwiko wa kukaanga chipsi, je lini utahitaji kuununua tena.Unaweza kuangalia kwa macho tofautitofauti ikitegemea "faida" unaichkulia katika hali gani.

12. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#12
Aug 9, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,826
Likes Received: 22,467
Trophy Points: 280
milioni kumi kiwanja?
kujenga utatoa wapi pesa?
kwa nini hiyo pesa usiizungushe iongezeke?
au uanze ujenzi kabisa uone utakapoishia?

13. Mwenzetu

Mwenzetu JF-Expert Member

#13
Aug 9, 2011
Joined: Dec 16, 2010
Messages: 500
Likes Received: 89
Trophy Points: 45
.............changamka ikiwezekana hata kesho wahi nenda kakamilishe taratibu za huo mkopo,unapo nunua ardhi hakikisha kuwa imesajiliwa au ina hati.Hakika thamani ya fedha kwenye ardhi inapanda sana,kama iko dar ndo usiseme.Fahamu tuu kuwa ardhi haiongezeki.Kiwanja au ardhi ya thamani ya 10mil ya leo baada ya miaka 3 ni 70 mpaka 80mil kwa makisio ya haraka haraka..........

14. Ngwanakilala

Ngwanakilala JF-Expert Member

#14
Aug 10, 2011
Joined: Jun 25, 2011
Messages: 396
Likes Received: 163
Trophy Points: 60
Ungejaribu ku-save kwa miezi kama sita ukawa na kama millioni 4 then ukakopa mil 6 miezi sita from now. hiyo itakuwa rahisi kulipa haraka. Unless una mke au unaishi na GF au kwa wazazi kuishi kwa laki 5 kwa mwezi for 3 years inaweza ikawa ngumu. Tafakari!

15. Jimbi

Jimbi JF-Expert Member

#15
Aug 10, 2011
Joined: Aug 16, 2010
Messages: 871
Likes Received: 23
Trophy Points: 35
fuata moyo wako mkuu

16. Njaa

Njaa JF-Expert Member

#16
Aug 10, 2011
Joined: Dec 6, 2009
Messages: 970
Likes Received: 227
Trophy Points: 60
Asanteni wakuu kwa ushauri wenu....

17. A

Akiri JF-Expert Member

#17
Aug 10, 2011
Joined: Sep 21, 2010
Messages: 1,447
Likes Received: 63
Trophy Points: 145
mi nina mkopo wa accessbank kama ungekuwa unalejesha ndani ya mwaka mmoja ungerejesha 13,500,000 coz mimi nilichukua 2m kwa mwaka narejesha 2.7 mikopo yao inatoka kirahisi kama una dhamana na mdhamini mwenye kipato kikubwa. kwenye dhamana kuna unafuu kidogo kama una gari wanaliangalia then wanakaa na kadi ya gari. niliwahi kuenda easy finance wanamasharti yasiyo tekelezeka

18. Husninyo

Husninyo JF-Expert Member

#18
Aug 10, 2011
Joined: Oct 24, 2010
Messages: 23,814
Likes Received: 583
Trophy Points: 280

ni rahisi kuongea ila biashara ina risk kubwa kuliko hicho kiwanja. Tena biashara ambayo ndio kwanza anaanza!!

19. Mutensa

Mutensa JF-Expert Member

#19
Aug 10, 2011
Joined: Feb 20, 2009
Messages: 426
Likes Received: 12
Trophy Points: 35

Risk is the actual grammar of business language. If you cannot embrace grammar, you will never speak a good language.

20. Husninyo

Husninyo JF-Expert Member

#20
Aug 10, 2011
Joined: Oct 24, 2010
Messages: 23,814
Likes Received: 583
Trophy Points: 280
tunajua high risk high returns ila kwa case ya huyu kuchukua mkopo kuanza biashara simshauri. Bora ingekuwa ni mwendelezo wa biashara hata trend ya income angekuwa anajua.
Anyway, yeye ndio mwamuzi wa mwisho.

Loading...