Mke wangu hataki kunisamehe. Nifanyeje?

Habari wakuu wa kaya..igweee
Nina account humu ila imebidi nifungue nyingine sababu tunafahamiana na baadhi ya watu humu na mimi ni mjuaji yani mbele za watu napenda kuonekana mwanamke hawezi kunipelekesha.

Mwanamke uliyeishi nae kwa muda wa miaka saba hawezi kukuacha kirahisi hisi hata kama unaemkosea vipi, kama umetumia mbinu zote kumrudisha imeshindikana wewe jua tu hakuwa na mapenzi na wewe kabisa!
 
Kama hautasema kosa ulilomfanyia basi inaonekana bado haujajutia kosa ulilomfanyia hivyo basi kusema kosa kisaikolojia ni sehemu ya kuponya majeraha yako ya moyo. Nakushauri kaa kimya kwanza muache na yeye ajitafakari hata miezi sita usimbuguzi naami baada ya kipindi mtapona majeraha yenu atakubali kurudi nyumbani chochode kujutia kosa ni sehemu ya msamaha
 
Inategemeana na alipoenda, Mwanamke anayeheshimu ndoa akiondoka anaenda kwa wakwe, yaani kwenu. Kinyume na hapo uwezekano wa ......... ni mkubwa.

Kama hayupo kwenu we endelea kukaa hapo ukisubiri msamaha, atakusamehe ndio maana ni mume na uwezekano wa kuolewa tena ni mdogo sana, ila sasa.
 
Ni aibu nilichofanya ila sihitaji mwanamke yeyote. Mke wangu nimeanza nae mbali sana tokea hatuna kitu. Siwezi kuruhusu tu mtu mpya kirahisi ana stahili kufurahia matunda ya nyumba sababu alikuwepo kipindi cha ku struggle
Aibu ipi bro, tuanzie hapo, in case huwezi kuisema hapa hebu njoo inbox, ntakuongoza vizuri mno na mtarudiana na mkeo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mwanamke uliye ishi nae kwa muda wa miaka saba hawezi kukuacha kirahisi hisi hata kama unemkosea vp,kama umetumia mbinu zote kumrudisha imeshindikana wewe jua tu hakua na mapenzi na wewe kabisa!
Mwanamke aishi na Mwanaume kwa miaka 7 harafu uandike hakuwa na mapenzi nae kuwa seriaus mkuu mtoa mada kwanza hakuandika nini kimetokea pamoja na kuja na Feki Id ni jinsi gani ametenda kosa mara nyingi kiasi nafsi inamsuta.
 
Shida inaanza hapa, kwanza haujasema umemkosea kitu gani hadi akafikia hayo maamuzi.

Pili na muhimu zaidi, inaonekana haujajutia kosa ulilofanya, hadi sasa naona kinachokuumiza zaidi ni kuachwa na yeye kuwa na mwanaume mwingine, najua itakuuma lakini usipokua makini ataliwa na unaweza usijue.

Ikiwa unaenda kwake kumbembeleza kama ulivyokuja hapa, itakua unaendelea kumtia hasira tu. Haunyeshi kabisa kwamba ulichokifanya kimekuumiza, unajutia na unadhamiria kutorudia tena.

Pia kumbuka yule nae ni binadam, anahisia, anasikia uchungu na anakwazika kama watu wengine, mpe muda. Usimzonge sana, mwachie nafasi. Ilimradi amekuruhusu kuwaona watoto, hapo ndio iwe mwanya wa wewe kuonyesha ulivyobadilika. Acha aone kwa vitendo sio maneno.

Ni hayo tu mkuu, pole sana.
 
Mtengenezee matatizo vibaka wapite na pochi na simu alafu kazini tafuta mtu amtie fitina la nguvu akikaa wiki mbili tuma vibaka nyumbani kwake aibee nguo na viatu vyote kama kuna hospital mnatumua ongea na doctor mtoto akiumwa hata na vimafua doctor amtishe mtoto ana mawazo yanayomsumbua anaweza pata tatizo kubwa mbeleni ahaa atarudii tu Mume ni kiongozi, mlinzi, mfadhili, mshaurii na muhudumiaji
 
Mwanamke uliye ishi nae kwa muda wa miaka saba hawezi kukuacha kirahisi hisi hata kama unemkosea vp,kama umetumia mbinu zote kumrudisha imeshindikana wewe jua tu hakua na mapenzi na wewe kabisa!
Usiseme hivyo. Hujui undani uliosababisha mwanamke kuondoka. Kuna mambo mengi siku hizi yanaweza mfanya mwanamke asirudishe moyo wake. Mfano ametishiwa kuuwawa, kamfumania na mwanaume mwenzie etc
 
Mtengenezee matatizo vibaka wapite na pochi na simu alafu kazini tafuta mtu amtie fitina la nguvu akikaa wiki mbili tuma vibaka nyumbani kwake aibee nguo na viatu vyote kama kuna hospital mnatumua ongea na doctor mtoto akiumwa hata na vimafua doctor amtishe mtoto ana mawazo yanayomsumbua anaweza pata tatizo kubwa mbeleni ahaa atarudii tu Mume ni kiongozi,mlinzi,mfadhili,mshaurii na muhudumiaji
We unachekesha Mwanamke akiamua kuvumilia udhaifu wa Mwanaume anavumilia na akiamua kuacha hata utumie malaika harudi tukishapenda sehemu nyingine kurudi ni ngumu.
 
Back
Top Bottom