Waache watu wa Chato wajiletee maendeleo yao wenyewe kwa juhudi zao wakijua wanafanya nini na nini gharama ya maendeleo kuliko kuletewa maendeleo wasiyojua yanatoka wapi. Wazaramo ni watu wa asili ya Dar es Salaam. Hawa wangepaswa kuwa ndio watu walioendelea zaidi ya wengine wote Tz. Lakini kwasababu waliletewa kila kitu mlangoni hawakufanya chochote cha kujiendeleza, wakabaki wakifikiri kwamba maendeleo ni kitu cha kuletewa na wengine kama zawadi. Angalia leo hii wazaramo miaka 200 baada ya kuishi na waarabu, wajerumani, waingereza, wahindi na wapare, wachagga, n.k. bado ni primitive na wanazidi kuuza ardhi na kusogea mbali na jiji huko Mkuranga na kwingineko.