Mkijirekebisha Mtakaribishwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkijirekebisha Mtakaribishwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jan 24, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jan 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkijirekebisha Mtakaribishwa!

  Siku moja nilikuwa nimesimama sehemu fulani nikizungumza na mwenzangu mmoja. Akapita kijana mmoja. Nilikuwa nikimfahamu siku nyingi. Alikuwa ni kijana mwenye kupenda sana chama tawala; lakini alikuwa ana tatizo la akili.

  Alipotuona, alitutolea salamu, kisha akamgeukia yule mwenzangu akamwuliza, "Habari za siku nyingi Sheikh? Mko wapi siku hizi, mbona huonekani?" Yule mwenzangu akamjibu. "Habari nzuri kaka; kwani huna habari? Siku hizi nimehamua kuungana na mchwa naishi kwenye vichuguu, sitoki isipokuwa siku za Alhamisi tu!" Kusikia hivyo yule kijana ambaye ni mgonjwa wa akili aliangua kicheko, akacheka kwa sauti kubwa sana, kisha akauliza kwa kustaajabu, "Hizi ni habari kubwa! Hivyo siku hizi binadamu wanaishi na mchwa? Si ajabu hiyo!?"

  Naam, kweli hiyo ni ajabu! Hakuna binadamu anayeweza kuishi na mchwa.

  Juu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, bado mwanadamu hajaweza kukifanya kichuguu kuwa maskini yake. Ndiyo maana, hata yule mgonjwa wa akili aliona vigumu kuamini yale maneno ya mwenzangu, alipomwambia kuwa yeye siku hizi amehamia Kichuguuni.

  Lakini kisa hiki ni sawa na mazingira alisi ya nchi yetu na utitiri wa vyama vya upinzani, kila chama chajiona kuwa wao ndio binadamu na wenzi wao ni mchwa na ni kero na hawana haki ya kuishi na binadamu.

  Wanandugu, nilikuwa napitia pitia kwenye mitandao nikakutana na tovuti yenye kichwa cha habari kisemacho Utitiri wa vyama vya siasa wa nini?

  Nami nikapata swali badala ya kusema Utitiri wa vyama vya siasa wa nini? Nadhani suwala lingekuwa kujadili umoja wa kitaifa na kujiuliza ‘Utitili wa Wagombea Urais wa nini?’

  Nilichonacho kichwani kama kitawezekana kwa vyama ambavyo vinapingana na chama tawala ni kuwa... Wakutane viongozi wote wa vyama pinzani kisha waamue kwa sasa kuitisha kula ya maoni ya jumla kwa Watanzania wote wa vyama vyote pinzani kisha wahamue kuchagua at least wagombea wawili yaani mgombea atayepata kura nyingi ndio asimame kugombea na yule atakaye shika nafasi ya pili basi ndio hawe mgombea mwenza. Kisha kwa pamoja washindanishwe yule atakayesimamishwa na chama kilicho madarakani.

  Lakini ili linaonekana kama vile ni sawa kwa binadamu kuishi pamoja na mchwa kichuguuni. Kwa ufupi haiwezekani, je ni kweli haiwezekani!?

  Nakumbua msemo mmoja kutoka vitabu vya wa kihindu Satyameva Jayate, nan ri tam! (Ukweli hushinda, uongo haushindi). Haya ni maneno ya Vyan, mwandishi wa Mahabharata, moja ya vitabu vya kidini vya imani ya Kihindu. Hii ni kweli kabisa. Hata yule mwanamuziki, Peter Tosh, aliwahi kuimba na kusema: You can't fool the youth of today (huwezi kuwadanganya vijana wa leo). Lakini mbona vijana wetu wa Kitanzania kila baada ya miaka mitano wanadanganywa na kina Matata (soma: Mapinduzi ya Fikra), kulikoni!?

