Mke wangu hatimizi majukumu yake ya nyumbani ipasavyo

yello masai

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
3,542
3,502
Heshima kwenu ndugu zangu.

Jambo likikukuta mshirikishe mwingine mwenye uzoefu, na mficha maradhi kifo humuumbua.

Naamini humu wapo wengi wenye ndoa na wazoefu wa changamoto mbali mbali,

Nimekaa nikatafakari sana nikaona bora nilete huku jambo langu hili ili nipate mawazo mapya.

Nimekuwa na changamoto kadhaa kwenye ndoa yangu, japo nimekuwa nikizichukulia poa lakin sasa naona ni wakati wa kuwa serious kidogo,

Ninaomba niorodheshe mambo kadhaa ambayo kwa upande wangu nayaona kama ni madhaifu ya mke wangu na niseme tu kuna baadhi nilishaongea nae lakin sijaona mabadiliko yoyote.

Mke wangu ana umri wa miaka 28 na mimi nina 33 na tumejaliwa watoto wawili mpaka sasa. Na mke wangu ni mama wa nyumbani (sio mfanyakazi).
Namshukuru Mungu mengi natimiza na hatujawahi kulala njaa.

Mke wangu ananishangaza kwa tabia ya uvivu aliyonayo,
Ni mvivu kufua nguo, tenga la nguo chafu linaweza kujaa na zaidi lakin nguo hazifuliwi mpaka umkumbushe. Na ukimkumbusha atafua lakin utakuta nusu zimebaki.

Mimi ninafanya shughuli zangu karibu sana na tunaposhi, lakin nikimwambia apike mchana aniletee chakula inakuwa adhabu kubwa sana kwake. Kwahiyo mara nyingi naamua kula kwa mama ntilie tu.

Mwili wake ni mzito sana, hajui kujiongeza katika mambo mengi madogo madogo, kitu kinaweza kuwa kipo sehem sio yake lakini hawezi kunyanyuka akakiondoa mpaka umwambie, hawezi kuona meza ina vumbi au TV akachukua kitambaa akafuta.

Huyu mke wangu suala la kuamka kitandani saa mbili au tatu asubuh kwake ni la kawaida.

Mbaya zaidi, huyu mwanamke hajui kuonesha mapenzi. Navyojua mwanaume ukirud kutoka kwenye mihangaiko unatarajia upokelewe vizuri na mkeo, lakini yeye unakuta kakaa tu kwenye kiti, hakupi ile hali ya kujisikia kama umerudi nyumbani umemkuta mke.

Mbaya zaidi huyu mwanamke ni mvivu hata kwenye kufanya tendo la ndoa. Usipomkumbusha mwenyewe mnaweza kukaa hata wiki mbili na wakati mwingine nikihitaji anagoma mpaka nitumie ushawishi wa hali ya juu au nguvu. Lakini kwa hili siku hizi nimeamua kumpotezea, siombi kabisa, nkishashiba nalala zangu. Mpaka akili inaniambia nitafute mchepuko niwe najipoza kidogo.

Kama upo kwenye ndoa naomba mtazamo wako, maoni na ushauri kuhusu haya yanayonikuta kama mwanachama mwenzako kwenye chama hiki.
 
Poleee..
Labda jaribu kua na dada wa kazi pia.
Kama hakua hivyo tokea mwanzoni,bas amejichokea tuu, kukaa tuu nyumbani kunachosha sana,unakua sort of depressed ivii.kila kitu unaona sawa tuu.
Inshort life la kua ndani tuu ya nyumba is like living with no purpose.
Pole,my 2 cents japo mie sio mwanaume mwenye ndoa.
 
Sina uhakika na hili ila naomba nichangie

Ni kwamba kama kuna uwezekano mtaarifu mama mkwe juu ya matatizo ya mwanae, iwe kinaga ubaga sana akuelewa. Au sijui utumie mshenga, miiko ya ndoa siijui i stand to be corrected

La msingi Mama mkwe awe someone decent usije kuyakoroga zaidi.
 
Kaa nae chini umkumbushe wajibu wake kama mke,mwambie kwa uwazi na upole yote anayotakiwa kufanya.Natumai atabadilika
Wakati mwingine msimamie afanye. Kwa mfano kufua, tenga muda toa nguo zote weka sehemu ya kufualia halafu mwite mfue wote.

Kuhusu kitandani nina hofu hata wewe hujaweka mazingira sawa kumfundisha unachotaka. Wanawake wengj hawana tuition ya ndoa, ukimwoa anza kumfunza unavyotaka awe.

Lakini, ndoa ndiyo taasisi kubwa zaidi duniani ambayo haijapewa wakufunzi bora kuijenga. Mjenzi ni wewe. Jitahidi, usikibali kushindwa haraka kiasi hiki.

You are too young to fail.
 
Heshima kwenu ndugu zangu.

Jambo likikukuta mshirikishe mwingine mwenye uzoefu, na mficha maradhi kifo humuumbua.

Naamini humu wapo wengi wenye ndoa na wazoefu wa changamoto mbali mbali,

Ni
Mkeo ni "pisi kali?" Au katokea "familia bora?"

Haya makundi mawili ni pasua kichwa saaana huwa yanaringia sana hizo sifa.

Sababu nyingine ni sometimes kabila lake au nature ya kwao.
 
Poleee..
Labda jaribu kua na dada wa kazi pia.
Kama hakua hivyo tokea mwanzoni,bas amejichokea tuu, kukaa tuu nyumbani kunachosha sana,unakua sort of depressed ivii.kila kitu unaona sawa tuu.
Inshort life la kua ndani tuu ya nyumba is like living with no purpose.
Pole,my 2 cents japo mie sio mwanaume mwenye ndoa.
he kumbe wewe mwanaume
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom