macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,846
- 39,714
Mjini kuna mengi. Ni kweli siku hizi kinadada ni moja ya kundi lenye matapeli sana. Kuna baba mmoja, ni mtu mzima na ameoa na ana cheo kikubwa tu serikalini. Katika kuchepuka akazaa na binti mmoja. Aisee huyo baba alikuwa ananitia huruma sana kwani alikuwa anaendeshwa kama gari.Karibu Kilingeni
Yule kimada alikuwa anamkamua hasa kwani yule baba alifanya kosa la kumwomba sana sana issue ya kuzaa na yule binti iwe siri na mtu yeyote asijue. Na zaidi alikuwa anamwogopa sana mke wake. Basi ifikia kipindi yule kimada akamtafutia na mwanasheria feki.
Akamtishia fedha alizokuwa anatoa hazitoshi na asipoongeza atampeleka mahakamani. Basi yule baba alikuwa anaomba sana na ilibidi awe anamtumia fedha nyingi.
Mwenye akizipata anaenda kutanua... sijui ilikuja kuishiaje kwani nilihama pale nilipokuwa naishi, karibu na huyu dada.