  Nakumbuka wakati ule wa Mfumo wa siasa wa vyama vingi uliporudishwa nchini mwaka 1992, chama tawala kilidai kutaka kusifiwa kwa kurudisha mfumo huo kwa hisani yake kutokana na kupenda demokrasia, maana ilidaiwa kuwa wananchi waliukataa mfumo huo kwa asilimia 80 (80%) ya maoni yao. Wakati si kweli… maana chama hicho icho wakati ilipokuwa TANU ndio walio futa vyama vingine na kubakia wao peke yao kwa kujiona kuwa ndio wenye haki ya kutawala. Maradhi haya haya ya kujiona kuwa hakuna wengine wenye uwezo yamevikumba vyama vingine vya kisiasa vinavyoitwa vyama kinzani (Pinzani). Chama cha TANU ambacho kilikuwa ndio baba na mama wa chama kilichopo madarakani hivi sasa, kinajivika sifa ya kuwa chama kilicholeta amani wakati si kweli.

  Amani hii haikutengenezwa na yeyote kutokea kwenye jukwaa la siasa. Wala haitokani na mikopo ya IMF au ruzuku toka nchi tajiri. Ni amani ya asili iliyojengwa na kudumishwa na mabibi na mababu wa nchi hii. Kama ulikuwepo uhasama baina ya wananchi wa makabila mbalimbali, mabibi na mababu hao walikwisha umaliza na kuwapatanisha wahusika ambao leo ni watani tu; wakutaniana katika misiba na sherehe.

  Juhudi na mbinu za wakoloni za kutaka kutumia dini na makabila ili waendelee kutawala nazo zilishindikana. Wananchi waliungana kwa dini na makabila yao, wakawang'oa wakoloni.

  Nayasema hayo kwasababu hivi sasa nchi yetu imo katika mfumo wa siasa za kidemokrasia, mfumo unaotoa haki kwa kila mwananchi kuamua kujiunga na kupigia kura chama akitakacho. Lakini kwa msusuru huu wa vyama, kwa kisingizio cha demokrasia, nasema hakika hatutofika mpaka tutakapokubali kuwa wamoja kama vile walivyozika tofauti zao Mababu na Mabibi zetu na kusaidia kupata uhuru wa nchi yetu.

  Ili suhala linawezekana sana kama kweli viongozi wetu hawa wana nia nzuri na nchi yetu. kama watashindwa kuungana sasa ni vipi wataweza kutuunganisha pale watakapopata madaraka? (in their dreams)

  Ushauri huu ni kwa kwa vyama ambavyo nimeweza kuvikumbuka navyo ni:


  • Civic United Front (CUF),
  • Tanzania Labour Party (TLP),
  • Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
  • National Convention for Constitution and Reconstruction-Mageuzi (NCCR Mageuzi),
  • National League of Democracy (NLD),
  • Democratic Party (DP), na
  • Demokrasia Makini
  • Chama cha Jamii (CCJ !?)
  • Jahazi
  Na vingine vyote ambavyo sikuweza kuvikumbuka

  Hii ndio demokrasia itakayowaweka madarakani Kama hamtaki demokrasia hii, mnataka nini basi?

  Nasema na nimesikika kwa maana ...Mkijirekebisha Tutawkaribisha!
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Divide and rule ndio mtindo wa chama tawala, hawataungana kamwe hao mpaka tuwe tumezinduka wakalazimishwa na wananchi, lakini viongozi kuungana sahau wana bei kila moja..ka muhogo kake
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  ......... Dah!!

  Nina wapangaji wengi ambao ni mchwa na nguchiro lakini sijawahi kupata mpangaji binadamu. Hata hivyo nawakaribisha biandamu wote wanaopenda kusihi kwenye KICHUGUU
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  ....kila chama chajiona kuwa wao ndio binadamu na wenzi wao ni mchwa na ni kero na hawana haki ya kuishi na binadamu... !
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wakiamua kujirekebisha na kuungana Mwezi wa kumi tutawakaribisha.
   
 6. t

  thesonofafrica Senior Member

  #6
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  ninaamini chama kina imani na falsafa.Ikiwa vyam hivi falsafa zake hazishabihiani.kuungana si suluhisho la kumkomboa Tanzania.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna falsafa nyingine kwa vyama vya kisiasa zaidi ya kutaka kukiangusha chama tawala na wao kutawala!?
   
Loading...