mkitaka kuongopa mjipange..

Negrodemus

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
2,316
677
Wanafunzi watano wa chuo kikuu
kimoja hapa nchini walikuwa
wanatakiwa wafanye mtihani siku
inayofuata. Wale wanafunzi
walikunywa pombe mpaka saakumi za
usiku,asubuhi ya siku ya mtihani kila mmoja alikuwa na uchovu wa
Hangeover hivyo walishindwa kufanya
mtihani.Wakatunga uongo wa kwenda
kumuongea Lecture wa somo husika.
Wakaenda kumuongopea Lecture
kuwa wameshindwa kufanya mtihani kwa sababu jana walikuwa kwenye
harusi na wakati wanarudi gari yao
ikapata pancha na wakavamiwa na
vibaka na kuibiwa pamoja na kupigwa.
Yule Lecture alikubali na akawapa siku
tatu za kujiwekasawa na kujiandaa na special exam.Siku ya mtihani wa Special
yule Lecture aliwapa mtihani na
aliwasimamia mwenyewe. Mwongozo
wa mtihani ulikuwa kama ifuatavyo,
1.Mtihani huu ni kwa wanafunzi
watano 2.Majibu yao lazima yawe sawa na yakiwa tofauti wote wanapata ziro
na wanafeli
3.Mtihani huu una maswali matano na
yote lazima yajibiwe. Maswali ya mtihani
yalikuwa hivi. 1.Harusi ilifanyika katika
ukumbi gani? 2.Gari mliomtumia mpaka mkapata pancha inaitwaje? 3.Ajali
imetokea eneo gani? 4.Nani alikuwa
dereva?
5.Tairi ipi ilipata pancha,ya mbele au ya
nyuma? NAWATAKIA MTIHANI MWEMA
 
We 've seen this thread before!

So..!
Kwan wote tulikuwepo?
Kwa hyo ka wewe ulikuwepo kipindi cha vita ya kagera ukikuta mtu au makala ya hyo vita utaiharibu au kumwambia huyo mtu kuwa mbona hvyo vita tumeviona, unataka watoto waliozaliwa 80,90,2000 waambiw na nan juu ya hiyo vita acha use...!
 
jamani this is the first tyme for me to read this thread nimechekaje? kama kibela baada ya kutangazwa mshindi wa milioni kumi na voda com ochinekeeeeee!
 
watu wengne sijui sijui wapoje ful ubinafs na kukatisha tamaa watu wenyewe wamekuja juz tu wanataka kutusumbua kisa wameona weng wao wanacomment hvyo njoo na style yako usikariri za wenzako kama kuna thred mnajua zipo waambie mods kabla ya kupost wawe wanazipitia bas ka ilikuwepo inatolewa ili wajue wao tu waliowai kuziona, hivi kwa thred zote zilizopo humu jamvin inawezekana ukasoma zote?
 
So..!
Kwan wote tulikuwepo?
Kwa hyo ka wewe ulikuwepo kipindi cha vita ya kagera ukikuta mtu au makala ya hyo vita utaiharibu au kumwambia huyo mtu kuwa mbona hvyo vita tumeviona, unataka watoto waliozaliwa 80,90,2000 waambiw na nan juu ya hiyo vita acha use...!

JF-Inawageni kila siku. Siwezi kumtukana! Sjui ana muda gani hapa jukwaani.
 
Back
Top Bottom