Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

bobby dolat

Senior Member
May 18, 2015
167
263
Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.

Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?

Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?

Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?

Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?

Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.

Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.

Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?

Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.
 
Duh we kazi unayo ila wasiwasi wako nini kama ni binamu yako unahisi atakuchukulia mke amuaminiani na binamu yako kiasi hicho,kama vip muite mwambie unapataje mawazo kwenye mji wako kwani kakusaidia kujenga au anakulisha muite mwambie ndugu yangu apa kwangu sitaki moja mbili tatu awezi aende si kwako bwana kuwa mwanaume
 
Unamuonea wivu mdogo wake mkeo. Boss wewe ni hatari. Jokes!!

Mimi naona huyo jamaa amepata treatment nzuri sana ambayo labda hajawahi kupata katika maisha yake, mfn mazingira ya hapo home, upendo, vyakula, nidhamu, townlife, kuthaminiwa, uhuru nk. Sasa hivi vitu ni kama vinamfanya arudhishe fadhila, ama niseme kucompensate ili aonekane ni mtu wa faida, ndio maana utamuona ana give back upendo, anatamani afue, apike, aoshe vyombo nk. Hii yote ili asionekane mzigo hapo home na pia aonekane si lelemama. Ni wanaume wa mkoani hua wapo hivyo boss.

Pia nahisi mke wako anakujali sana kukwambia upunguze kitambi uwe kama hilo lijitu, hii ni kwa afya yako, ila kwasababu tayari umeshamchukia lijitu, unaona km vile upo insulted. Kiuhalisia mkeo yupo sahihi sana, jivunie boss kua na mke anaependa ndugu wa kila aina, km mkeo angekua hovyo hayo yote unayoyasema kuhusu hilo lijitu yangefanyika kwa siri mno.
 
ha hahahahaha kwanza hilo jitu lisipomgonga wife wako basi wengine wenye mwonekano wa hilo jitu watamla, fanya mazoezi ya kutafuta pesa kwa bidiii zaidi achana na likifua ila piga mazoezi kishikaji usipate magonjwa....

hilo lijitu liambie liache mazoea na wife hawa tunawaita wazee wa kutengeneza mazingira anaweza kuwagonga wote wa kike humo ndani kiutani utani tu kuwa makini... huwa hawatongozi yani ..

kama unaweza liambie hilo jitu lisepe tu mazoea hutaki jitu kubwa
 
Binam.....
Hivi ndio mambo gani ya kuja kunianika huku jf....
Kama uliona nakukera, kwanini haukuniambia tukiwa nyumbani, kuliko kunileta huku mitandaoni..
Basi sawa.
Leo ukirudi toka kazini, hauto nikuta hapa nyumbani kwako. Na nikifika kijijini nitamueleza shanga ambae ni mama yako, kwa yote haya ulivyo nitendea
 
Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa Anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta

Nimewaandikia kwa sababu, Huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwa sababu amevimba kifua anataka tumwone au?

Mke wangu na house girl wanafua nguo jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, Natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?

Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?

Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mm pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, Ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwa nn aseme sasa wakati hili jitu lipo?

Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili

Jumapili Nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa

Hivi unaendaje ugenini halaf unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?

Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka
Huyo mzee wa BALIMI we endelea na LITE
 
Si binamu yako, mwache tu akusaidie kula mkeo kuliko kwenda kuliwa na watu baki.
Hivi wewe mwanaume rijali kabisaaa, anakuja mgeni wa kiume kwako, anajifanya yeye ndo mtawala wa nyumba, anatembea na vichupi ndani ya nyumba yako, anatoa mkeo out alafu wewe umetulia tu kisha unakuja hapa kulalamika, wewe unaakili kweli. Kwambi mimi ndo mkuu wa nyumba, hata akija baba yangu kwangu anatakiwa awe chini yangu na afanye nitakacho mimi.
 
ha hahahahaha kwanza hilo jitu lisipomgonga wife wako basi wengine wenye mwonekano wa hilo jitu watamla, fanya mazoezi ya kutafuta pesa kwa bidiii zaidi achana na likifua ila piga mazoezi kishikaji usipate magonjwa....

hilo lijitu liambie liache mazoea na wife hawa tunawaita wazee wa kutengeneza mazingira anaweza kuwagonga wote wa kike humo ndani kiutani utani tu kuwa makini... huwa hawatongozi yani ..

kama unaweza liambie hilo jitu lisepe tu mazoea hutaki jitu kubwa
miss chaga unaongea kwa confidence inaonekana una evidence ya mzee m1 wapo wa kutengeneza mazngra tyar ashawah kutengeneza mazngra akakulamba . Eti "hawatongozagi hao" . Hii ni evidence tosha miss chaga wetu tayar ishamkuta .
Ndukiii . Manake nkikaa hapa miss chaga ataniua nlivomtobolea siri yke
 
Mhhhhhhhh ningekuwa mimi namfukuza tu maana ni nyumbani kwangu mfukuze au kama unahera kiasi furani kinachoweza kuwasafilisha kwenda sehemu yoyote ambayo mnaweza kupanga chumba hata siku tatu mnamuambia tu kwamba sisi tunasafiri kama linawafuata fanya lolote lile mmtoloke mfunge ndani
 
Back
Top Bottom