Mke wangu kanitoroka kisa kubadili Dini

Mke wangu kanitoroka kisa kubadili Dini

Shaffihsiraji

Senior Member
Joined
Dec 15, 2018
Posts
160
Reaction score
120
Habari wana jamii forums mimi ni Kijana eg yangu
29 nilianza mahusiano na mwana Dada eg 26
Tulianzisha mahusiano mwaka 2015 tukiwa Dsm

Tulifanikiwa kupata mtoto wa Kike mwaka huo huo

Lakini kwa kuwa nilikuwa nataka kumpata anikunalie nilimdanya jina na
Dini yangu ili akubali

na sikujua kama nitaishi naye miaka mingi
Nilimwambia naitwa Rich
ni mkiristo ivo ikawa rahisi kuwa naye pia

Lakini kadiri muda unavyokwenda alikuja jua ukweli na nilimwambia anisamehe maisha yakaendelea

Nilienda kwao nikatoa Mahari nusu ila walijua Dini
yangu wakati wa Mahari 2016 na walinipokea

Yeye alipendelea sana kwenda kanisani na hakutaka kuwa mbali na Maombi

Ilifika kipindi anataka nimuoe lakini alitaka nimuoe kupitia Dini yake dhehebu Anglican

Nilimzungusha sana ila nilikuwa nampenda sana hata yeye alinipenda sana
Sijawahi hata ona mwanaume akipita pita kwake

Miaka niliyoishi naye imetosha kumuamini lakini kilichokuja kuleta tofauti ni Dini tu

Kuna kipindi nilienda nae kanisani kwao kwa mchungaji wake nikaomba anipe muda wa kufikiria ili swala la kubariki ndoa nikapewa muda wa kufikiria

Lakini haikutosha nikaja kuongea na Mke nikamwambia naona ubadilishe wewe au tukafunge ndoa ya Kiserikali hakunijibu ila alionekana kukasirika sana

Mwisho wa siku nilikuwa ofisini yeye anafanya kazi sehemu nyingine kwa hiyo tunatofautiana kurudi

Nilikuta kachukua vitu vyake tu kaondoka nikamtafuta akaniambia unavyoona ndo ivo nimechoka ruhusu maisha mengine yaendelee

Kwa kweli nilichoka sana niliumia mno ukizingatia alinivumilia sana kwenye shida nyingi nilizopita nae ila now sipo nae

Nilimtumia mesej na nikaongea nae pia kuwa nipo tayari kufanya ivo na nikaenda kwa mchungaji nikamwambia maoni yangu

Lakini yeye anasema hata ukija church siwezi rudi kwako lakini kwa moyo wangu najua ana hasira sana na mimi

Na kwao niliwaambia kuhusu kuondoka kwake pia
wakasema wataongea naye lakini hawakurudisha majibu sahihi

Sasa ndugu zanguni msinicheke kwa Mapenzi yangu ila naomba mnishauri je anaweza rudi nikamuoa nikienda church kwao? au ndo kama alivosema hata nikienda church kwao harudiani na mimi nitafute msichana mwingine wa kumuoa?

Naombeni ushauri ndugu marafiki
 
Badili tu dini Kaka Mimi mwenyewe nimepata mchumba wa kiislam anataja anifanye nibadilishe kutoka John niende kuwa Adinani..mapenzi Yana nguvu sikucheki ila kuhusu ye kukusamehe sijui ila we badili Kisha mfuate akizingua Basi sio case rudi kwa muhamad Kwanza sio dhambi kubadilisha dini Kama peponi utaenda utaenda tu bila kujali dini
 
Habari wana jamii forums mimi ni Kijana eg yangu
29 nilianza mahusiano na mwana Dada eg 26
Tulianzisha mahusiano mwaka 2015 tukiwa Dsm

Tulifanikiwa kupata mtoto wa Kike mwaka huo huo

Lakini kwa kuwa nilikuwa nataka kumpata anikunalie nilimdanya jina na
Dini yangu ili akubali

na sikujua kama nitaishi naye miaka mingi
Nilimwambia naitwa Rich
ni mkiristo ivo ikawa rahisi kuwa naye pia
NIMESIKIA SIKIA KUWA KUNA WATU WAMETUMWA KUZALISHA WANAWAKE WA DINI NYIGINE ILI KUONGEZA IDADI YAO. JE WEWE N MMOJAWAPO? KAMA KAGUNDUA IMEKULA KWAKO
 
Badili tu dini Kaka Mimi mwenyewe nimepata mchumba wa kiislam anataja anifanye nibadilishe kutoka John niende kuwa Adinani..mapenzi Yana nguvu sikucheki ila kuhusu ye kukusamehe sijui ila we badili Kisha mfuate akizingua Basi sio case rudi kwa muhamad Kwanza sio dhambi kubadilisha dini Kama peponi utaenda utaenda tu bila kujali dini
Wewe koma,tumia hiko kichwa vizuri kufikiri acha kufuata upepo na vijana mtakaopita hapa muisome post iliyo ktk link hapo chini muelewe kilichoandikwa humo dini haibadilishwi kwa sababu za kitoto toto eti mapenzi...ndo kitu gani hicho?

Badili tu dini Kaka Mimi mwenyewe nimepata mchumba wa kiislam anataja anifanye nibadilishe kutoka John niende kuwa Adinani..mapenzi Yana nguvu sikucheki ila kuhusu ye kukusamehe sijui ila we badili Kisha mfuate akizingua Basi sio case rudi kwa muhamad Kwanza sio dhambi kubadilisha dini Kama peponi utaenda utaenda tu bila kujali dini
Naona wewe na mtoa mada ni pipa na mfuniko
 
Sasa ndugu zanguni msinicheke kwa Mapenzi yangu ila naomba mnishauri je anaweza rudi nikamuoa nikienda church kwao? au ndo kama alivosema hata nikienda church kwao harudiani na mimi nitafute msichana mwingine wa kumuoa?

Naombeni ushauri ndugu marafiki

So kwa line hii umeshakubali kabisa kabisa kwamba uzi mwembamba wa wewe kuingia peponi (well nasema uzi mwembamba maana maisha wengi tunayoishi kwa sasa ni kudra tu kuiona hiyo pepo) umeshikiliwa na huyo mwanamke?
 
Usibadili dini kwa sababu ya Mapenzi Mungu akuepushe na Chetani anayetaka ubadili dini ya haki
Vijana siku hizi ni hovyo sana,kwanini wasitafutane wa imani moja mapema ili kuepusha rabsha kama hizi?

Huu ujinga wa kulia mapenzi mapenzi kizazi hiki unawa-cost sana.
 
So kwa line hii umeshakubali kabisa kabisa kwamba uzi mwembamba wa wewe kuingia peponi (well nasema uzi mwembamba maana maisha wengi tunayoishi kwa sasa ni kudra tu kuiona hiyo pepo) umeshikiliwa na huyo mwanamke?

Hapana sijashikiliwa ila nafsi inanisuta sana naona
sijamtendea jema katika maisha aliyoishi na mimi
 
mpka leo kuna watu wanateseka na mahusiano kisa dini?? imani hizi zakipuuz tulizoletewa??? asee kuna watu kwel mnateseka, mm mtu wangu nlmchana makavu kuwa sina dini japo wazaz wangu wana dini, so dini yake huyo mwanamke haiwez kuwa kikwazo kwangu maana nmempenda mm wala sio hiyo iman ambayo haitamsaidia kitu, kabla ya mengineyo ultakiwa kumpa somo la kujitambua ndpo mengine yafuate, dini ni tatzo sana ktk mahusiano haswa watu wasipo jitambua....poleee
 
Back
Top Bottom