Mkojo wa mjamzito: Biashara nyingine ya siri isiyojulikana na wengi

Hahaah, mwishoni mwa sredi umenichekesha mkuu One! Eti "Boya wewe"

Halaf kuna jamaa yang flan alikuw ni mtu wa totoz, sasa kila aliyekuw akipita nae lazma aambiwe ana mimba yake na kashagharamikia kuabort kam mimba 5 hv na kila akimaliza kuhudumia inakuwa ndo mwisho wao.
Boya huyo...
 
Mji mzito sana huu
Kuna mambo yanaendelea kimyakimya na chini kwa chini huku baadhi wakibaki na vicheko baada ya kupiga pesa ya mabwege na huku wengine wakibaki na majuto na kujiapiza kutorudia tena.

Baadhi ya wanaume wenye macho juu Wamepigwa sana kwenye hili jambo.. Naamini hata kati ya wasomaji watakaosoma hii mada ni wahanga wa hili jambo.

Ujumbe wa BABY NINA MIMBA YAKO.. huwachanganya sana mabazazi na wale wanaojiita mabaharia bila kuwasahau wazee wa mjini... Wazee wa bandari... Unapopata ujumbe kama huu toka kwa mchepuko wako ambaye anaweza kuwa mke wa mtu bandia au halisi, mwanafunzi (halisi au bandia) danga nk unachanganyikiwa kabisa.. Cha kwanza kuwaza ni mkewako nyumbani... Mpenzi wako... Kazi yako ama maisha yako.

Kuna wanawake siku hizi hii ndio biashara yao kubwa na inawalipa vizuri tuu.. Unakutana na binti au mdada mzuri kweli unatupa nyavu zinanasa kimaskhara kabisa lakini unapewa onyo mapema... Mimi ni mwanafunzi au mimi nina mtu wangu au mimi ni mke wa mtu.... Bila kutafakari hilo onyo unasema utafanya siri.. Unakubaliwa unakula mzigo kiboya kabisa

Bila kujijua kuwa uko kwenye foleni ndefu ya kubambikiwa ujauzito feki mwanaume kidume wewe unajiachia kwa raha zako.. Ukimhitaji mtoto unampata unakula anasepa. Na anaweza kabisa awe hakusumbui kwa shida ndogo ndogo.... Usijione mjanja ukadhani umepata... Tambua tu umepatikana

Siku yako ya kupigwa ikifika unapata ujumbe mbaya wa ujauzito na unaambiwa wazi kabisa kuwa hayuko tayari kuzaa kwa wakati huo... Kwahiyo mzee inabidi udhamini mchezo... Na ili kukuaminisha mnaenda wote hospital kupima.. Kumbe tayari mwenzako ana kichupa chake cha mkojo wa mtu mwingine kabisa mwenye ujauzito amekificha kwenye chupi yake

Ni wazi hutamsindikiza mpaka chooni hata akikuomba.. Sana sana utaishia mlangoni.. Yeye huko ndani atabadili tu mkojo toka kichupa alichokuja nacho kwenda alichopewa hospital... Majibu yakitoka... Imooo.. ...
Kifuatacho ni gharama za kutoa mimba tena anachagua Marie Stopes.. Ukikomaa kwenda naye mpaka daktari atapangwa...
Baada ya hapo unahudumia 'mgonjwa' na akipona unapigwa chini.. Mchezo unaendelea kwa maboya wengine....

Wanaonunua mikojo ya waja wazito wengi wao sio kwa ajili ya ushirikina bali kwa ajili ya kuwapiga mabazazi... Najua umesoma huku ukikumbuka pesa ulizotoa kwa ajili ya abortion huku ukijisifu kwa wanaume mwenzako kuwa una mbegu Kali sana.. Ukigusa tu kitu na box... unaibiwaaa...Boya WEWE
Kuna ka kicheche kamoja kalitaka za hivyo nikakastukia.Kakitaka tukapime hospitali nikakambia kaje nikapime kakagoma baadaye kakadai imoo,niliookabana Sana kakajifanya kameitoa na Mimi nikakabania hapohapo,nikapiga chini.
 
alimkomesha. Ndio dawa ya midume isiyotaka kutulia na wake zao. Mtu unajua kabisa huwezi kuhandle matokeo ya dhambi zako unaenda kuchepuka pekupeku unategemea nini

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiwa unamsimamo hakusumbui,labda kama huna nguvu kwa mkeo,kwangu akijaribu namaliza kesi asubuhi saa1 moja na ushindi juu....namheshimu mke sio kumuogopa
 
Sasa mabaharia wenzangu kama tulivyoazimia kwenye maazimio yetu ya 2020/2021 ni lazima mimba moja wapewe wababa hata 10. Yani yoyote aliyekupitia hata one night stand wewe mbambikizie tu n hakikisha wote wanhudumia ipasavyo. Kam tulivyokubaliana umakini unahitajika ili usistukiwe.
Na hata kama huna mimba jithidi uwabambikizie mimba hewa kuhusu mkojo tulishaelekezana ni wapi mkojo unapatikana kwa bei nafuu. Msikubali kupimwa mkojo gest maana hapo sio maabara.
Mbinu zote zitumike vizuri kuhakikisha hawastukii mbinu za kivita
Ujumbe tumeusikia baharia,sasa tutakua tunafukua mtaro tu ndio family plan
 
Kuna ka kicheche kamoja kalitaka za hivyo nikakastukia.Kakitaka tukapime hospitali nikakambia kaje nikapime kakagoma baadaye kakadai imoo,niliookabana Sana kakajifanya kameitoa na Mimi nikakabania hapohapo,nikapiga chini.
 
Ndo masna utashangaa mwanamke wa mbagala anakwenda clinic Sinza palestina !!
Kweli nikupe ongera kwa kufikiria na kupata hili na kupost pia.
Ulichopost kina ukweli ndani yake wako wengi wakina mama wa aina hiyo ya kihuni.
Wako na wengine mimba moja baba wa mimba hiyo wako (10) na wote wanaitumikia hiyo mimba na wajuani na kadi za clinic ya mimba zina kuwepo idadi hiyo kila anaetaka aone kadi hupewa ilioandikwa jina lake.
Na vituo vya huduma viko sawa na idadi ya baba wa hiyo mimba hapo upo?
 
Neno la ziada...!!!
Kuna mdau kanicheki hapa akinilaumu kwa hii mada.. Kumbe hizi ishu zinafanyika hata hapa JF... Sikuwa na fununu yoyote wala tetesi.. Sikumuandika mtu.. Ni coicedence tu imetokea...
Nasema kweli na mbele za Mungu sikumlenga yoyote hapa jukwaani wala hakuna popote niliwahi kujadili na yoyote kuhusiana na hili
 
Nunua URINARY PREGINANCY TEST. Anachuchumaa chini namuona anaukojoa naupima. Kwisha habar yake. Iko hivi mm ukitaka kunitapeli labda niamue mm kwamba ngoja huyu binadamu nimpe hela anashida sana wacha nimpe kidogo vihela atatue shida zake. Kwa staili hii siwezi pigwa labda ije staili nyingine
 
Akikwambia baby nina mimba yako.. Kamkinge mwenyewe mkojo halafu kanunue KIPIMO mwenyewe upime mwenyewe na bado unahitaji kujiridhisha na tarehe pia
Hii unaweza kuikwepa kama unatumia akili kidogo tu maana kipimo cha mkojo uwa kinasema mimba ina miezi mingapi. Sasa kama wewe unajua ulicheza mwezi mei halafu mimba ina miezi mitano si unajua unapigwa. Ni ngumu sana hapa kumpata mtu ambaye ni smart unless awe amepanga na daktari
 
Nunua URINARY PREGINANCY TEST. Anachuchumaa chini namuona anaukojoa naupima. Kwisha habar yake. Iko hivi mm ukitaka kunitapeli labda niamue mm kwamba ngoja huyu binadamu nimpe hela anashida sana wacha nimpe kidogo vihela atatue shida zake. Kwa staili hii siwezi pigwa labda ije staili nyingine
Haha noma Sana but UPT inaweza kusoma positive wiki mbili baada ya mimba kutolewa
 
Back
Top Bottom