Wakuu katika maazimio ya bunge , wamesema kua Stanbik bank itangazwe kua ni bank ya kutakatisha pesa, naomba kuuliza kwa nini mkombozi bank hawajaitaja? Kuna nini hapa? Nini tofauti ya alichofanya stanbink bank na Mkombozi bank?
The bias was obvious and intentended from what they presented, binafsi kufukuza watu kazi kwa sababu ya mapendekezo yanayo tokana na kamati za wabunge sasa nimekosa nayo imani.
Kuna kila sababu ya kubadilisha huo mfumo enough of bunge kutumika kuwang'oa walio mbogo kwa wahalifu.Ni hatari kuendesha nchi kwa utaratibu huu.
Uliyasema lakini for the most it was just common sense given the facts mapendekezo ya kamati hayaku make sense in the end.Naam, nilyasema kama hayo baada tu ya kusikia hoja za kamati. Uongo ulikuwa mwingi kuliko ukweli.
Kama waliingia bank na magunia bank huwa kuna CCTV camera hivi PCC wameshindwa pata back up ya tarehe taja ili waondoe huu wizi. Maana kila MTU hataonekana alivebaje hayo manoti
1) kwanini benk ya mkombozi haijatajwa kama ni benk inayotakatisha pesa?
2) Pro tibaijuka alipata pesa kutoka mkombozi kwanini ameingizwa wakati mkombozi haikutajwa?
3) kwanini walio pata hizo pesa wote ni dini moja?
4) kama spika anahisi kuna waliochukua hongo bungeni kwann asiunde kamati kuchunguza?
5) kwanini jk alimchagua muhongo kutoka nje ya bunge inamaana aligundua bungeni hakuna mwenye uwezo?
6) Pinda alisema hakuna pesa za umma, muhongo nae alisema hakuna pesa za umma kwanini anatakiwa ang'oke mmoja?.
7) je unafikiri ktk mawaziri wote waliopita wa hii wizara nani amefanikiwa zaidi?
( short answer please!!!)
Huko Stanbib zilitoka 73b cash,yaani not za elfu kumi kumi milioni 7.3 ambazo uzito wake wake ni karibia tani tano! hapo cjui walitumia fuso kubeba?
Kuna swala la kujiuliza kuhusu kiwango cha CASH mteja wa bank anaruhusiwa kudraw kutoka bank, kuna watu humu wanasema ni million 10, mimi nasema hapana, kwani in practice watu wengi wanafanya miamala ya cash zaidi ya 10million, hapa inabidi bankers watupe sheria hiyo inasemaje, kwani kama mtu anataka kudrwal cash kwenye account yake kwanini awekewe kiwango? mbona mtu akitaka kudiposit cash kiwango chochote hazuiwi? iweje akitaka kudraw azuiwe?. Chukulia mfano watu wanaofanya biashara za Cash Zaidi kama vile minadani, n.k wao watahitaji cash kiasi kikubwa sana, pia watu wanaonunua madini migodini, huwa wanabeba cash, kama 10million ndio kiwango cha juu, je wangeweza kufanya biashara?
mkuu nina vitu vingi tu ninavyoviona na vya kusema kwenye hili (sorry kama litakugusa);Mkuu kuna kitu unataka kusema sio?
Naamini zile bilioni 73 zilizotoka kwa cash within 2 days,kwenye viroba na magunia ya lumbesa, pale Stanbic bila kudislose, majina ya walipwaji, ambayo ni ukiukwaji wa hali ya juu wa taratibu za BoT, ambao hauruhusu transaction yoyote inayozidi kuwithdraw more than 10 million in cash.
Hiyo ndiyo sababu iliyopelekea, Mwenyekiti wa PAC , Zitto Kabwe, alielezee tukio hilo kuwa linawezekana tu kutokea kwenye nchi ambayo mifumo yake ya kiutawala,itakuwa imecollapse, kama vile Somalia.
Sasa hapo ndipo linapokuja swali kubwa kuwa, ni kitu gani kilichofanya vyombo vyote vya ulinzi na usalama, vishikwe na ganzi na kigugumizi katika kulidhibiti tukio hilo siku hizo 2, kama siyo kwa the highest office in our country, 'kulibariki ' tukio hilo?!
Kwa kuwa hakuna siri inayoweza kudumu, inayoimvolve mtu zaidi ya mmoja, naamini kabisa ipo siku, hili suala la ubebaji wa noti kwa viroba na magunia ya lumbesa pale Stanbic, ni lazima one day litakuja bumbuluka tu lazima!
ile sakata la mwanasheria kijana wa tanesco aliyeandika barua ya kuacha kazi inasemekana kunamtu alimlazimisha aandike barua hiyo na ni mjumbe wa bodi ya tanesco ni nani huyo mtu naomba mnijuze wakubwa
Inaelekea zilizimwa kwa maagizo ya the highest office in town!Yaani hapa najiuliza kuwa CCTV zilikuwa hazifanyi kazi siku hiyo.?
Nimekosa jibu