Wadau,
Naomba ufafanuzi wa sheria juu ya mikopo ya taasisi za fedha.
Nilichukua mkopo Stambic Bank kwa dhamana ya mshahara kutoka kwa mwajiri wangu lakini kabla sijamaliza mkopo huo kumetokea kuyumba kwa uchumi hapa kazini hali iliyopelekea kukosa mishahara kwa zaidi ya miezi sita sasa kutokana na shirika ninalofanyia kazi kutegemea wafadhili kwa 100%
Kutokana na hali hiyo mambo kadhaa yamejitokeza na kupelekea nijiulize maswali yafuatayo;
1. Ni kwanini kuwe na adhabu wakati benk inafahamu kuwa kwa sasa sina mshahara na dhamana yangu ni mshahara?
2. Kwa nini adhabu hiyo isianze kutumika baada ya tarehe ya mwisho ya urejeshaji mkopo (Oct, 2015)? Kwani katika kipindi hiki harakati ninazofanya zinaweza kuzaa matunda na hata nikaweza kurejesha kiasi chote hata kabla ya tarehe hiyo.
3. Mwajiri anawajibika vipi na deni hilo? Au nini msaada wake kisheria?
4. Je, ni sawa kisheria benk kupiga mnada mali za familia kama shamba, nyumba/gari amabavyo nimevipata nje ya mkopo huo?
5. Je, ni sahihi benk kuendelea kunipiga fine hata baada ya kuonesha nia ya kurejesha kidogo kidogo kwa kadri ninavyopata?
Majibu ya maswali hayo yatanipa mwanga wakuu, naomba kuwasilisha.