The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 3,613
- 9,272
Waache waje..Kuweni waangalifu. Hii ni dormant ID. Ipo tangu 2011. Hii ni ID ya kazi. Wenye D mbili bila shaka mtakuwa mmenielewa. Kuweni waangalifu!
View attachment 3364754
Na ukiona hivi, maana yake dawa ya sindano za NO REFORMS NO ELECTION zimeingia sawasawa, wanatoka kupima upepo, kutafuta opinion....
Ukiona hivi, ujue ni giza limeingia kwa popo kutoka walikojificha...
Wewe hebu angalia tu hoja zake. Ni purely za ki - CCM...
Hana hata akili za kufikiri vyema...
Kwamba, tuingie kwenye uchaguzi kwa sheria na tume ileile iliyokwisha ku - prove failures halafu utegemee matokeo tofauti..?
Huyu jamaa Dr Adam Francis bila shaka udaktari wake ni wa kupewa tu na si wa kutumia akili darasani...
Ushauri wake huu, laiti ungekuwa ndio enzi za kina Nelson Mandela, basi South Africa mpaka leo ingekuwa bado chini ya wazungu wabaguzi wa rangi...!!
Ushauri wake huu, ungekuwa ndio wa enzi za Julius K. Nyerere na TANU yake, basi Tanganyika mpaka leo ingekuwa chini ya ukoloni wa Mwingereza...!!
Dr Adam Francis sikiliza bwana
Ule woga na utu kidogo wa kuruhusu chaguzi huru, za haki na za wazi kwa kiwango fulani kama ilivyokuwa back in 2015 na kurudi nyuma kwa sasa Tanzania haupo na hauwezekani tena...!!!
And actually the reason is very simple, na ni kwamba, CCM wameshakula nyama za watu na hawawezi kuacha kula asilani kwa maneno laini na ya kubembeleza unless itumike nguvu kuwafanya waache...!!
Kwa hiyo your advice is nonsense and it can't be accepted by free minded people..
Vita imeanza na haitakoma mpaka uhuru wa pili wa Tanganyika upatikane. We understand kwamba, you don't care anymore. Mnaweza kuendelea na kufanya mliyozoea kufanya, kujiweka kuwa viongozi kwa nguvu pasipo ridhaa ya wananchi. Endeleeni, lakini mna muda mfupi sana kufurahia matunda ya udhalimu wenu and THE PAYBACK IS COMING FAST BEFORE YOU...
Waambie CCM wenzakohivi, kama ina wanachama watiifu 13,000,000 kama inavyojidai, kwanini waogope uchaguzi huru, wa haki na wa wazI? Kwani wanaogopa ku - champion electoral system reforms kuanzia ktk katiba hadi kwenye sheria zetu za uchaguzi..?
Ni rahisi tu. Watanzania tunataka hicho, kisha twendeni kwenye uchaguzi kwa pamoja. Ashindae, ashinde kwa haki na ashindwaye, ampongeze aliyeshinda.
Mr Dr Adam Francis ugumu kwenye hili uko wapo? Kwanini mnang'ang'ania kuishi mkiwa mbeba roho ya wizi na dhuluma ndani yenu? Hamuogopi hukumu ya HAKI ya adhabu yenu toka kwa mwenyezi Mungu iliyo mbele yenu..?