Mkeo ana bodaboda wake?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Ukisikia mama au dada anakwambia ngoja nitamtuma 'bodaboda wangu' basi ujue huyo Bodaboda wake ni bodaboda wake kweli kweli.

Ninamjua mdada ambae anamtuma bodaboda wake kumtolea hela Kwa ATM. Kuna mmoja aliniletea bidhaa nikatakiwa nimrushie zaidi ya 300,000, nikamwambia makato upande wako. Akaniambia basi acha 'namtuma bodaboda wangu'.

Bodaboda anaweza kumsubiri mdada aoge amalize ndo ambebe. Cha kushangaza bodaboda hawa ni wakali mno kama wana deal na vidume. Hawataki kupotezewa muda na mahesabu ya gharama wanakuwa makini but kwa wadada watapigishwa round kibao malipo kiduchu lakini 'watiifu na waaminifu' kupita maelezo.

Achilia mbali wale boda wanaokunywa na wake zetu au kuwafata bar wakiwa hoi ili wawalete nyumbani wakati huo we umesafiri kikazi.

Hii connection ya wamama na wadada na bodaboda si ya mchezo.

Nawauliza Wana JF, mkeo ana bodaboda wake?

1647243051649.png

 
Yap hiyo nimeiona sana, unakuta demu kaja kwenye kijiwe cha bodaboda kasimama takriban lisaa lizima anamsubiria bodaboda wake.

Mi nikamuuliza kwani huyo jamaa huwa anakubebaga bure? Kwanini usichukue hizi za hapa uwahi kuliko kuendelea kumsubiria huyo huoni kua unazidi kuchelewa

Akasema "Aah nimemzoea tu naogopa kubadilisha bodaboda mwingine naona anaweza niangusha maana huyu nimemzoea hakimbizi sana"
 
Yap hiyo nimeiona sana, unakuta demu kaja kwenye kijiwe cha bidaboda kasimama takriban lisaa lizima anamsubiria bodaboda wake.

Mi nikamuuliza kwani huyo jamaa huwa anakubebaga bure? Kwanini usichukue hizi za hapa uwahi kuliko kuendelea kumsubiria huyo huoni kua unazidi kuchelewa

Akasema "Aah nimemzoea tu naogopa kubadilisha bodaboda mwingine naona anaweza niangusha maana huyu nimemzoea hakimbizi sana"
Keyword nimemuzoea
 
Ukisikia mmama au mdada anakwambia ngoja ntamtuma 'bodaboda wangu'
Basi ujue huyo Bodaboda wake ni bodaboda wake Kweli kweli..

Nnamjua mdada ambae anamtuma bodaboda wake kumtolea hela Kwa ATM..

Kuna mmoja aliniletea bidhaa nikatakiwa nimrushie zaidi ya 300k..
Nikamwambia makato upande wako..
Akaniambia basi Acha 'namtuma bodaboda wangu'..

Bodaboda anaweza kumsubiri mdada aoge amalize ndo ambebe..

Cha kushangaza bodaboda hawa ni wakali mno kama Wana deal na vidume..
Hawataki kupotezewa mda ..na mahesabu
Ya gharama wanakuwa makini..but Kwa wadada ..watapigishwa round kibao malipo kiduchu lakini 'watiifu na waaminifu' kupita maelezo..

Achilia mbali wale boda wanaokunywa
Na wake zetu au kuwafata bar wakiwa hoi ili wawalete nyumbani wakati huo we umesafiri kikazi.....

Hii connection ya wamama na wadada na bodaboda si ya mchezo...

Nawauliza Wana Jf ..mkeo ana bodaboda wake?...
Hii mada ina maswali mengi hapa pengine linaongelewa suala ambalo ni zaidi ya bodaboda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom