Mke wangu hataki kunisamehe. Nifanyeje?

Allan Rwego

Member
Jul 25, 2021
20
100
Habari wakuu wa kaya.

Nina account humu ila imebidi nifungue nyingine sababu tunafahamiana na baadhi ya watu humu na mimi ni mjuaji yani mbele za watu napenda kuonekana mwanamke hawezi kunipelekesha.

Nimemkosea mke wangu wa miaka 7 ya ndoa. Miaka 7. Tuna watoto wawili. Amegoma kunisamehe ameondoka, naumia kuwaza kuna mwanaume anaweza kummliki.

Msinishauri nijikaze, siwezi siwezi siwezi kuona kuna mwanaume atakuja kuwa anatambulika kama baba au uncle kwa wanangu, nasema siwezi. Ameacha kila kitu nyumbani ina maana kuna mtu ataenda kumnunulia vingine au? Nimejenga ila sioni faida ya kuishi kama watoto wangu hawazunguki nyumbani hapa na kelele zao.

Siamini kuzaa nje ovyo ovyo najua madhara yake. Nifanyaje arudi mama Doreen wangu. Amenivumilia mno. Najisikia vibaya sana naishi kama mhuni tu nyumbani. Nifanyeje arudi. Nizeeke mwenyewe au mtu mpya hapana hapana.

Mtakaotukana tukaneni tu, nahitaji njia za kumrudisha.

Yupo kwao

Pia soma: Mke wangu amerudi nyumbani igweee
 

copernicucci98

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
877
1,000
Vuta subira tu mzee.. Hata yeye huko aliko, ndani ya miezi mitatu atakuwa ameteseka na kutokuwepo kwako---Sema atajidai dai kukaza, we utampotezea kidogo----Then atajileta.

As long as una watoto, hakuna la kuogopa. Labda kama yeye ndo main provider wa ndani ya nyumba yako, ikiwa hivi i can not guarrantee cz psycholojia ya hawa dada zangu wanaijua wenyewe wakiyapatia maisha.
 

Allan Rwego

Member
Jul 25, 2021
20
100
Vuta subira tu mzee.. Hata yeye huko aliko, ndani ya miezi mitatu atakuwa ameteseka na kutokuwepo kwako---Sema atajidai dai kukaza, we utampotezea kidogo----Then atajileta.
As long as una watoto, hakuna la kuogopa. Labda kama yeye ndo main provider wa ndani ya nyumba yako, ikiwa hivi i can not guarrantee cz psycholojia ya hawa dada zangu wanaijua wenyewe wakiyapatia maisha.
Huu ni mwezi wa pili tayari hana dalili kabisa ya kurudi tena ninamjua vizuri. Nani anampa sexual needs zake miezi miwili hii?

Watoto kanipa uhuru niwaone ila namtaka na yeye. Provider ni mimi mkuu ila ana kazi yake, anaweza kuishi.

Ninatuma hela anarudisha. Nyumba nimejenga mimi ila ni yetu sababu leo sipo wakukaa ni yeye na watoto. Hajawahi kukasirika hivi. Nifanye nini?????
 

Juandeglo

Senior Member
Dec 20, 2014
162
500
Una uhakika unajutia?

Una hakika unauhitaji msamaha na hautorudia?

Inaonekana vitendo vyako vilimchosha na vikasababisha majeraha ya moyo. Sasa ikiwa unajutia kweli je unaweza kusali??

Ushauri: Rudi kwa Bwana Mungu. Embu tulia muombe Mungu msamaha kwa makosa uliyofanya. Katika toba ndipo kuna msamaha wa dhambi.

Jisacrifice omba toba tena kwa kufunga ikiwezekana. Ulishaichezea ndoa kwa kutoiheshimu. (Ndoa na iheshimiwe na watu wote..)

Kaa katika machozi kwa Mungu. Then ukishasikia nafuu muombe Mungu amrudishe mke wako. Sasa huku unamuomba Mungu huku unamtafuta physically. Yani rohoni na mwilini. Mtafute tu. Msalimie, mjulie hali, kila unapomtafuta omba msamaha. Mwambie umejutia kweli.

Anza kumtongoza upya. So huku unaomba mbele za Mungu ili ambadilishe moyo wake, huku unamtongoza. Ulishamess up so maybe jaribu hii njia.,..na Mungu aendelee kukuelekeza cha kufanya.

Wapendwa tuiheshimu ndoa, tuipende ndoa...tumuogope Mungu wapendwa.

#goodweekpeople#
 

J.wawatu

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
354
1,000
Ukimuomba msamaha ndiyo unaharibu, huyo atakuwa Ana kazi na anaona anajiweza kuishi na wanawe,
wanawake wengi wenye kazi wakishazaa watoto wawili wanatamani kuwa single mother bila sababu za msingi.
Cha kufanya kuwa kimya na usimtafute hata kidogoo atajiona mjinga atarudi Ila ukizidi kumtafuta na kukuomba masamaha ndiyo kiburi kinamzidi.
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
53,695
2,000
Ni aibu nilichofanya ila sihitaji mwanamke yeyote. Mke wangu nimeanza nae mbali sana tokea hatuna kitu. Siwezi kuruhusu tu mtu mpya kirahisi ana stahili kufurahia matunda ya nyumba sababu alikuwepo kipindi cha ku struggle
Unatumia fake id umeificha, umetafuta fake yake tena bado unashindwa kufunguka!!! Utakuwa umefanya makubwa sana.....umemgegeda nani yake waifu????
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom