Mke wangu habebeki...

Huyo anajenga kwao na nafanya biashara zake ukirudi tu unapigwa kibuti, ushauri wangu kabla hujatuma hela mwambie akupe matumizi ya hela iliyopita lakini pia punguza kumtumia hela nyingi manake anajua unazo tu, au mwezi huu ukituma mwezi mwingine atumie mshahara wake, kwani mtoto si niwenu wote hata yeye anapaswa amtunze. Vinginevyo kama ulivyosema peleka mtoto kwenu mtumie pesa za matumizi mama yako. Ndo atatia akili.... watu wengi wanachezea maisha, dollar iko 1800 na ushee halafu analeta ubazazi kwenye pesa?
 
Kama umefikia kulalamika hapa jf maana yake hali ni tete.
Sipendi mambo ya kupeana devorce kwani unaweza oa mwingine akawa wa ajabu kuliko huyu.
Anaweza kurekebishika, pengine ni ushauri wa mashost tu.
Jaribu baadhi ya miezi mtumie hela kidogo kuliko hiyo tufanye dola 500.
Sababu ni kwamba kipato chako kimeshuka na hivyo umuombe ajitune aishi kulingana na kipato chenu.
Maamuzi atakayochukua baada ya hiyo hatua yatakuonyesha nini unatakiwa kufanya.
 
Niko nasoma nje ya Tanzania huku nifanya kazi katika company fulani nikilipwa mshahara dollar 1,800 kwa mwezi,najigharamia mwenyewe masomo yangu kwa 50% nyingine ni sholarship na gharama nyingine za maisha.
Nimeacha mke na mtoto mmoja nyumbani.mke wangu najitahidi kumtumia dollar 1,000 kila mwezi.yeye anafanya kazi katika shirika fulani Tanzania na anapokea mshahara kiasi fulani mara zote analalamika pesa ninayomtumia haitoshi imagine juzi nimetuma kwa exchange rate ya Tanzania alipokea kama Tsh,1,800,000 bado ananipigia cim na kunigombeza pesa haitoshi kwenye matumizi yake ya maisha na mtoto sasa jamani huyu ni mke au mzigo?nimemweleza hari halisi ya maisha ya huku haelewi naishi kwa kujibana ili kile kinachopatikana tukiserve lakini wapi.nahisi kama nilikosea kwenye uchaguzi au anafanyia nini hiyo pesa ya kila mwezi au anaamua kunifanyia ushenzi tu.nimemwambia kuna watu wanalia mchana na usiku wanakosa bahati kama hiyo lakini haelewi.ila ninafikiria kumchukua mtoto wangu akalelewe na mama yangu mzazi au nimchukue nihishi naye ..nahisi huyu mwanamke nimzigo tena haubebeki..nasiyo kwamba kuna assets za ndani ananunua nyumba hiko full hadi usafiri nilimpatia wa kutumia.

Jamani mke wa namna hii nimfanyeje?
Subhanallah! watu tunatamani wenza hata wa kuchangia elf 50 tu kwa mwezi na hawapo sembuse 1.8 mil na ana mshahara.

Huyo atakua anafanya matanuzi ya kufa mtu, na mashoga zake wamemtia ujinga kuwa mtu akiwa nje ana hela, heri ukose vyote lakini sio mke aliyekosa maarifa. Hiyo hela inatosha wewe kurud kukuta nyumba imeisha ndani ya mwaka. Amka kaka hapo hakuna mwanamke. Lea mwanao kwa mama kama ulivyosema!
 
Anakula nn cha thamani kiasi hicho,labda awe anajenga mkuu...vinginevyo chukua MTT kama bibi yake yuko kamkabithishe..
 
Mkuu save hizo pesa umri unaenda nguvu zinapungua hutoweza kubeba box uzeeni.Hizo pesa ungezichanga urudi nyumbani hata na trector uje ujiaajiri .
 
Subhanallah! watu tunatamani wenza hata wa kuchangia elf 50 tu kwa mwezi na hawapo sembuse 1.8 mil na ana mshahara.

Huyo atakua anafanya matanuzi ya kufa mtu, na mashoga zake wamemtia ujinga kuwa mtu akiwa nje ana hela, heri ukose vyote lakini sio mke aliyekosa maarifa. Hiyo hela inatosha wewe kurud kukuta nyumba imeisha ndani ya mwaka. Amka kaka hapo hakuna mwanamke. Lea mwanao kwa mama kama ulivyosema!
njoo tuunganishe chemistry new gal hata mke wa tatu sio mbaya eti..
 
Mkuu shtuka mapema kuna namna zamani niliwahi kuwa mkoani kikaz kwa miaka miwili mitatu hivi mke wangu alikuwa anafanya kazi na analipwa kama 400k mimi nikawa namtumia 500k kutoka mshahara wangu so inakuwa kama 900k hivi kwaajili ya matumiz yake na mtoto na anatumia mwez mzima bila kuniomba hela ya ziada huyu wako vipi au ndo mafuta yamepanda bei maana mimi sikuwa na usafir wakati huo???
 
Mtoa madaa km bado upo jamii forum tupe mrejesho
 
ni kwamba watu tumefikwa na ukomo wa kufikiri au. mambo mepese kama haya mpaka tutake ushauri na ni jambo linalojieleza na majibu yake ni mepesi 1.8mlion unaona ni pesa ndogo kwa mawazo yako mkuu
 
Tuma tu nyumba ya wazazi kamaliza sasa hivi anajenga yenu akikusumbua ujue mafundi wanamzingua hata mke wangu alinifanyia hivyo hivyo
 
Mkuu shtuka mapema kuna namna zamani niliwahi kuwa mkoani kikaz kwa miaka miwili mitatu hivi mke wangu alikuwa anafanya kazi na analipwa kama 400k mimi nikawa namtumia 500k kutoka mshahara wangu so inakuwa kama 900k hivi kwaajili ya matumiz yake na mtoto na anatumia mwez mzima bila kuniomba hela ya ziada huyu wako vipi au ndo mafuta yamepanda bei maana mimi sikuwa na usafir wakati huo???
ASA astuke nini?? Thread ya mwaka 2011 unataka astuke leo
 
Back
Top Bottom