Mke wangu alibadilika baada ya kumfungulia biashara. Nifanye nini kuokoa ndoa yangu?

Dec 8, 2016
79
170
Habari za Jumapili wanajamvi.

Niende Moja kwa Moja kwenye mada inayoniumiza kichwa mpaka nakosa amani ya moyo kwa muda wa week sasa.

Mimi na mke wangu tangu tufunge ndoa huu ni mwaka wa tisa. Hatukuwahi kuwa na migogoro mikubwa ingawa mikwaruzano ile midogo ilikuwepo.

Sasa katika kipindi cha miaka sita ya ndoa yetu nilimuweka tu nyumbani sikutaka ajishughulishe na biashara yoyote. Mwaka wa sita wa ndoa yetu nilipata ajali ya pikipiki iliyopelekea mimi kuvunjika baadhi ya viungo vya mwili. Hivyo nilikuwa admitted Muhimbili hospital kwa muda wa kama miezi 3 kabla ya kuruhusiwa.

Kutokana na uwekezeji wangu kwa kipindi chote hiki wakati naugua hatukuwahi kupata Shida ya mahitaji ya nyumbani. Baada ya lile tukio nikajiuliza hivi ikitokea nimefariki Huyu mama ataishije na watoto wangu. Nikamshirikisha nimfungulie biashara ili aanze kujifunza mbinu za utafutaji. Nilipopona tukafungua biashara ya kufanya miamala ya simu na kuuza soft drinks jumla na rejareja.

TATIZO:
Miaka mitatu ya hii biashara imeanza kuniletea matatizo Kwenye ndoa. Wanaume wamekuwa wanapiga simu mpaka Jumapili Siku ambayo wanajua hafanyi biashara na mbaya zaidi kuna mmoja nilikuta SMS za mitongozo na wife alikuwa ameshaingia king. Sasa nilimtafuta yule kijana na kuongea naye ingawa alisema alikuwa hajui kama yule mke wa mtu tangu sasa hatomsumbua tena. Mke wangu yeye alijitetea kuwa alimwambia yule kijana kuwa yeye ameolewa lakini aliendelea kumsumbua tu.

Hivyo nilifunga biashara for a while nikitafakari nini cha kufanya.

NDUGU WA WIFE:

Hawa watu walianza kuongea maneno ya hivyo sana kuwa mimi sitaki maendeleo ya ndugu yao baada ya kuona sasa hivi ameanza kufanikiwa ndio nataka kumrudisha nyuma bila kuangalia kiini cha tatizo.

Wengine mpaka wakadiri kwenda mbali na kusema wao ndio walimpa mtaji niliwauliza ni kiasi gani cha mtaji mlimpa wanasema laki saba. Niliishia kucheka tu kwa sababu hiyo lakini saba haitoshi hata kulipia kodi ya hilo eneo kwa mwaka.

NINACHOOMBA:
Wadau ninachoomba kutoka kwenu ni mawazo jinsi gani niweze kuliweka hili jambo sawa iwe kwa kufunga kabisa biashara yenyewe au vyovyote vile ili mradi ndoa yangu irudi Kwenye amani kama Mwanzo. Mama mkwe amenikasirikia hivyo yeye sioni kama ni mshauri mzuri kwa mke wangu.

Mniwie radhi kwa maelezo marefu ila nitasoma kila comment ili niweze kupata suluhisho.

Ahsante.
 
Kwani hana namba ya biashara ( ya kazi) ambayo atakuwa anaizima akimaliza kazi ?
Asiitumie hiyo namba kwa matumizi yake binafsi..

N. B
Kama hiyo biashara inamlipa irejeshe mkuu
Hana namba ya biashara wakati tunaanza biashara hatukufikiria haya mengine. Hivyo iwapo tutafikiria kuendelea na biashara hili litazingatiwa.

Kuhusu biashara ni kweli inatulipa sana kwa sababu kupitia hapo tunalipia ada ya shule watoto wawili.

Nashukuru kwa mawazo mkuu.

Ahsante.
 
Hana namba ya biashara wakati tunaanza biashara hatukufikiria haya mengine. Hivyo iwapo tutafikiria kuendelea na biashara hili litazingatiwa.

Kuhusu biashara ni kweli inatulipa sana kwa sababu kupitia hapo tunalipia ada ya shule watoto wawili.

Nashukuru kwa mawazo mkuu.

Ahsante.
Sawa mkuu, kila la kheri
 
Mwanamke akiamua kufanywa hana kwamba ni vile anatoka kwenda kwenye biashara au kwenda market.

Biashara iendelee, mwambie aache tabia ambazo huzipendi
Well said, dhamira yetu ni Nzuri lakini inataka kutuharibia ndoa. Swala la kufanywa ni lengine ila kugundua ndio Shida. Afanywe lakini asioneshe ishara hizo mbele yangu.

Nimeshaongea yote hayo ila napata Shida kwa ndugu zake hawamshauri kurekebisha ndoa yake bali wanamfundisha kukaza ili aendelee na biashara yake.

So nitazingatia pia ushauri wako Mamndenyi

Ahsante
 
Waambie hao vijana hivi uwachimbe mkwara sana😁😁😁
Screenshot_20210819-141618.png
 
Mwanamke kama kuliwa ataliwaa tu tena boraa ashide kazini na Ukiweza dukua simu yake baada ya kumuonyaa asiposikia mkuu huyo hata Ukifunga Biasharaa umalayaa hata acha kamwee mzee pole sana huo ndo ushauri wangu...!!

Na ukimdukua ukakuta bado anachepuka bhasi huyo sikio la kufaa na kiufupi ni wa kufukuzaa akajifunze kwanzaa..
 
Mwanamke kama kuliwa ataliwaa tu tena boraa ashide kazini na Ukiweza dukua simu yake baada ya kumuonyaa asiposikia mkuu huyo hata Ukifunga Biasharaa umalayaa hata acha kamwee mzew pole sana huo ndo ushauri wangu...!! Na ukimdukua ukakuta bado anachepuka bhasi huyo sikio la kufaa na kiufupi ni wa kufukuzaa akajifunze kwanzaa..
Hapa nimeshamdukua naendelea kufuatilia nyendo zake bila kujua ingawa kuna rafiki yake nahisi ndio aliyemtafutia huyo bwana sasa hivi ndio anatumia simu yake.

Maana niliona SMS imetumwa akiomba simu ili awasiliana na huyo mtu.

Ahsante mzee wa kula tunda kimasihara.
 
Kuna amani na utulivu. Inawezekana ndoa yako haikuwa na amani ila ilikiwa na utulivu sababu hukujua tabia ya mkeo. Tabia haina uhusiano na kumfungulia biashara au kushinda nyumbani. Ifahamu tabia ya mkeo, fanya maamuzi kulingana na tabia yake. Kufuga mke ndani hakubadili tabia.
 
Mwanamke kama kuliwa ataliwaa tu tena boraa ashide kazini na Ukiweza dukua simu yake baada ya kumuonyaa asiposikia mkuu huyo hata Ukifunga Biasharaa umalayaa hata acha kamwee mzew pole sana huo ndo ushauri wangu...!! Na ukimdukua ukakuta bado anachepuka bhasi huyo sikio la kufaa na kiufupi ni wa kufukuzaa akajifunze kwanzaa..
Kabisaa ikishindikana mle tunda kimasihala , kanji leo kapita na mkeka wakoooo.
 
Hapa nimeshamdukua naendelea kufuatilia nyendo zake bila kujua ingawa kuna rafiki yake nahisi ndio aliyemtafutia huyo bwana sasa hivi ndio anatumia simu yake.

Maana niliona SMS imetumwa akiomba simu ili awasiliana na huyo mtu.

Ahsante mzee wa kula tunda kimasihara.
Mkute huyo rafiki yake mpige marufuku aache tabia mbovu, najua kumuacha mke ni ngumu aisee ukizingatia mna watoto dah! Em kaa na huyo mwanamke mzungumze maisha yalivyo na jinsi kipindi akiwa single mother itakuwaje?
 
Nimefanya hivyo mkuu. Nilimpigia simu huyo kijana nikaomba akae Mbali na wife na kama ni issue ya biashara azingatie muda wa kuwasilina.

Aweke Heshima kwa mke wa mtu.

Ahsante.
Wakanye mkuu vijana hawana adabu sana yakija watokea mabaya wanalaumu watu
 
Mkute huyo rafiki yake mpige marufuku aache tabia mbovu, najua kumuacha mke ni ngum aisee ukizingatia mnawatoto dah! Em kaa na huyo mwanamke mzungumze maisha yalivyo na jinsi kipindi akiwa single mother itakuwaje?
Huyu mama ni mtu mzima wamejuana hapo Kwenye biashara ila yeye ni hawa wanawake wa kiswahili.

Nimeshachukua namba yake natafuta muda niongee naye pia huyu mama.

Ahsante kwa ushauri mkuu.
 
Hapa nimeshamdukua naendelea kufuatilia nyendo zake bila kujua ingawa kuna rafiki yake nahisi ndio aliyemtafutia huyo bwana sasa hivi ndio anatumia simu yake.

Maana niliona SMS imetumwa akiomba simu ili awasiliana na huyo mtu.

Ahsante mzee wa kula tunda kimasihara.
Karibu fazaa hawaa kenge bilaa hivyoo watatuchezea sanaa yani utatunza mafala watakulaa tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom