Mkoa wa Dar es Salaam ni mchafu; Amos Makalla fanya ziara kujionea

Myfancyface

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
948
900
Salaam Mkuu wa mkoa,

Nikiwa mkazi wa Dar es Salaam hasa Ilala Jiji, nimeshuhudia kuendelea kuchafuka kwa jiji hili.

Ulipoteuliwa nilipata matumaini ya mabadiliko hata kidogo. Hali ni mbaya; mitaro imeziba na karatasi zimesambaa sehemu nyingi.

Jiji la Ilala na vitongoji vyake vinaongoza kwa uchafu kuanzia Kariakoo na sehemu nyingine (ikifuatiwa na Temeke, Ubungo na Kinondoni (Kigamboni sijatembelea sehemu nyingi)

Fanya ziara ujionee, kama unatuma watu watakuwa wanakupa taarifa ambazo sizo sahihi.

Wasalaam

Mkazi wa Jiji (Ilala)
 
Back
Top Bottom