God bell
JF-Expert Member
- May 13, 2011
- 590
- 211
Kwanza niwatakie lunch njema. Kabla hatujaoana aliniorodheshea hobbies zake kama kusafiri, kuangalia tamthilia, movies, usafi wa ndani na mazingira ya nje, outing. Tumeingia kwenye ndoa mwaka wa 5 sasa hayuko interested na kitu chochote. Jumatatu hadi ijumaa yuko busy kazini. Jumamosi anaenda sokoni kufanya shopping. Jumapili kwenye ibada.
Nikimuliza ni wimbo gani anaupenda uwe wa dini au kidunia hajui manake hapendi kuangalia hata TV, hata taarifa ya habari huwa namlazimisha.
Hajui kujiremba anavaa kawaida sana. Nikimwambia outing anasema bora hiyo hela tununue chakula tupike hapa nyumba. Hata usafi wa nyumba sio wa kiviile saana.
Yeye akiona watoto wameoga wameshiba ndo starehe yake basi, hata kuwatembelea marafiki huwa namlazimisha.
Nimejaribu kumuliza hana jibu anaona kama namuonea na siyo kwamba anachoka sana iwe ndo sababu kwani msichana wa kazi tunae. Na sio kwamba tuna umri mdogo hapana, tulioana tukiwa na umri wa kuitwa mama na baba.
NISHAURINI NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU MKE WANGU