Tegelezeni
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 268
- 124
- Thread starter
-
- #101
Mkuu kama ni hali nzuri kiuchumi mimi ninao zaidi ya huyo kaka yangu ambaye alikuwa ameajiriwa tu na hakuwahi kumiliki gari.Kwa hiyo umetamani mabaki ya hilo gari na mali nyingine ndio maana unajifanya umeshikilia mila!! loooo hebu uwe na haya kidume wewe! Unaonekana wazi huna upendo zaidi ya kutamani vya kaka yako, nyie ndio mnaowatamanigi shemeji zenu!
Acha bana, endelea kumtunza mke wa marehemu na watoto wake na umuheshimu kama shemeji; USIMRITHI na kumfanya mkeo.
sidhani kama kuna damu kati ya kaka yako na mkewe!ungesema watoto ningekuelewa!... lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee...
Sasa si ushasema alikuwa ni ke wa rafiki yakeKuna kijana namfahamu yeye alimlea Mke wa marehemu rafiki yake ambae alikuwa mjamzito, alijifungua na jamaa akalea mtoto na mama yake na akamsomesha mtoto hadi leo hii jamaa ana mke wake na huyo mke wa mareheu rafiki yake alishaolewa kitambo na amini usiamini jamaa hakuwahi tembea na huyo dada hata siku mojs!Kumbuka alikuwa mke wa rafiki tu, sasa wewe kaka yako!!!!!!!!!!!!Ebu acha uhuni bwana
Mke alishakuw amwili mmoja na kaka yangu, tayari ni damu yetu huyosidhani kama kuna damu kati ya kaka yako na mkewe!ungesema watoto ningekuelewa!
siku hizi nimeokoka na kuacha matusi otherwise ungenikoma
Huyo mke wa kaka yangu kanichagua mwenyewe kwa hiyari yake bila shuruti kuwa mimi nimrithi awe mke wangu.Cheeeee!!!Yaani izo mila potofu bado ipo!! Ebu acha ujinga wewe. Mpeni huyo mwanamke uhuru wa kuamua aolewe na nani na ivi hujui kuwa ni matusi kumuoa mke wa kakao?Na vipi kuhusu magonjwa!!! Lol!!Ebu badilikeni bwana
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.
Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.
Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...
Huyo mke wa kaka yangu kanichagua mwenyewe kwa hiyari yake bila shuruti kuwa mimi nimrithi awe mke wangu.
tatizo ni mke wangu hataki kuwa na mwenzie.
Mkuu kama ni hali nzuri kiuchumi mimi ninao zaidi ya huyo kaka yangu ambaye alikuwa ameajiriwa tu na hakuwahi kumiliki gari.
Mke wa marehemu mwenyewe ndio amenichagua nimrithi sasa tatizo liko wapi?
happiness win tamaa iko wapi hapo?Mlokole gani unatamani matapishi?
Sasa si ushasema alikuwa ni ke wa rafiki yake
Hiyo ni kesi tofauti ukifananisha na ya kwangu ni kama vile unanionea, mila zetu hazisemi tuwarithi wake wa marafiki zetu bali wake wa kaka au wadogo zetu tumbo moja.
Je huoni tofauti hapo?
hicho kikao cha familia na wewe uliyeridhia hovyoooooo
au mnataka mali za marehemu? Maana kama mna nia ya dhati mnaweza kumsaidia shemeji yako bila kumridhi... Tena kamati nzima ya ukoo mmeshindwa kuja na njia endelevu ya kusaidia zaidi ya hiyo?
Na huyo mwanamke kakubali umridhi? Au mlikuwa mnatamaniana kabla mumewe hajafa?
Anyway najiuliza tu
Temea chini rafiki yangu, hayo si mambo mazuri kusema hapa JF, mimi siwezi kumuua kaka yangu kwa sababu ya mkewe, mbona wanawake wapo wengi tu, tunachofanya ni kufuata matakwa ya mila zetu.Amekuchagua kwa sababu una mali! Kumbe hapo ni tamaa zenu tu, mila kisingizio. Mkeo ana kila sababu ya kuomba talaka, Mkuu kuna jambo limejificha hapo kati yako na huyo shemeji tena isiwe ikawa ndio sababu ya ajali ya marehemu!
Sasa mtandao na mila vinaingiliana vipi?
Kusoma haimzuii mtu kufuata mila na desturi za kwao
Mimi ni mmatumbi halisi hata kama nimesoma mpaka PHD niaenzi mila za kwetu
Mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga.
Ukoo na mwengine sitakueleza