Mkoa wa Tabora upunguzwe ukubwa

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,759
Reaction score
37,374
Mkoa wa Tabora ni mkubwa sana! Kuna vijiji hata mkuu wa mkoa amalize muda wake kuvifikia ni ngumu.

Mkoa wa Tabora mkiupunguza na kutengeneza mikoa mtasaidia kufikisha huduma, leo nimeshangaa kuona watu Tabora kama Kaliua wakija Kahama kupata huduma ya afya.

Tabora kuna wahamiaji wengi wamejificha huko ususani warundi, wanyaruanda na wakongo, kuna vijiji na mapori mengi mpaka kuna sehemu huduma ni ngumu kufikia.

Serikali tambueni ili.
 
Ni kwel Tabora huwa ni chaka la wakimbiz kuna sehem hazifikiki na ni salama kwa wakimbiz, kina wadau huko wanakwambia n kama serikal imewasau
 
Sio Tabora tu Bali ata Morogoro na Kagera[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Igunga, Nzega na Uyui ziunde mkoa wao. Zinaweza kuzaa wilaya 5 au 6 kwa kugawanya Nzega na Uyui. Nzega iwe mkoa
 
....na ni kati ya mikoa yenye kiwango kikubwa cha umaskini.
 
Hivi morogoro mnaijua vizuri kweli wadau? Kutoka moro mjini mpaka mlimba ni kilomita 395.hapo utaona namna gani watu wanapata ugum wa kufuata huduma za kijamii. waangalie na huu mkoa ase
Vip Barbara za moro mfano huko mlimba zinapitika kweli? Tuweke probox zetu
 
Wananchi wanahitaji service delivers SIO utitiri wa mikoa au wilaya nchi hii ilitakiwa iwe na mikoa 8 tu,ukubwa wa serikali yetu ni mkubwa mno,Zimbabwe wana chini ya 15 Botswana chini ya 15,Zambia chini ya 15,Namibia 🇳🇦 chini ya 15,na nchi zote hizi hazitofautiani sana na ukubwa wa nchi na Tanzania yetu hii,na nchi zote hizo zinapiga hatua kimaendeleo kuliko sisi wenye mikoa zaidi ya 25 na wilaya zaidi ya 100 huu ni upuuzi, huku lingusenguse tunahitaji huduma bora za kielimu maji, matibabu, usafiri etc etc sio kuniongezea kodi nyingine ya kulipa watumishi wa mkoa mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…