PreGE2025 Mkitaka reforms mkapige kura

PreGE2025 Mkitaka reforms mkapige kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Waache waje..

Na ukiona hivi, maana yake dawa ya sindano za NO REFORMS NO ELECTION zimeingia sawasawa, wanatoka kupima upepo, kutafuta opinion....

Ukiona hivi, ujue ni giza limeingia kwa popo kutoka walikojificha...

Wewe hebu angalia tu hoja zake. Ni purely za ki - CCM...

Hana hata akili za kufikiri vyema...

Kwamba, tuingie kwenye uchaguzi kwa sheria na tume ileile iliyokwisha ku - prove failures halafu utegemee matokeo tofauti..?

Huyu jamaa Dr Adam Francis bila shaka udaktari wake ni wa kupewa tu na si wa kutumia akili darasani...

Ushauri wake huu, laiti ungekuwa ndio enzi za kina Nelson Mandela, basi South Africa mpaka leo ingekuwa bado chini ya wazungu wabaguzi wa rangi...!!

Ushauri wake huu, ungekuwa ndio wa enzi za Julius K. Nyerere na TANU yake, basi Tanganyika mpaka leo ingekuwa chini ya ukoloni wa Mwingereza...!!

Dr Adam Francis sikiliza bwana

Ule woga na utu kidogo wa kuruhusu chaguzi huru, za haki na za wazi kwa kiwango fulani kama ilivyokuwa back in 2015 na kurudi nyuma kwa sasa Tanzania haupo na hauwezekani tena...!!!

And actually the reason is very simple, na ni kwamba, CCM wameshakula nyama za watu na hawawezi kuacha kula asilani kwa maneno laini na ya kubembeleza unless itumike nguvu kuwafanya waache...!!

Kwa hiyo your advice is nonsense and it can't be accepted by free minded people..

Vita imeanza na haitakoma mpaka uhuru wa pili wa Tanganyika upatikane. We understand kwamba, you don't care anymore. Mnaweza kuendelea na kufanya mliyozoea kufanya, kujiweka kuwa viongozi kwa nguvu pasipo ridhaa ya wananchi. Endeleeni, lakini mna muda mfupi sana kufurahia matunda ya udhalimu wenu and THE PAYBACK IS COMING FAST BEFORE YOU...

Waambie CCM wenzakohivi, kama ina wanachama watiifu 13,000,000 kama inavyojidai, kwanini waogope uchaguzi huru, wa haki na wa wazI? Kwani wanaogopa ku - champion electoral system reforms kuanzia ktk katiba hadi kwenye sheria zetu za uchaguzi..?

Ni rahisi tu. Watanzania tunataka hicho, kisha twendeni kwenye uchaguzi kwa pamoja. Ashindae, ashinde kwa haki na ashindwaye, ampongeze aliyeshinda.

Mr Dr Adam Francis ugumu kwenye hili uko wapo? Kwanini mnang'ang'ania kuishi mkiwa mbeba roho ya wizi na dhuluma ndani yenu? Hamuogopi hukumu ya HAKI ya adhabu yenu toka kwa mwenyezi Mungu iliyo mbele yenu..?
Changamoto kubwa ya nyinyi wenzetu ni kuwaza kuwa mnayo hati miliki ya usahihi wa mawazo. Mtu asipoamini katika mnayoyaamini nyinyi mnamwona amepotoka, hafikiri vizuri, ni mjinga au ananufaika moja kwa moja na serikali. Nijibu objectively, moja, ukiwa na kadi ya CCM unakuwa umetenda kosa gani? Mbili kwakupiga kura, unakuwa umevunja sheria gani ya nchi? Tatu, kipi kinakufanya udhani mawazo yako ya no reform no election ndio mawazo bora kuliko no election no reform?
 
Ahadi ya katiba mpya ndio imekukera hivi? Kwani kwenye No reforms No election unadai nini?
Kwani kwenye uchaguzi wa mwaka 2019,2020 na 2024 kwenye serikali za mitaani nn kinaendelea hadi NO ELECTION NO REFORMS isiwe kitu cha maana kwa watanzania.
 
Tutabaki na kura zetu na kuzilinda kwa wivu mkubwa,
Kwa nini nipoteze muda wangu kupanga foleni ya kupiga kura wakati najua kabisa kuna majizi yanaivizia kura yangu waiibe
 
Changamoto kubwa ya nyinyi wenzetu ni kuwaza kuwa mnayo hati miliki ya usahihi wa mawazo. Mtu asipoamini katika mnayoyaamini nyinyi mnamwona amepotoka, hafikiri vizuri, ni mjinga au ananufaika moja kwa moja na serikali. Nijibu objectively, moja, ukiwa na kadi ya CCM unakuwa umetenda kosa gani? Mbili kwakupiga kura, unakuwa umevunja sheria gani ya nchi? Tatu, kipi kinakufanya udhani mawazo yako ya no reform no election ndio mawazo bora kuliko no election no reform?
Nendeni mkachaguane muibiane wenyewe kwa wenyewe
Hatuna muda wa kupoteza
 
Katika siasa, kaulimbiu na propaganda ndizo karata zinazounogesha mchezo wa uchaguzi. Kila mshindani wako anapochanga karata zake, timu yako lazime ichange karata zako. Hiki ndicho kilichotokea kuelekea October 2025.

Wakati CHADEMA wanaendelea na campaign ya No reform no election, CCM wamekuja na ilani ya uchaguzi inayoahidi katiba mpya ambayo kimsingi ndio reforms zinazodaiwa. Kwa lugha rahisi hili ni tamko thabiti kuwa, MKITAKA REFORMS, MKAPIGE KURA.

Sasa mpira upo kwa wapiga kura, kuhusu njia gani waitumie kupata reforms, kwa kushiriki uchaguzi kama wanavyohimizwa na CCM? Au kwa kuzuia uchaguzi kama wanavyohimizwa na CHADEMA. Nachelea kusema kama mnayo nia thabiti ya kuleta mabadiliko ya katiba, basi njia rahisi kati ya hizi ni kuchagua CCM.

Kwa faida ya wasomaji, Misingi na Malengo Kuu ya Ilani 2025-2030 ni kama ifuatavyo:
1. Kuendeleza Uchumi wa Viwanda na Biashara Ndogo (TEHAMA)
Kuimarisha mazingira ya biashara na kukuza uwezo wa viwanda vya ndani, pamoja na kuwawezesha wafanyabiashara wa TEHAMA kupitia mikakati ya kifedha na kiutawala.

2. Uboreshaji wa Huduma za Kijamii Vijijini
Kupanua upatikanaji wa maji safi, huduma za afya, elimu bora, na nishati kwenye maeneo ya vijijini kwa kuzingatia ufanisi na uendelevu.

3. Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Kupanda miti milioni 100 kila mwaka ili kudumisha misitu, kudumisha mazingira, na kuongeza mvua .

4. Kuimarisha Diplomasia ya Kiuchumi na Usalama wa Taifa
Kukuza ushirikiano wa kimataifa, kulinda rasilimali za taifa (gesi, madini, misitu), na kuimarisha usalama wa ndani na nje.

5. Katiba Mpya ya Muungano
Kwa mara ya kwanza, Ilani ya CCM imeipa kipaumbele kuongoza mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano ndani ya miaka mitano ijayo, ikilenga kujibu mahitaji ya kisasa kijamii, kiuchumi, na kisiasa
No reforms no election. Huu ujinga kajadili na mkeo usituletee huku
 
That's very good..

Umekuja precisely kutaka hoja, basi tutakupa hoja japo, from my persective najua kabisa kuwa unaelewa tatizo la chaguzi zetu liko wapi lakini unajifanya hamnazo tu...

It doesn't matter, kwamba, pamoja na kujifanya "mjinga", we will teach you as much as you want, mpaka ukiri kwa kinywa chako kuwa - NIMEELEWA...
Changamoto kubwa ya nyinyi wenzetu ni kuwaza kuwa mnayo hati miliki ya usahihi wa mawazo.
1. Sio kweli. Hiyo ni dhana yako tu na kutojiamini kwako kwa sbb unajua kuwa wewe na CCM yenu huko hamna hoja kabisa za kutetea uhalali wa ushindi wenu ktk chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1995 ktk maswala haya...

2. Wazo sahihi ni sahihi tu, na wazo la kijinga ni la kijinga tu. Na usahihi au ubovu wa mawazo unapimwa kwa hoja kuhusu kinachojadiliwa. Mawazo yako yakiwa hovyo, hayajibu hoja basi automatic, yanakuwa ni upogo na ujinga tu kwa yeyote anayepima!
Mtu asipoamini katika mnayoyaamini nyinyi mnamwona amepotoka, hafikiri vizuri, ni mjinga au ananufaika moja kwa moja na serikali.
Wewe huamini nini na sisi tunaamini nini kwa ulinganifu?

Hoja zako ni zipi ambazo unazipima kutoka kwenye hoja zetu ili tukuamini?
Nijibu objectively, moja, ukiwa na kadi ya CCM unakuwa umetenda kosa gani?
Hakuna kosa...
Ni haki yako kuwa mwanachama wa chama chochote...
Na wewe nikuulize, kuna ubaya gani kuwa mwanachama wa kadi ya CHADEMA? Kuna kosa hapo kisheria? Why are harrasing, torturing and putting them in custodies just because of their dissent opinions against the govt..? Why..? Una hoja kwenye hili..?
Mbili kwakupiga kura, unakuwa umevunja sheria gani ya nchi?
Hakuna..
Na kutokwenda kupiga kura kwa kuwa unajua kuwa kura yako haitahesabiwa na kuhesabika kwa kiongozi uliyemchagua badala atatangazwa ambaye hukumchagua ni kuvunja sheria gani?
Tatu, kipi kinakufanya udhani mawazo yako ya no reform no election ndio mawazo bora
Kwa sababu;
1. Uchaguzi HURU, wa HAKI, wa WAZI na KUAMINIKA Tanzania kwa sasa haiwezekani. Ushahidi ni chaguzi za 2019, 2020 na 2024


