Mkoa upi naweza kwenda kutulia kimaisha?

Merchante

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,292
2,679
Wasalaam! wanabodi.

Ni matumaini yangu wengi mko salama na kwa wale wenye madhila mbalimbali basi yule unae muamini akapate kukuponya.

Niende moja kwa moja katika mada husika, kama kichwa kiavyojieleza hapo juu.

Nimekuwa nikiishi katika mikoa mbalimbali katika shughuli za kujiingizia kipato huku nikijaribu kutafakari mkoa gani nikae kati ya hiyo lakini bado nakua nashindwa kuamua wapi nitulie.

Hivyo basi, nimeamua kushare nanyi mada hii ili kila mmoja kwa uelewa na uzoefu wake apate kudadavua ni mkoa gani ambao sasa naweza kutulia na kutengeneza pesa.

Hapa namaanisha; mkoa wenye mzunguko mkubwa pesa, mkoa wenye fursa nyingi (ingawa fursa ni popote ila zinatofautiana katika urahisi wa upatikanaji) nk.

Kikubwa mkoa wenye mzunguko wa pesa na maisha ya wastani.

Kwenu wakuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkoa wowote uleee waeza enda cha msingi usilete ujuaji kuliko wenyejii...waheshimu wazee na woteee...utafanikiwa...all the best for 2020, ufanikiwapo ukuje tupa feedback
 
Nenda Moro, nilikaa pale Mazimbu kwa mda wa mwezi ivi , bei ya chakula ni ndogo mno, yaani ni nusu ya Dsm wa wastani
sema mzunguko wa pesa ni changamoto mno
 
Merchante,
Dar es salaam.
Pesa nje nje, inategemea kasi yako ya kujituma.
Bisahara ni watu, Dar ina watu wengi kuliko Mkoa mwingine wowote ule Tanzania.
Unaweza ama nunua au uza vitu Kariakoo. Kariakoo ni jalala linalomwaga na kupokea.
Sio lazima umuheshimu mtu, kila mtu yupo kivyake.

Ila kama Mzembe, mvivu, mwingi wa aibu. Nenda kaishi kisiwani utempele.
 
Back
Top Bottom