Lyrics Master
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 482
- 681
VERSE 01;
kimo cha hekima za ndugu sasa ni dhaifu,
imani zao chache na wamekosa uaminifu,
wako radhi kuua ndugu na kumdhulumu mkufu,
au kama si kumuua basi watamuacha na upofu,
wakati tafsiri wa hali hii ni upotofu,
nikiwa kama mkiwa ndani ya dimbwi la matatizo,
maana yake nimefiwa na haki zimekwenda likizo,
kifo cha wazazi wangu kimenipa shinikizo,
kuishi bila wazazi maisha yangu maigizo,
kwani sina muongozo,
ndugu wa ukoo wangu kuishi nao kwa mzozo,
kula na kulala kwangu kwa shida na mizevezo,
ona haka kamchezo,
nyumba ya pili imeibiwa naambiwa ni mimi,
huku mjini hakuna shamba naambiwa silimi,
uonevu kwangu hauishi, vibao mpaka makonzi,
nisilie mtoto wa kiume nisiwachulie kwa majonzi,
mlo wa siku tuu naupata kwenye njozi.
chorus; Feruz
Ningeweza ningeomba wazazi wangu warudishwe duniani,
Ningeweze ningeomba wazazi wangu warudishwe duniani,
kwani mateso ninayopata nahisi kama nimetelekezwa peke yangu jangwani,
nguzo zangu zote zimeanguka sasa sielewi nitaokolewa na nani,
mkiwa mi najikongoja, mkiwa mi najikongoja,
dunia naiona chungu naona bora niwafuate mbinguni tuwe pamoja
VERSE 02:
sasa moyo wangu sultan bado unasaka likizo,
mbona cha mtu sitamani na bado kuna matatizo,
unayekula chips kuku mimi sielewi hizo,
kwangu ugali na maharagwe yenye uozo,
sitaki maneno sababu nimeshahusiwa,
nikiishi na ndugu baki nikubali kubaguliwa,
nione kawaida hali ya kutapeliwa,
mpaka mizimu ya wazazi wangu itakapofunguliwa,
mkiwa nipo njia panda,
saa kumi na mbili jioni na kiza chaanza kutanda,
bundi na mindege ya ajabu angani waanza kuranda,
sauti zao za mauti hazifanani na vinanda,
kila siku miguu yangu mizito mkiwa nashindwa kwenda,
vumbi la njia panda machoni linanishinda,
narudi hali ya utoto sina kauli mfano wa kinda,
moyo unaniwaka moto na umauti unaniwinda,
siulizi ukiwa wangu na dhiki kanipa nani?
ikiwa mambo haya hayana ugeni ulimwenguni,
mwenye mioyo safi mola anawafahamu,
tutaonana Paradiso huku tukitabasamu,
walio kinyume na haki makazi yao Jehnamuuuuuuu,
as-salamu aleykum