Mke wangu hatimizi majukumu yake ya nyumbani ipasavyo

anakula bata sana, ataishi maisha marefu kuliko wewe, utakufa utamwacha, mwenzio anapumzisha akili na mwili havichoki wala kuzeeka na wewe unajichakaza. pole.

kosa kubwa ulilolifanya ni kumfanya awe mama wa nyumbani, tafuta hata mradi wowote asimamie, hajazaliwa kwa ajili ya ngono na kuzaa watoto kama ng'ombe, anatakiwa kufanya kazi ili hata leo ukidondoka asikimbilie kutafuta wanaume wengine wa kumlea kwa pupa, atakuja kupata limtu litaharibu hadi watoto wako, umeshindwa hata kumfungulia genge? mradi wowote hata wa kufuga kuku? mimi mke wangu ukimwambia awe mama wa nyumbani nahisi ndio utakuwa mwisho wa ndoa, manake anajishughulisha na huwa anapenda aweke kitu mezani. funguka.
Mwingine unampa mtaji hata wa laki5 lakini baada ya mda huoni anachokifanya yaani kapoteza zote na anakukopa umsaidie tena angalau laki8 sababu laki5 ya mwanzo ilikuwa ndogo,baada ya muda tena utaambiwa walau nikiwa na ml1 naweza fanya kitu cha maana,nasema wengi wa hao viumbe ni shida full stress hawajui wanataka nini kwenye haya maisha
 
Kabla ya kumuoa ulitumia muda gani kuchunguza vigezo unavyoitaji kwa yeye kuwa mkeo!! Je kuna mabadiliko tofauti na yale yaliyokupelekea kujiridhisha anafaa kuwa mkeo wa ndoa?? Ukiwa na majibu ya haya ni rahisi kupata jibu kama ulioa mtu sahihi kwako ama ulikurupuka!! Si rahisi kubadili tabia za asili za binti wa miaka 28 zaidi ya kukubaliana na hali hiyo...
 
Kiongozi pole Sana! Kuna kitu kimoja sisi wanaume huwa tunaambiwa/kufundishwa au ni mapokeo kutoka kwa wazee wetu kuhusu maisha ya ndoa au jinsi ya kuishi na mwanamke kwenye ndoa. Tumeshazoea au zoezwa kuwa kazi zote za ndani ni za mwanamke! Mfano tunategemea mwanamke akufulie nguo, apasi nguo nk. Sawa lkn ushawahi fanya hizi kazi ukiwa gheto? Wakati wa u bachelor? Ni time consuming halafu haviishi unazunguka tu hapo hapo mwisho wa siku unajikuta umechoooka!

Naanza na story yangu. Nikiwa na std 5 Mama yetu mlezi aliamua kutushirikisha watoto wote kazi za nyumbani. Watoto wa kiume tulikuwa wawili wa kike watatu. Kaka yangu alipewa kazi ya kufagia uwanja yeye alikuwa std 7 wakati ule. Mimi nikapewa jukumu la kuosha vyombo! Ikawa mchana ndo naifanya hiyo kazi. Wakati ule primary tunarudi nyumbani mchana kula halafu saa nane tunarudi tena shule. Huwezi amini nimeifanya kazi hiyo mpaka namaliza std 7. Kuna wakati nikiwa std 7 nilitamani Sana kuiachia lkn baba alikuwa haulizi mara mbili, hicho kibano ningekipata Cha maana. Nilipomaliza form six nikaja dar kwa Kaka mkubwa hajaoa na tulikuwa watatu, mie ndo mpishi na chores zote za jikoni. Happy napo miaka 2 huku napiga evening classes IFM. Hapa nilipata uzoefu mkubwa Sana Hawa Kaka zangu walinifundisha maujuzi ya mapishi ya haja.

Nilipooa nlijitahidi ku maintain Yale mapokeo ya mfumo dume, mwaka wa Kwanza haikuwa shida, tulipopata Mtoto ikawa shida Dada wa kazi hawakai, wanakimbia kukaa na Mtoto. Wife akawa anachoka Sana na yeye alikuwa housewife. Mwaka wa pili akawa ht kuniwekea chakula inakuwa shida, kufua ndo kabsaa ikawa Sasa nafadhaika nimeoa Nini tena? Kweli tulifarakana kwa issues ndogo ndogo tuu! Lkn Kuna siku nikiwa ofisini Kuna mtu alikuwa analalamika same issue, boss wetu alikuwa mmama mtu mzima akatuita akatuambia yeye akiwa Kama mwanamke na mke wa mtu hakuna kitu anafurahia km mmewe akimpikia chakula! Anasema mme wake siku za jpili huwa aningia jikoni na watoto wake wa kike wanatengeneza msosi mtamu kichizi.

Anasema huwa week yote yeye anawaza jpili tu, na akishakula anajikuta ana hamu na mmewe balaa hahh. Kilichotokea nikahamishia hilo zoezi home. Wife akashangaa nakusanya zana naanza mapishi, alishangaa Sana lkn nikamwambia km unachoka let me help kweli bana wiki mwezi ingawa sio kila siku nikaona ht kauli zake zinabadirika anaanza penda kampani yangu! Hasa jmosi akaomba niwe namtengenezea wali Nazi na roast ya kuku! Ikawa kila jmosi hao mabibo sokoni kwenda kununua mahitaji kitu ambacho mwanzoni hakikuwezekana. Baadae tukaanza kutoka jioni na Mtoto tunakaa sehemu tunapata mbuzi choma. Sasa hivi almost 14 yrs mpaka watu wanatuita mapacha maana huwa almost kila kitu utatukuta pamoja.

Kitu kingine mdau nnachokushauri jaribu kujua talent ya wife wako! Anaweza fanya Nini ili umpe nafasi huenda anaona hatimizi ndoto zake. Mimi niligundua wife anauwezo mkubwa wa kufanya connection za biashara kwenye kuuza/ kununua na ku bargain Bei. Nikitaka kununua kitu popote tunaenda wote halafu kazi inakuwa kwake. Yaani lzm tupate kwa Bei nzuri.

Halafu wanasema umeoa mke na si mfanyakazi wa kukuhudumia wewe! Sawa anawajibika kuwa kinara was hizo shughuli lkn huyo no mwenza wako kwa hizo kazi ndogo ndogo za nyumbani ikifika jioni anakuwa amechoka ht hamu na wewe hana tena, hasa ukichukulia ni kazi zinazojirudia rudia kila siku! Mwekee Dada wa kazi halafu jaribu kutafuta kutengeneza mradi utakaofanya muwe mnawasiliana mara kwa mara hence kuleta ukaribu na ari mpya kati yenu!

Yapo mengi lkn mwisho jaribu kuanza kidogo kidogo kuzitatua hizo kero mwenyewe km hajafuta vumbi chumbani wewe futa. Mimi mke wangu akishakula tu anasinzia hata kitanda hawezi tandika kwa hiyo Mimi hutandika najua huo ndo udhaifu wake, lkn mwambie akasimamie site mnajenga, au gari imeharibika ipo kwa fundi au Kuna crisis atafute polisi wa kusolve issue hapo utampenda! Chukulia hayo km ndiyo mapungufu yake Kiongozi!
 
Heshima kwenu ndugu zangu.


Mimi ninafanya shughuli zangu karibu sana na tunaposhi, lakin nikimwambia apike mchana aniletee chakula inakuwa adhabu kubwa sana kwake. Kwahiyo mara nyingi naamua kula kwa mama ntilie tu.
Mkeo anaweza kuwa na mtindio wa ubongo. Chunguza historia yake. Jaribu kumtisha kuwa utaoa mwingine akiendelea hivo uone reaction yake
 
Poleee..
Labda jaribu kua na dada wa kazi pia.
Kama hakua hivyo tokea mwanzoni,bas amejichokea tuu, kukaa tuu nyumbani kunachosha sana,unakua sort of depressed ivii.kila kitu unaona sawa tuu.
Inshort life la kua ndani tuu ya nyumba is like living with no purpose.
Pole,my 2 cents japo mie sio mwanaume mwenye ndoa.
Mama wa nyumbani anakuwa na mfanyakazi tena!! Sikatai lkn uwe umepiga hatua fulani katika maisha. Huyu mwanamke kwa haraka ni Mkeo ni katika wanawake na wavivu! Huyo ni wako jitahidi kumvumilia na kuendelea kumkumbusha na kumuonesha kuwa tabia zinakukera.
 
Back
Top Bottom