2. Electoral system ya Tanzania ni presidential (inadhibitiwa na Rais aliyeko madarakani) ambaye huwa ni wa chama kishiriki pia ktk uchaguzi na huyo Rais akiwa mgombea kupitia chama chake. Mfano, Rais ndiye anateua wasimamizi wa uchaguzi wote kuanzia kwenye vituo vya kupigia kura hadi Mwenyekiti wa Tume yenyewe na Mkurugenzi wa uchaguzi. Sasa ktk scenario hii, kwanini asijipendelee yeye na wagombea wengine wa chama chake? Kwanini asiwafanyie mtima nyongo washindani wake wa vyama vingine? What happened 2019? 2020? 2024?
√ Do you know that 96% ya opposition candidates in 2019 local gvt election walikuwa disqualified using baseless grounds?
√ Na unajua kuwa ktk uchaguzi mkuu wa 2020 wa Urais mpaka leo matokeo ya kura ya urais jimbo kwa jimbo hajatangazwa?
√ Si unajua kuwa, Magufuli/Samia walitangazwa tu randomly kuwa wameshinda lakini huwezi ku - verify ushindi wao popote..?

3. Tunahitaji referee aitwaye "Tume Huru ya uchaguzi" hapa Tanzania. Rais awe mbali kabisa na huyu refa...

4. Tunahitaji matokeo ya kura ya u - Rais kama yana utata na wagombea wengine hawajaridhika, basi waende mahakamanj wahoji. Hii itaepusha mtu kutangazwa tu bila verification yoyote ya uhalali wa kura za ushindi wake..!

5. Tunahitaji usawa wa mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi kwa uwakilishi wa wabunge kwa kigezo cha idadi ya watu (ambao ndio wanaokilishwa). Mfano, inawekana vipi jimbo lenye wapiga kura 5,000 liwe na mbuge mmoja sawa na jimbo la wapiga kura 450,000+? Hii wewe inakupa maana gani ukiona mgawanyo wa majimbo kwa namna hii?
kuliko no election no reform?
√ Mimi ninataka tufanye mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kwanza ndo twende kwenye uchaguzi ambayo ndiyo maana ya NO REFORMS NO ELECTION..

√ Hili la NO ELECTION NO REFORMS ni la kwako, wewe ndiyo toa sababu zako..
 
Siku utakapojifunza kutofautisha agenda na personality utakuwa umepevuka kwenye siasa. Siasa sio mapenzi, kwamba unachagu wako na kukubaliana kufa na mapungufu yake. Siasa ni jukwaa la kujadili maswala yahusuyo maisha ya watu wetu. Hoja nzuri inachukuliwa nakutelekezwa bila kujali imetolewa na nani? Dr Slaa ali-campaign kutoa elimu bure akiwa anagombea urais, ingawa mwanzo CCM walisema haiwezekani alipokuja JPM alitekeleza. Hiyo ndio siasa yenye tija.
1. Sasa ndugu Dr Adam Francis, hivi kweli unaweza kumtofautisha mtu kwa kile asemacho (ajenda/hoja) na personality yake?

2. Kama siasa ni maisha ya watu, kwanini huko CCM mnatumia ulaghai wa kisiasa kulaghai/kuwadanganya watu wanyonge wapiga kura?

3. Kwanini CCM mnafanya manipulative politics, kuiba kura, kuiba uchaguzi, kuteka na kuua watu unaosema "siasa ni maisha ya watu lakini mnawaua" ili kubaki madarakani? Hizi ni siasa au ujangili wa kimadaraka?

4. Kwa ufahamu wangu mimi, siasa ni consensus au mapatano ya hiari (mutual agreement) kati ya viongozi na wanaoongozwa. Ikifika wakati viongozi wanajifosi kwa nguvu kwa watawaliwa kuwa viongozi na kuita hiyo ni siasa, basi utakuwa very wrong kwa kuwa hizo sio siasa bali ujangili kwa jina la siasa..!!
 
Mleta mada nina swali moja tu.

Je Tundu Lissu angekua ndio anateua mkurugenzi wa tume, mwenyekiti wa tume , wajumbe na makamishna wa tume na kikawepo kifungu ambacho kinaipa nguvu tume kwa maamuzi ya na matokeo kutopingwa mahakamani yoyote.

Je CCM mngeshiriki uchaguzi?
 
Back
Top Bottom