Mkongo wa mawasiliano ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkongo wa mawasiliano ni nini?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtego wa Noti, Feb 4, 2011.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Ndugu wanaJf, mimi ni mtanzania ila bado kuna kitu naomba mnisaidie. Nimekuwa nikipita katika maeneo mbalimbali ya nchi na ninaona kuna watu wanachimba mitaro na kuzika nyaya fulani maarufu kama mkongo wa mawasiliano. Kinachonishangaza mimi ni kuwa sifahamu ni jinsi gani waya ulio ardhini utasaidia katika kurahisisha mawasiliano. Au wataunganisha hayo ma-cable kwenye hii minara tuanyoiona imesimikwa mitaani? Hii itafanyeje kazi jamani? naomba mnielezee kwa simple language ili nielewe ni jinsi gani huu mkongo unafanya kazi.
  Asante sana waungwana kwa kukubali kunisaidia katika hili.
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hapo zamani mawasiliano ya Internet yalikuwa yanapita kwenye waya za simu na satellite, ndani ya nchi na africa. yalikuwa

  Lakini kutoka Africa na kwenda Europe na Mabara mengine ilkuwa ni kwa njia ya Satellite pekee, sasa huu mkonga umeunganisha africa na Continent nyingine kwa njia ya huu mkonga

  Sasa ni kwamba ni nini tofauti ya huu mkonga na zile njia za simu za zamani ? Huu mkonga ni Fibre Optic yaani signal inakuwa ni mwanga, kwa hiyo hii ina kasi zaidi ni kama badala ya kutumia barabara za uchochoro wa magari kupita sasa wamejenga Highway

  Kwa hiyo mawasiliano yataendelea kupita kwa njia za satellite kama zamani pia na kwenye huu mkonga...,

  Kwa mfano wa magari mkonga ni kama Highway kubwa imejengwa ambayo itafanya magari mengi yapite na kwa kasi.., pia tuseme zamani kwenda ulaya kulikuwa kuna usafiri wa meli peke yake lakini sasa kutakuwa na usafiri wa ndege.

  Kwahio huu Mkonga ni kama barabara kubwa zinasambazwa nchi nzima ili magari yapite kwa urahisi na kwa kasi
   
 3. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  asante sana Voice OfReason, kwa hiyo hizo optic fibres zitaunganishwa kwenye hii minara au zitakuwa zinachukua signals zikwa ardhini hivohivo? au kutakuwa na station maalum ambayo hizo fibres zina chukua na kurusha signals?
  Thanks for you kindness in elaborating this to me!
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Unajua internet ni (web) kama ile nyumba ya buibui au barabara

  Kwahiyo kutoka kwangu signal inaweza ikapita kwenye mkonga then satellite then mkonga then satellite then ndio inafika kwako.., inategemea na traffic jams (mfano wa magari kwenye barabara, Kufika Pugu kuna njia zaidi ya moja) kwahiyo hizi zote zitakuwa interconnected kama barabara zilivyo connected zote.., uzuri kwa sasa badala ya signal kutoka marekani kuja africa kutumia satellite peke yake, sasa kutakuwa na huu mkonga

  Hata hiyo modem yako ya Zain/Zantel/Tigo..., signal inaweza ikatoka kwako kwa njia ya satellite mpaka huko kwa hao Zain/Zantel/Tigo (Gateway) ambapo hapo kutakuwa kuna barabara nyingi (Mikonga na Satellite) kupeleka signal yako inapokwenda.

  Pia kumbuka hata ukituma Picha ili ifike kwangu hiyo picha inavunjwa vunjwa kwenye pcs ndogo ndogo alafu hizo pcs (pkts) zinatumwa kwa njia tofauti alafu zikifika kwangu browser yangu inazikusanya zote na kuziunganisha ili nipate full picha.., kwahiyo huenda pua ya picha ilipitia njia ya mkonga then satellite wakati sikio lilipita kwenye satellite peke yake.
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160


  interesting!!! you are very GREAT!!! nashukuru sana mkuu maana mi nilikuwa nashangaa naona jamaa wanachimbia nyaya...kumbe ndio iko hivyo? now i understand!!! hapo kwenye red nimecheka mno....big up
   
 6. GATS

  GATS JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 240
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante umetufumbua wote ambao hatukuwa na uelewa sawa sawa
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Alafu walidai hii kitu italeta mapinduzi ya mtandao kwa kushuka bei lakini naona siku zinasonga tu bei ile ile
   
Loading...