Mke wangu namtongoza upya kila siku

Mke wangu namtongoza upya kila siku

ukimbile

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2015
Posts
212
Reaction score
55
Ndugu zangu ndoa yangu ina miaka saba na tumejaaliwa watoto wawili. Kabla ya kufunga ndoa alikuwa mtiifu na mnyenyekevu, baada ya ndoa mambo yamebadilika.

Nikirudi kazini namkuta kalala saa mbili tu anadai nimechelewa. Usiku nikilala wala hanigusi hata, nikiomba mechi anabana miguu, kwa mwezi nabahatisha mechi mbili ambazo zote ni counter attack.

Najiuliza hivi ndoa zote zipo hivihivi au ni mimi tu? Kwa sasa nipo kwenye harakati za kutafuta mchepuko ambao utanipa fleva ila sitaupa full mkataba.
 
Pole Sana, wengine ndio wapi hivyo. Wamemaliza.
 
Yaani maisha ya ndoa ni kuvumiliana...jaribu kuongea naye kwa upole anaweza kwambia tatizo linalomsumbua....hata mwanamke pia hamu ya mapenzi hupungua sio wanaume tuu
 
Kaeni chini mjadili tatizo ni nini, na mtafute suluhu juu ya tatizo la mkeo. Usije ukatafuta mchepuko hadi kieleweke na mkeo.
Ikishindikana muwajulishe walezi wenu wa ndoa watawasaidia
 
pole mkuu kama unasema kweli.

ndoa zina changamoto sana hasa kwa wanawake wanabadilika sana.
 
Kama SAA mbili unafika home kwa maisha ya DSM ni kwamba umewahi Sana kurudi. Hebu Sinza kurudi SAA sita za usiku huenda atakuelewa
 
mlivutwa na nn kufunga ndoa ?
Je ni Upendo, Kufunga ndoa au Tendo la ndoa?
Tendo la ndoa ndio kiini cha ndoa mkuu. Ni lazima akupe mzigo mkuu.
 
ukimbile

JF bana, siku hizi imekuwa Shigongo sana. Huu uandishi na maudhui kwa mtu mwenye miaka 7 ya ndoa na majukumu ya familia haviendani.,, inamaana mkuu umeoa badala ya ubongo kutanuka umeamua kusinyaa na kurudi nyuma kwenye utoto. This is cook issue. By the way labda utaje umri wako!!
 
Last edited by a moderator:
''kwa mwezi nabahatisha mechi mbili ambazo zote ni counter attack"

Very interesting
 
poleeee...ongeeni,unaweza kuta ye anafikiri unamchepuko tayari
 
Mkuu check hizo counter attacking techniques. Muda si mrefu utajikuta una kesi ya kujibu TAMWA!
 
Mwanangu mke ukimwandaa anapanua mwenyeweeeee. Kuwa kocha mshambuliaji, acha kutegemea counter attacks
 
Unaweza kumuona tatizo kumbe wewe ndo tatizo.
Wanaume wengine gubuuu afu akitaka mechi ndo anajichekesha mxiuuu na asubuhi hujaacha kodi ya Meza!

Hivi unajua kwamba kei Haina thamani siku hizi? Hivi Kuna m/ke mwenye akili timamu akambania mmewe? Nikija kuishi na Mke akibana tu simuulizii tena natafuta mwenzake basi.
 
ukimbile

JF bana, siku hizi imekuwa Shigongo sana. Huu uandishi na maudhui kwa mtu mwenye miaka 7 ya ndoa na majukumu ya familia haviendani.,, inamaana mkuu umeoa badala ya ubongo kutanuka umeamua kusinyaa na kurudi nyuma kwenye utoto. This is cook issue. By the way labda utaje umri wako!!

hujaelezea kwanini unadhani hii ni cooked issue
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom